DOKEZO Mwalimu Mkuu Shule ya Sekondari Daniel Ole Njoolay, amewafukuza wanafunzi Kidato cha 4 kwa kutotoa Tsh 70,000 ya kambi

DOKEZO Mwalimu Mkuu Shule ya Sekondari Daniel Ole Njoolay, amewafukuza wanafunzi Kidato cha 4 kwa kutotoa Tsh 70,000 ya kambi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hakika japo kwa sasa uchumi wa wazazi unaweza usiwe imara

Ila ikiwa hatashindwa kutoa 70K watengeneze mfumo wa kuchangiana yaani waweke target kuwa Kama watoto wapo 100 basi at least watoto wenye nafuu za maisha ambao hawatopungua 60 wali pie then wale 40 ambao familia zao hazijiwezi wawekewe mfumo wa Credit wasome kwa kudaiwa


Ila wakisema hizo kambi ni za wale watakaotoa hela cash tu basi itapelekea kuwanyima fursa wengine.
Huu upuuzi unaoitwa kambi ni njia ya kifisadi ya kuwapiga wazazi tuache kutetea ujinga.

Yaani ili mtoto afaulu anahitaji kuwekwa kambini kweli? Ndipo tulipofikia?

Yaani elfu 70 unaichukulia poa mkuu? Kama wewe unaimudu unadhani ni wazazi wote wenye uwezo huo?

Kama mzazi amempeleka mtoto shule za kawaida ambazo ada haulipi maana yake uwezo wa mzazi wa kumpeleka shule za kulipia hana.
 
Kama ni tatizo ni kambi mbona hao walimu hakuwekaga kambi enzi zao wakafaulu, Mana nina uhakika hakuna mwalimu hapo mwenye A ya fizikia na maths both levels.
Huu ni upigaji mbona watu wanasoma na wamefaulu bila ya kambi.
Kama ishu ni kambi basi makubaliano yawepo kuwa anatoa hela asipofaulu warudishe hela.
Iweje awachape wanafunzi kwani wao ndio wanaotoa hela.
Kumbuka ada ya ,20k ilikuwa kazi ikatolewsa
 
Toeni hela acheni kulalamika. Fanyeni kazi sio kuzaa tu mnashindwa kulipia watoto elfu 70 tu.
Watu hawakatai kulipa issue ziwe hizo gharama ziwe formal, sio zile mtu anaamka anasema kesho mje na ada ya fagio la mwalimu mkuu
 
Toeni hela acheni kulalamika. Fanyeni kazi sio kuzaa tu mnashindwa kulipia watoto elfu 70 tu.
Naona ambavyo elimu ama ukubwa hata nyumbani hujapewa elimu yoyote. Unajua Kodi inayokusanywa inafanya nini, ilitakiwa matibabu , elimu, maji mpaka umeme iwe free kwa Taifa tajiri Kama hili. Hata Russia wanafunzi wanasoma bure chuo kikii wao kazi yao ni kufaulu tu.
Kuna usafiri wa umma nauli ni ndogo mno.
Unachaji kwa 50k mwezi mzima wewe ni kusafiri unapotaka.

Iko ivi nchi yenye ustawi mzuri Haina haja ya kuumiza wananchi wake Mana wanalipa Kodi, inaonekana hujui Mana ya Kodi na inafanya nini. Mwishowe utasema kuwa Kila mtu ajijengee shule ama Barabara zake Mana unao uwezo.
Mpaka nyumba zinajengwa zinapangishwa kwa gharama nafuu kwa wananchi wake , unajua Mana ya cost sharing
 
Mwalimu mkuu wa Daniel Ole Njoolay Secondary School Mwanza amewafukuza wanafunzi wa kidato cha nne na kuwachapa viboko vitano, akiwaambia wafuate Tsh 70,000 kila mmoja kama hela ya kambi.

Kwani huu utaratibu wa kambi ni upigaji mpya ulioanzishwa na wakuu wa shule wakishirikiana na viongozi wa wilaya.

Tunakuonya na huu uwe ni ujumbe kwa walimu wote nchini: Acheni mara moja tabia hiyo, kwani Tsh 70,000 kila mwezi ni hela kubwa mno kwa wazazi.

Hawawezi, na mtaongeza idadi kubwa ya watoto wa mitaani.
Hivi Daniel Ole Njolay yuko wapi huyu muheshimiwa
 
Kama ni makubaliano toeni hizo pesa ili shughuli ziende ,hizi siasa zinawafanya kuwa wajinga .Toeni pesa mambo yaende
 
Kama wazazi walikuwa wanashindwa kulipa ada ya 20,000 kwa mwaka mzima hadi kufikia serikali kufuta ada hiyo sasa hao walimu njaa kali sijui ni uelewa finyu wanakuja na upuuzi wa kuchangisha wazazi elfu 70.

Serikali ilifuta ada ili watoto wote wamudu kwenda shule halafu wanatokea wapuuzi wanaanzisha ada mpya kwa mgongo wa michango.

Wazazi kwa umoja wenu nendeni hapo shuleni mkamueleze aache mara moja upuuzi huo kabla hamjafikisha taarifa kwa waziri husika akachukuliwa hatua stahiki.
 
Hakika japo kwa sasa uchumi wa wazazi unaweza usiwe imara

Ila ikiwa hatashindwa kutoa 70K watengeneze mfumo wa kuchangiana yaani waweke target kuwa Kama watoto wapo 100 basi at least watoto wenye nafuu za maisha ambao hawatopungua 60 wali pie then wale 40 ambao familia zao hazijiwezi wawekewe mfumo wa Credit wasome kwa kudaiwa


Ila wakisema hizo kambi ni za wale watakaotoa hela cash tu basi itapelekea kuwanyima fursa wengine.
Sasa mtu kama hawezi kumudu elfu 70 kwanini anazaa?
 
Kuna wakati baadhi ya walimu vilaz,a kama huyo anayemuadhibu mtoto kwa kutotoa mchango wa 70,000 ndiyo wanasababisha walimu wote kudharaulika na jamii.

Sasa mtoto anatoa wapi fedha ya mchango hadi umuadhibu?

Mbona ni vitu vya kipuuzi sana hivyo wakuu. Halafu utakuta kuna mtu anatetea upuuzi kama huo.
 
Fikiria kama Mkuu wa Shule hajui hata sheria/mwongozo wa utoaji adhabu mashuleni unaoweka wazi kabisa kwamba Mwalimu mkuu/Mkuu wa Shule anaweza kumuadhibu mwanafunzi viboko visivyozidi vinne tena kwa kosa la juu kabisa ambalo lingepelekea kufukuzwa shule.

Sasa kama anamuadhibu mtoto viboko vitano kwa kukosa fedha ya mchango ambao sio lazima vipi kwa makosa mengine atamuadhibu vipi?

Hii kada inajishushia heshima yenyewe halafu wanasingiziwa wengine kwamba wanaidharau kada hii.

Walimu fuateni miongozo na sheria mbalimbali za elimu kuonesha maturity yenu sio kuongozwa na mihemko mnajidhalilisha.
 
Ila waTz wa maeneo yanayoendelea ni shida kubwa sana
 
Washindwe kumuandaa miaka yote mitatu na nusu waje kumuandaa mienz minne iliyobaki ......upigaji tu
Huu ndiyo ukweli kabisa mkuu.

Eti mtoto anaandaliwa kambini miezi michache kabla ya mitihani na mzazi bogus kama huyo anayesema eti wanaandaliwa naye anaunga mkono upuuzi huu.

Mtoto anaandaliwa tangu akiwa kidato cha kwanza ndiyo maana serikali iliweka ratiba ya vipindi vya masomo na mapumziko.
 
Kama ni tatizo ni kambi mbona hao walimu hakuwekaga kambi enzi zao wakafaulu, Mana nina uhakika hakuna mwalimu hapo mwenye A ya fizikia na maths both levels.
Huu ni upigaji mbona watu wanasoma na wamefaulu bila ya kambi.
Kama ishu ni kambi basi makubaliano yawepo kuwa anatoa hela asipofaulu warudishe hela.
Iweje awachape wanafunzi kwani wao ndio wanaotoa hela.
Kumbuka ada ya ,20k ilikuwa kazi ikatolewsa
Mazingira yetu ya miaka ya 1990s yalikuwa hayana destruction Kama mazingira ya Leo .

Unaweza ukawa unaongea Ila ni bora waangalie namna ya kuboresha wazo Lao Ila usililipinge .

Mimi nimewahi kufundisha na moja ya mawazo ambayo niliwahi kuyapendekeza ni kuhakikisha wanafunzi wanapokuwa wanaelekea katika mitihani ya mwisho wapate muda wa kukaa boarding ili kuwaongezea ufanisi .
 
Kuna wakati baadhi ya walimu vilaz,a kama huyo anayemuadhibu mtoto kwa kutotoa mchango wa 70,000 ndiyo wanasababisha walimu wote kudharaulika na jamii.

Sasa mtoto anatoa wapi fedha ya mchango hadi umuadhibu?

Mbona ni vitu vya kipuuzi sana hivyo wakuu. Halafu utakuta kuna mtu anatetea upuuzi kama huo.
wanakosa busara
Yani mwanafunzi asisome kisa kambi🤔
Aisee
 
Pamoja na Kambi utakuta kuna Zero
Kama itakuwepo basi ni ZERO WORKDONE
 
Mwalimu mkuu wa Daniel Ole Njoolay Secondary School Mwanza amewafukuza wanafunzi wa kidato cha nne na kuwachapa viboko vitano, akiwaambia wafuate Tsh 70,000 kila mmoja kama hela ya kambi.

Kwani huu utaratibu wa kambi ni upigaji mpya ulioanzishwa na wakuu wa shule wakishirikiana na viongozi wa wilaya.

Tunakuonya na huu uwe ni ujumbe kwa walimu wote nchini: Acheni mara moja tabia hiyo, kwani Tsh 70,000 kila mwezi ni hela kubwa mno kwa wazazi.

Hawawezi, na mtaongeza idadi kubwa ya watoto wa mitaani.
wazazi watoe hera za kambi waache visingizio,............ikiwezeka wauuze hizo baskeli watoto wasome tujenge taifa la kesho tuache visingizio
URITHI WA MTOTO NI ELIMU SIO MALALAMIKO.
 
Back
Top Bottom