Mwalimu Mwakasege: Corona ndio Tauni kwa mujibu wa Biblia

Mwalimu Mwakasege: Corona ndio Tauni kwa mujibu wa Biblia

Mwalimu Mwakasege amesema wanadamu wanapaswa kujihoji ni wapi tumemkosea Mungu kisha tutubu na kumrudia.

Mwakasege amesisitiza kuwa hii Corona siyo mpya bali ni ile Tauni iliyosemwa katika Biblia takatifu.

Mwalimu Mwakasege amesema hayo wakati wa semina inayoendelea huko Njiro Arusha na kesho ndio siku ya kufunga semina.

Source Upendo tv!
Anafunga saa ngapi hayo maombi








kush and Wisdom
 
Hawa matapeli kumbe bado wapo na kushindwa kuponyesha corona? Ona linavyopotosha , plague/Tauni inaletwa na bacterium Yersinia pestis , corona ni virus, wapi na wapi!
Bado utapeli umejichimbia kwenye vichwa vyao
Hujaelewa chochote, yani kiufupi katika haya mambo wewe ni mweupe kabisa kichwani!

Mwenzio kajikita kwenye ishu tafsri ya kibiblia ila wewe umejikita kwenye ushabiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mhhh, kwamba hakuna audience, ? jana nimefuatilia kwenye TV naona yupo kwenye Jukwaa ila camera imeelekezwa kwake mwanzo mwisho, Je ni kwamba kaenda uwanjani bila ya kuwepo watu au wameamua kutoonesha waumini waliokuwepo uwanjani?
Aache uongo. Spanish flu ilikuwa na rate kuwa ya kuua kuliko Coronavirus.
Watu mamilioni walikufa. Spanish flu pia ilikuwa tauni ?
Plague ni ndiyo tauni jamani.
Taun ni ugonjwa ambao unaua watu wengi kwa mda mfupi kwa hiyo hata Spanish flu ilikua tauni, shida moja watu wamekariri lakin inajulikana neno moja linaweza kuwa na maana Zaid ya moja lakin watu wanajifanya hawajui
 
mhhh, kwamba hakuna audience, ? jana nimefuatilia kwenye TV naona yupo kwenye Jukwaa ila camera imeelekezwa kwake mwanzo mwisho, Je ni kwamba kaenda uwanjani bila ya kuwepo watu au wameamua kutoonesha waumini waliokuwepo uwanjani?
Kwan haiwezekan yeye kuhubiri bila audience acha kukariri
 
Kwa mujibu Wa Mwl Mwakasege kama umesikiliza vizuri..alichosema ni kuwa kwenye biblia Tauni inamaanisha ugonjwa wowote unaoambukiza haraka na akalinganisha na Corona kwa sasa na bado ameongeza kwa kusema kuwa yeye anasimamia neno na si sayansi yetu hii ambayo ukitafsiri wote tutasema kuwa ni plague na organism ni Yersnia kama mdau alivyosema juu hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndio mwanafunzi msikivu(umeelewa)

Wengine wasikilizaji! Naona hawakuelewa alichomaanisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom