Mwalimu Mwakasege kufundisha katika semina ya Karismatiki ya Kanisa Katoliki jijini Dodoma 31/05/2022

So
Kwahiyo mkuu unataka kusema lilikua ni kosa kwa wanakarismatiki Jimbo la Dodoma kumpa mualiko Mwl. Mwakasege kufundisha hiyo juzi?

Nikukumbushe tu kua Yesu alivyokuja duniani hakuja kwa ajili ya watu fulani tu bali alikuja kwa ulimwengu mzima bila kujali dini sijui dhehebu...
Yohane 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Mkuu unaweza kusema sala ya dakika mbili tu ila nina uhakika itafanya mabadiliko makubwa sana kwenye maisha ya watu waliotoka kuokoka, na Mungu haesabu sijui huyu ameokokea kwa nani ila cha muhimu ni kuokoka!!
 
You see, hata wewe tayari kuna mafundisho yanaelekea kukutoa kwenye kweli. Mfano Mwakasege amesema pale ukiokoka unapigwa chapa right? Kwa andiko gani? Ubatizo ndio chapa na mlango wa Ukristo. Kumjua zaidi Mungu na njia zake ni swala la mafundisho sio kuokoka.

Vipi huoni Waislamu wanaoamua kuacha ya dunia ikiwemo ulevi na kuifuata kikamilifu dini yao waliitwa mbele kuokoka?

Kidogo kidogo utaanza kuacha kitubio, Ekaristi itakuwa ktk picha ya kilokole! Rozali utaiona ni ritual tu! Hii itakuingia kidogo kidogo

Sijasema asialikwe bali tuwe na muongozo ili kulinda tunachoamini. Mwakasege alipania ku promote ulokole! Angalia hekima ya mchungaji Kimaro jana! Hakuingilia msingi unaotutofautisha and he preached very well.
 
Kwahiyo wewe shida ni kuokoka tu?
 
Suala la MUNGU halihitaji elimu mnayoijua nyie makanjanja...elimu ya MUNGU anakupa yeye mwenyewe kwa kazi maalumu kupitia ROHO MTAKATIFU.
Yaani ukae tu ndani bila kusoma eti unasubiri Roho Mtakatifu akupe elimu! Ndio mnadanganywa hivyo hivyo kwamba kuna hela za miujiza
 
Mkuu kwani kuokoka ni nini? (Nini maana ya kuokoka?)
 
Hili kanisa katoliki inabidi libadilike bila hivyo litakuja kukosa waumini kabisa maana ndo kanisa ambalo waumini wake wengi wanakimbia baada ya kuisoma biblia vizuri.
Yaani wafuate biblia kama ilivyoandikwa na sio kama wanavoijua wao.
Nashauri mambo haya yafuatayo.
1. Waondoe masanamu na mapicha yote kanisani.
2. Mapadri na maaskofu waruhusiwe kuoa.
3. Watu waache kuungama kwa padri
4. Kuwe na huduma ya kichungaji na maombezi.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka
Asante. Lile andiko la atayeamini na kubatizwa ataokoka wanafikiri tunalipinga! Kila mbatizwa ameokoka maana tayari anachapa ya wokovu ambao anapaswa kuulinda hata mwisho kama ulivyonukuu. Tatizo tunataka kusimika namna mpya ya mtu kuwa Mkristo nje ya kuamini na kubatizwa!

Waulize waliookoka siku ile watabatizwa tena? Sasa kama hapana ni wokovu upi? Kuzaliwa mara ya pili ni kupitia ubatizo tu sio ile sala fupi na kuaminisha watu kuwa wameshaokoka! Baada ya pale akitenda dhambi lazima akafanye kitubio kama Mkristo mwingine yeyote! No exception!

Nimesema huko juu, hata nyakati za mitume wabatizwa wengine waliishi kinyume na wokovu waliopokea, wale hawakuambiwa waokoke kwa sala fupi bali waliungama dhambi zao na kufanya malipizi! Mkristo mbatizwa anapaswa kuhubiriwa jinsi ya kutunza wokovu wake na kama amekengeuka anarudia ahadi zake za ubatizo! Sio kuokoka! Hii ni myth iliyoibuka majuzi tu hata waanzilishi wa uprotestant kama Lutheran wanaushangaa!
 
Biblia ni sehemu ya mafundisho ya Kanisa! Biblia imekuja karne ya 4 tu na ni zao la Kanisa! Yesu alituachia Mitume ( Kanisa) na Roho Mtakatifu tu! Hakutupa kitabu kinachoitwa Biblia. BTW Biblia ni Catholic book inspired by holy spirit.

Biblia yenyewe hasemi popote kuwa Wakristo waamini yaliyoandikwa humu tu kama Quran! Biblia inakiri kupitia kitabu cha Timothy kuwa The church is the pillar and foundation of truth!

Mwenye authority of scriptures interpretation ni Kanisa na si mtu fulani!
 
Ni mali yetu. Kama hujui habari ndio hiyo. Wakatoliki ndio wakristo. Nyie wengine ni waasi tu. Ukidhani bibilia imekusanywa na nani Yani labda? Adui yeyote wa ukristo anadeal na kanisa la ulimwengu sio vijikanisa. Vimadhehebu.
Kwa hiyo Mbingu ni maalum kwa wakatoliki pekee?
 
Umeandika shairi refu sana ila All in all Wakatoliki wameokoka Tena maelfu kwa maelfu....

Wewe ni nani hata upinge....

Na Bado Moto unaendelea...na Sasa litakuwa linafanyika kila mwaka...
 
Unakuwa mbishi lakini hujasoma maandiko ni kweli ukiokoka unapigwa Chapa yaani Muhuri...baada ya wokovu unapigwa muhuri wa Roho Mtakatifu
Soma:-

(Waefeso 1:13-14)

Au unafikiri Mwakasege alibuni hayo maneno??
Unapompinga mtu hakikisha na wewe umesoma biblia na kuimaliza ili uwe na uhakika ya kwamba neno hilo ni la kutunga au ni Maandiko.
 
Yaani ukae tu ndani bila kusoma eti unasubiri Roho Mtakatifu akupe elimu! Ndio mnadanganywa hivyo hivyo kwamba kuna hela za miujiza
Mwakasege hajawahi kuwafundisha watu wasisome au wasipate elimu..Yeye mwenyewe ni Msomi na Amewahi kuwa Afisa mipango na Udhibiti...

Pia amewahi kuwa Mshauri wa Raisi kwenye sekta ya Uchumi...kipindi cha rais Mkapa...kamwe hajawahi kupingana na suala la kusoma..

hii ni yako tu umetunga..
 
Mpaka leo pamoja na technolojia ya kupata maarifa kukuwa bado kuna watu mnamuamn huyo mwalimu wenu wa uongo mwakasege?.[emoji16][emoji28]

Inauma ila ndio ukweli huo hakuna mwalimu, nabii, mchungaji wala mwinjilist wa kweli nyakat hizi maana wote wanatumia mafundisho ya uongo yaliyochakachuliwa na mkoloni.

Haijarish wanatumia maneno gan yanayogusa hisia zenu, lkn haiondoi ukweli kwamba hawana Roho wa kweli, bali roho ya mpinga kristo(ant-african spiritual reality),
mafundisho ya hawa walimu wenu yanatoka katika roho inayomiliki dini zote na kila aina ya imani na vitabu vyake

Huyo mtu wenu anawajaza sumu akilin ambayo ni ngumu kuiondoa ukishanasa, ni wengi tulikuwa wafuasi wa huyo mwalimu wenu wa uongo, lkn sasa tumeshazinduka ktk uo usingizi/kifo cha kiroho.

Mkoloni si mjinga kukupeni dini, eti ikukomboe for what? Kwa upendo gani?[emoji16], ukweli mchungu sana na unauma sana, zile siku ambazo ukweli utawekwa wazi tutakimbiana na wengi mtapata ukichaa maana yale mliyoaminishwa mtakuta ni uongo by100%..keep this komenti....
 
Ni mali yetu. Kama hujui habari ndio hiyo. Wakatoliki ndio wakristo. Nyie wengine ni waasi tu. Ukidhani bibilia imekusanywa na nani Yani labda? Adui yeyote wa ukristo anadeal na kanisa la ulimwengu sio vijikanisa. Vimadhehebu.
La kwako na nani wewe mmatumbi muabudu mizimu. Dini umeletewa lakini jinsi unavyoonyesha chuki dhidi ya wakristo wengine inaonyesha unaweza kuua. Umenifanya mpaka ni nimekufuru shenziii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…