Mwalimu, mwanafunzi wakutwa wameuawa ndani ya nyumba

Mwalimu, mwanafunzi wakutwa wameuawa ndani ya nyumba

Screenshot_20240402-144441_Opera%20Mini.jpg

Huyu hapa
 
Umasikini ni laana yahn mzazi unafika hatua ya kushindwa kukaa na binti yako unaruhusu akake kwa watu baki .....lakini pia uyo mzazi alikosa majina mpaka akampa mwanae jina la TATIZO.??
unaweza kuta mjini umeingia kwa hisani ya ndugu zako, ama ulisomeshwa na ndugu

haya kwa tanzania ni ya kawaida sana
 
Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbugani Kata ya Kiwanja, Herieth Lupembe na binti aliyekuwa akiishi naye ambaye ni mwananfunzi wa Kidato cha kwanza, Tatizo Haonga (16) wamekutwa wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mwilini.

Mauaji hayo yamefanyika ndani ya nyumba aliyokuwa wakiishi pamoja na mtoto wa mwalimu huyo mwenye umri wa miaka mitano.

Mwanafunzi aliyeuawa pamoja na mwalimu huyo alikuwa anasoma katika Shule ya Sekondari Isenyela wilayani Chunya.

Katika tukio hilo, Haris Daud (5) anayesoma darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kengold amejeruhiwa na sasa anapatiwa matibabu katika Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea jana Jumapili Machi 31, 2024 na majirani ndiyo waliobaini baada ya kutomuona mwalimu huyo akienda kanisani huku duka lake likiwa limefungwa, jambo ambalo si la kawaida.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Aprili mosi, 2024 jirani wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Merry Joel amesema walipoona duka limefungwa, waliamua kupiga simu ya mwalimu huyo ikawa inaita bila majibu.

“Tukaamua kufuatilia nyumbani kwake ndipo tukabaini kuwa ameuawa ndani kwake pamoja na huyu mtoto aliyekuwa anakaa naye. Mtoto wake tumekuta ameumizwa,” alidai jirani huyo na kuongeza;

“Tulipofika nyumbani kwake tulishtuka kukuta bidhaa za dukani zikiwa nje, umbali wa mita 50 kutoka nyumbani kwake na bidhaa hizo alikuwa ameziagiza kutoka mjini Mbeya.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, simu yake ya kiganjani iliita bila majibu.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbugani, Gideon Kinyamagohaamesema baada ya kupokea taarifa za tukio amewasiliana na Jeshi la Polisi na askari wamefika na kufanya uchunguzi wa awali kisha kuchukua miili kwenda kuihifadhi katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa uchunguzi zaidi na mtoto majeruhi amepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Mzazi wa mwanafunzi aliyeuawa, Faxson Simchimba amesema mwanawe alianza kuishi na mwalimu huyo baada ya kufaulu darasa la saba.

“Mwalimu alimchukua mwanangu ili aishi kwake kwa sababu ni jirani na shuleni alikokuwa anasoma, nini kimetokea hadi wameuliwa hata sijui,” amesimulia mzazi huyo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa wa Mbugani, Chambo Mpigauzi amesema hajawahi kusikia kama mwalimu huyo alikuwa na tofauti na mtu, bali alikuwa na uhusiano mzuri na jamii na ameshangazwa na mauaji hayo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Bosco Mwangindea ambaye ni Diwani wa Mbugani, amesema hilo ni tukio la kwanza kutokea kwenye kata yake.

“Hatujawahi kushuhudia mauaji ya kikatili namna hii, tunalaani vikali wote waliotekeleza mauaji haya na tunaliomba Jeshi la Polisi lifanye haraka uchunguzi,” amesema diwani huyo.

View attachment 2951481

Chanzo: Mwananchi
KIsu kama hiki unaanzaje kumdhulumu nafsi,ndio hivyo kila nafsi itaonja mauti mwingine atakufa kwa upanga,risasi,moto au baharini mradi maandiko yatimie pole sana kwa wafiwa!
 
Mkishapata kazi vijana mnajeuri sana,
Hivi huko kijijini, shule iko mbali, kuliko kumpangia bchumba binti mdogo kuna ubaya kukaa na mtu anaeeleweka?
Au we ndo umezaliwa na kukua mjini hufahamu maisha ya kijiji?

Ukute we ndo unalaana
Huyo jamaa hajielewi.. kwa maisha ya Kitanzania bila kusaidiana saidiana sidhani kama watu wengi wangefika waliko.
Kuna muda watu tumeishi mjini kwa mtu tunaetoka nae kijiji kimoja (hatuna undugu) ili tupate urahisi wa kusoma tution. Na tumesaidiwa mpaka tukamaliza shule.
 
Vifaa vya dukani havijachukuliwa....
Huo ni wivu wa mapenzi.. hapo Mwalimu mwenzie anahusika....na huyo binti aliyeuwawa ni kwa ajili ya kuficha ushahidi maana itakuwa aliwafahamu wahusika.
 
Mpumbavu unaejivunia ujinga.
Kwenye maisha OG ya Tanzania, kukaa kwa mtu baki au kuishi na mtu baki ni kawaida sana.
Pole sana junior ubinafsi utakuponza uzeeni.
Kuna sehemu shule ziko mbali kilometa hata 10
Bado point ya umasikini utabaki palepale na wabongo wengi tuna tabia mbovu ya kujifarji na umaskini....kama Shule iko mbali kwann mzazi asimpeleke mwanae Shule ya boarding???unadhani Kwa haraka haraka hakupenda au uwezo wa kumpeleka alikuwa hana???

Mtoto wa form one wa kike anaishi na mtu baki unajiridhisha vipi kama mzazi na nidhamu atakayojengewa???
 
Un
Bado point ya umasikini utabaki palepale na wabongo wengi tuna tabia mbovu ya kujifarji na umaskini....kama Shule iko mbali kwann mzazi asimpeleke mwanae Shule ya boarding???unadhani Kwa haraka haraka hakupenda au uwezo wa kumpeleka alikuwa hana???

Mtoto wa form one wa kike anaishi na mtu baki unajiridhisha vipi kama mzazi na nidhamu atakayojengewa???
Una utoto mwingi.
Pia hujui maana ya umasikini!
Ok junior!
 
Back
Top Bottom