Mwalimu Nyerere anaishi katika sura ya Magufuli

Nakuona umejikita katika suala moja tu la kuongea huku ukifumbia macho kabisa direction mpya ya kiuchumi ambayo ameianzisha Rais JPM. Nchi nyingi za kiafrika zimeanza kuiga mwenendo wa kiuchumi wa Tanzania.

Mwalimu Nyerere alitukomboa na kuwa nchi huru kisiasa. Lakini JPM anatuletea ukombozi wa kiuchumi.

Sasa basi unapojadili issue hizi ni muhimu kujadili katika context pana. Kwamba kwa wakati wake baba wa taifa aliweza kuipatia uhuru wa kisiasa nchi yetu. Lakini JPM yeye anatuletea uhuru wa kiuchumi.
Ukiwa na jicho la uhuru wa kiuchumi utaliona hilo. Lakini ukiwa bado umebaki katika mtazamo wa uhuru wa kisiasa utakuwa uneachwa na basi.
Ni jambo rahisi sana ni kubadili mtazamo na kuelewa kuwa tupo katika kipindi gani.
 
Mkuu pole kwa matusi uliyoyapata
 
huwezi kumfananisha Mwalimu Nyerere na vitu vya hovyo kama hivyo,
 
Nimeleta suala la kauli kwa sababu umejaribu kupindisha mambo kwamba Magufuli analeta nidhamu serikalini.

Mtu mwenye kauli za kishenzi hawezi kuwa analeta nidhamu.

Anaweza kuwa anatumia karata ya kuleta nidhamu kuogopesha watu na kuchukua point fulanikisiasa kwa watu wasiochambua mambo kwa kina, lakini kwa sisi tunaojua nidhamu ni nini, nidhamu inaanzia kwenye fikra na kuonekana kwenye kauli kwanza.

Kiongozi ambaye kashindwa kuwa na kauli nzuri, mwenye kauli za kishenzi, hawezi kujitapa kwamba anarudisha nidhamu.

Huko kwingine kote tunaweza kufika, lakini kwanza kubali hili.

Point yako ya nidhamu kwa Magufulini ya uongo, kwa sababu Magufuli kashindwa nidhamu ndogo tu ya kutumia kauli zenye staha za kirais.

Ondoa point yako kwamba Magufuli anarudisha nidhamu, tutaendelea kujadili mambo mengine.

Hakuna rais wa Tanzania aliyeudhalilisha urais kwa kauli zisizonidhamuwalastaha za kirais kama Magufuli.
 
Wikipedia siyo credible source.
Siyo credible source ya nini? Unajua nimeweka hapo kwa minajili gani?

Unajua naongelea nini hapo? Au unarukia tu mambo?

Unaelewa kwamba katika ulimwengu wa hyperlink nikikupa link ya Wikipedia sijakupa linkya Wikipedia tu?

Unaweza kukosoahata kitu kimoja katika Wiki hiyo? Au unapinga jumla tu hata kusoma huwezi?

Nikikupalinks za JSTOR na Lexis-nexis na Wall Street Journaluna subscriptions za kuingia?

Unajua hata JSTOR ni nini?

Kwa retort kama hizi, siwezi kushangaa unaposhabikia mtu kama Magufuli na kumfananisha na Nyerere.
 
Mkuu yapo mambo kila binadamu angetaka awe nayo,lakini sifikirii kuwa Raisi Magufuli angetaka kuwa Mwl.Nyerere by 100%au Mwl. Nyerere angetaka kuwa Magufuli by 100%
Kuna mambo Magufuli amefikia jawabu aliotaka Mwl.Nyerere lakini kwa kutumia njia tofauti.
Yapo mambo Mwl.Nyerere aliyahubiri sana,na kuyaandikia hata vitabu lakini aliambulia patupu,hakufanikiwa kwa sababu ya siasa za kubembeleza kwa mfano alisema kiongozi asiwe nyampara.
Lakini Raisi Magufuli yeye ni hapa kazi tu anataka magoli hana haja ya chenga nyingi za Mwalimu Nyerere.
Lakini wote walikuwa na common goal kwa wananchi wanyonge.
Kwa mfano maneno makali kwa matajiri kama haya aliyasema mwalimu Nyerere.
Mabepari,Wanyonyaji,Kupe,Mirija,Nyangau,Mabwanyenye.Na misemo ya Bw. Yesu kuwa ni ngumu tajiri kuingia ufalme mbinguni kuliko ngamia kupita kwenye tundu la sindano.
Nae Raisi Magufuli anasema Matajiri wataishi kama mashetani.
 
Ukiwa na jicho la uhuru wa kiuchumi utaliona hilo. Lakini ukiwa bado umebaki katika mtazamo wa uhuru wa kisiasa utakuwa uneachwa na basi.

Kwa hiyo tukiingia kwenye mapambano ya 'uhuru wa kiuchumi' tuache 'uhuru wa kisiasa'? Maana huko ndiko anakotupeleka Magufuli. Mimi hilo silikubali kamwe.
Ningefikiria kumsogeza kidogo karibu na Mwalimu kwenye juhudi za 'uhuru wa uchumi' kama asingeonyesha nia iliyo wazi, tena ovu ya kupora 'uhuru wetu wa kisiasa.' Hili limemwondolea sifa hiyo.
 
Hapa ndipo ninapokuja kusema kuwa ni mtazamo wako. Huo mtazamo wako hauondoi ukweli kwamba nidhamu kwenye ofsi za umma umeongezeka. Watu wanawahi kazini wanafanya kazi zao za kuhudumia wananchi kwa kiwango.
Huu ndio ukweli ambao unaonekana lakini wewe unaukana hadharani.
Wananchi hawahitaji maneno matamu ya kubembelezwa, wananchi wanahitaji services za uhakika. Wananchi wanahitaji maji, huduma hospitalini na huduma zingine za kijamii.

Tunaposema uwajibikaji ni kuhudumia wananchi. Mimi siwezi kubadili mtazamo wako lakini facts nitazieleza. Na baada ya hapo utaelewa kwanini nchi zingine Afrika zinaiga policy za JPM.

Mtazamo wako umeuekelekeza katika negativity thoughts so ni vigumu sana kukufanya uone chochote maana tayari umejiwekea msimamo mwenyewe. Lakini kama ungekuwa flexible ungeona kitu gani tunaongelea.

Unajua kwamba mtu anayekuchukia hata ufanye mazuri kiasi gani atakuongea vibaya tu. Haya mambo yapo hata sehemu tunazoishi. So hiyo ni mitazamo tu, ya mtu binafsi haiwezi kuondoa ukweli wa mambo makubwa yanayofanywa na JPM.
 
1.Nyerere hakuwahi kukopy plagiarism) PhD ya MTU mwingine
2. Nyrere alikuwa mjamaa haswa hakuwahi kuuza nyumba za umma na kuhonga vimada
3. Nyerere hakuwahi amuru wasiojulikana wawaue wakosoaji wake
4. Nyerere alikuwa mwanadiplomasia hakuogopa kwenda nje kukutatana na wenzake
5.nyerere hakuwahi kuhusishwa na kashfa ya uzinzi na watendaji wake
6.nyerere hakuwa mshamba wa trafick light na ndege hakuwahi jenga butiama traffic light na uwanja wa ndege
 
Maswali mengi mno wakati sentensi yangu ni moja tu. Unaweza ukathibitisha kuwa Wikipedia ni credible source!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…