Mwalimu Sekondari ya Mwilibona awapiga wanafunzi 2 na kuwavimbisha mikono sababu ya kuchelewa kufika shuleni

Mwalimu Sekondari ya Mwilibona awapiga wanafunzi 2 na kuwavimbisha mikono sababu ya kuchelewa kufika shuleni

Huo ndio ukweli, akili ikiwa katika utimamu wake hauwezi kumuadhibu mtoto kwa kiasi hiki, huu ni UKATILI KWA WATOTO haifai.
Yaani walimu wengi wana shida ya afya ya akili sio bure.

Hivi unapambana tena na mtoto wa kike kumuadhibu namna hii ili iwe nini yaani.

Tutahakikisha hii inasambaa kwenye mitandao ya kijamii ili mwalimu husika achukuliwe hatua za kisheria.

Tukiendekeza haya ipo siku watoto watauliwa kiholela mashuleni halafu tutakuwa hatujawalinda watoto wetu dhidi ya ukatili wa hawa walimu wasio na elimu.
 
Yaani walimu wengi wana shida ya afya ya akili sio bure.

Hivi unapambana tena na mtoto wa kike kumuadhibu namna hii ili iwe nini yaani.

Tutahakikisha hii inasambaa kwenye mitandao ya kijamii ili mwalimu husika achukuliwe hatua za kisheria.

Tukiendekeza haya ipo siku watoto watauliwa kiholela mashuleni halafu tutakuwa hatujawalinda watoto wetu dhidi ya ukatili wa hawa walimu wasio na elimu.
Shida ni stress na stress zenyewe ni madeni tu, huku bank, huku maboto, huku mkopo kausha damu, mkopo chupi mkononi, vicoba,......huu muunganiko ukimdaka mtoto wa mtu lazma umjeruhi 😁
 
Dah natamani kuzaliwa miaka hii nisome shule za serikali niwe sipigwi Wala siguswi yaani ni full kutetewa .

Hapo namkumbuka mwalimu Janeth (mke wa mwendazake ) niliwahi kubeba peni yake ofisini kumbe Kuna ticha aliniona yule mama alinifinya haswa mpaka leo nilikuwa najiapia kama angeng'aa kwenye sura yangu siku yoyote hakika ningemkumbusha kuwa mama Mimi ndiye yule kijana niliyekwiba peni yako alafu ukanifinya vibaya mno .


Jamani mtoto sio fimbo ila walau kipigo Cha kawaida ni muhimu kwa maendeleo ya akili ya mtoto .
 
Waalimu wawe makini nyakati zimebadilika. Waliosoma Manyara Ranch zamani wanajua shughuli ilivyokuwa. Wangesema video zichukuliwe enzi hizo taifa lingeweka siku moja ya maombolezo. Mimi kwa upande wangu naona hao watoto ni washenzi na adhabu waliyopewa sio kubwa sana ila ndo hivyo bahati mbaya. Mungu amsimamie mwalimu hili jambo lipite salama vinginevyo naona hatari ya yeye kwenda jela.
 
Jinai ni nini?
Dini imeandikwa na watu kama mimi, the same applies to jinai imeandaliwa na watu kama mie.
Swala la walimu kuwa Failures ni mtazamo wako!
Jinai ni kutenda kosa lililokatazwa na sheria husika.

Mfano kwenye hili mwalimu ametenda kosa la jinai kwa kujeruhi kinyume na sheria ya adhabu (Penal Code).

Kwa ushahidi huu wa wazi watoto wametapakaa damu huyo mwalimu hachomoki mahakamani lazima ale mvua zake kadhaa nabakitoka ajira hana maana ukipatikana na jinai huwezi kuajiriwa katika utumishi wa umma.
 
Watoto wenyewe ni legelege fimbo tano tu unakufa.

Ila na hao waleta clip tena waalim wenzie ni kama wana ugomvi
dada yangu dunia ya sasa watu ni kama half dead
mambo ya kujitia umwamba mbele ya waalimu wa kike uonekane unajua kuadhibu ni ushamba. akienda jela hao watamtembelea zile wiki 2 za mwanzo baada ya hapo ni yeye na manyampala wa gerezani.

mimi ningekua mwalimu hata ukaribu na wanafunzi nisingeutaka kupewa kesi ya ubakaji na ulawiti ni kugusa.
 
Kipindi nasoma ilikua ukishindwa kupata division 1 unapigwa kama hivyo mikono mpaka inavuja damu, unaweweseka usiku haulali homa jasho unatetemeka tafran. Akil yenyewe ni slow learner , walimu viboko vinaua saikolojia ya mtoto.
 
Kwa mujibu wa maelezo mwalimu alitaka wanafunzi waje kusaini ofisini kwake kila siku saa moja na nusu, hii inaonesha kuwa hawa wanafunzi ni sugu kwenye utoro na uchelewaji,,,

hii ni kawaida kabisa kwa shule zenye kujielewa na zenye kufuatilia watoto kwa ukaribu.

Lengo la kufanya hili zoezi la baadhi ya wanafunzi kuja kusaini kwa mwalim ni kumfanya mtoto wako awe anatabia ya kuwahi shule na asiwe mtoro bila sababu, kwasababu kadiri wanavyo chelewa wanakosa masomo hasa vipindi vya asubuhi, na huenda ni vipindi vya asubuhi huwa ni basic mathematics au physics, wanavyo chelewa wanashusha ufaulu wa shule,

HUENDA shule hii ni private na tabia hizi za wanafunzi kama hawa wanashusha taaluma ya shule na wanavuruga image ya shule husika.

INAWEZEKANA

mwalim amefanya uchunguzi na kujiridhirisha kuwa sababu za utoro na uchelewaji ni UZEMBE WA MWANAFUNZI TENA KWA MAKUSUDI, na ukisema uwaache tu tabia hii itaota mizizi. ukiwafukuza utalaumiwa na hao hao wazazi tena utatangazwa kila kona ya dunia kuwa mwanangu kafukuzwa shule kwa kosa la kuchelewa, ukimwacha kila siku anakuja shule muda wa vipindi na jamii hii hii itasema shule haina uangalizi, wanachapwa fimbo mbili tatu ila kila siku wanarudia makosa hayo hayo tena kwa makusudi, ukifuatilia zaidi sababu za kuchelewa shule unaweza kuta ni kufuatlia movie na tamthilia hadi usiku wa manane,

MWANAFUNZI AKICHELEWA AKICHAPWA WALIMU WANALAUMIWA

WAKIACHWA ,WALIMU WATALAUMIWA SHULE HAIFATILII WANAFUNZI, SHULE HAIJIELEWI, WATOTO WANADHURURA MUDA WA MASOMO,,,,

MWALIMU AFANYAJE??????


lawama zote kwa walimu, walimu, walimu, walimu walimu

Shule za serikali wameluona hili wameamua kuwaacha watoto wenu wafanye watakavyo, walimu wanachukua mshahara saa 9 wanasepa kufuga kuku na wengine wanaenda shamba, nafikiri ya watoto wenu walio shule za serikali hali mnaiona sasa na tabia za watoto wenu,,huo ni mfano tu, subirini jamii ya kesho mtaiona tu,,,, mmewadharau walimu subiri watoto wenu wa kesho mtaona ushoga na usagaji na mauaji yatakavyo ongezeka kupitia utandawazi huu na hizi filamu, ukweli nikuwa watoto wenu muda mwingi hawapo na wazazi bali wapo na walimu ambao wamekatishwa tamaa na jamii

Shule za private sasa wameanza kubadili mfumo, sasa shule zimeanza kuajiri hadi watu wakufanya usafi shuleni,,, tunatengeneza kizazi cha broilers cha hapo mbeleni,,,

WALIMU WANALIPWA MSHAHARA LAKI 3 HADI 5 ,,, hii ndo hali ya walimu nchi hii.

Wanaweza wakakosea kwa msongo wa mawazo ila ndo wanaolea watoto wenu, warekebishwe na sio kupost mitandaoni, mnaharibu taswira ya ualimu,shule na kuwapa Vichwa wanafunzi,
 
Back
Top Bottom