Mwalimu Sekondari ya Mwilibona awapiga wanafunzi 2 na kuwavimbisha mikono sababu ya kuchelewa kufika shuleni

Mwalimu Sekondari ya Mwilibona awapiga wanafunzi 2 na kuwavimbisha mikono sababu ya kuchelewa kufika shuleni

Sidhani wanafunzi wa sasa hivi kama wanapigwa kuliko sisi wa enzi Mwalimu tulivyopigwa!
Hata hivyo waalimu wengi kutokana na changamoto za maisha wana stress nyingi.
Wanahitaji cancelling.
 
Jinai ni kutenda kosa lililokatazwa na sheria husika.

Mfano kwenye hili mwalimu ametenda kosa la jinai kwa kujeruhi kinyume na sheria ya adhabu (Penal Code).

Kwa ushahidi huu wa wazi watoto wametapakaa damu huyo mwalimu hachomoki mahakamani lazima ale mvua zake kadhaa nabakitoka ajira hana maana ukipatikana na jinai huwezi kuajiriwa katika utumishi wa umma.
Hakuna kitu kama hicho. Watoto wanaweza wakajikata kwa nyembe na damu ikatoka.
Vitoto hivyo ni vihuni tu
 
Mwalimu Kisogi wa shule ya Sekondari Mwilibona awapiga wanafunzi wake 2 na kuvimba mikono na damu kumwagika kisa wamechelewa kufika shule.

Wanafunzi wao wamesema walikuwa wanakwenda kusaini ofisini kwake kwa sababu walikuwa wanakosa shule. Kwahiyo walitakiwa kila siku wasaini saa moja na nusu sasa leo wakiwa wamechelewa baada ya hapo mwalimu huyo akawashushia kipigo kizito wanafunzi hao.

Soma Pia: Mwalimu adaiwa kumpiga ngumi mwanafunzi na kumng'oa jino, eti Kisha kapata alama 29 za Hisabati
Halafuu kuna wathenge humu kutwa wanawatetea hawa mbwa, mi angekuwa mwanangu huyo mwalimu ningemtoboa macho yote mawili
 
Kwa mujibu wa maelezo mwalimu alitaka wanafunzi waje kusaini ofisini kwake kila siku saa moja na nusu, hii inaonesha kuwa hawa wanafunzi ni sugu kwenye utoro na uchelewaji,,,

hii ni kawaida kabisa kwa shule zenye kujielewa na zenye kufuatilia watoto kwa ukaribu.

Lengo la kufanya hili zoezi la baadhi ya wanafunzi kuja kusaini kwa mwalim ni kumfanya mtoto wako awe anatabia ya kuwahi shule na asiwe mtoro bila sababu, kwasababu kadiri wanavyo chelewa wanakosa masomo hasa vipindi vya asubuhi, na huenda ni vipindi vya asubuhi huwa ni basic mathematics au physics, wanavyo chelewa wanashusha ufaulu wa shule,

HUENDA shule hii ni private na tabia hizi za wanafunzi kama hawa wanashusha taaluma ya shule na wanavuruga image ya shule husika.

INAWEZEKANA

mwalim amefanya uchunguzi na kujiridhirisha kuwa sababu za utoro na uchelewaji ni UZEMBE WA MWANAFUNZI TENA KWA MAKUSUDI, na ukisema uwaache tu tabia hii itaota mizizi. ukiwafukuza utalaumiwa na hao hao wazazi tena utatangazwa kila kona ya dunia kuwa mwanangu kafukuzwa shule kwa kosa la kuchelewa, ukimwacha kila siku anakuja shule muda wa vipindi na jamii hii hii itasema shule haina uangalizi, wanachapwa fimbo mbili tatu ila kila siku wanarudia makosa hayo hayo tena kwa makusudi, ukifuatilia zaidi sababu za kuchelewa shule unaweza kuta ni kufuatlia movie na tamthilia hadi usiku wa manane,

MWANAFUNZI AKICHELEWA AKICHAPWA WALIMU WANALAUMIWA

WAKIACHWA ,WALIMU WATALAUMIWA SHULE HAIFATILII WANAFUNZI, SHULE HAIJIELEWI, WATOTO WANADHURURA MUDA WA MASOMO,,,,

MWALIMU AFANYAJE??????


lawama zote kwa walimu, walimu, walimu, walimu walimu

Shule za serikali wameluona hili wameamua kuwaacha watoto wenu wafanye watakavyo, walimu wanachukua mshahara saa 9 wanasepa kufuga kuku na wengine wanaenda shamba, nafikiri ya watoto wenu walio shule za serikali hali mnaiona sasa na tabia za watoto wenu,,huo ni mfano tu, subirini jamii ya kesho mtaiona tu,,,, mmewadharau walimu subiri watoto wenu wa kesho mtaona ushoga na usagaji na mauaji yatakavyo ongezeka kupitia utandawazi huu na hizi filamu, ukweli nikuwa watoto wenu muda mwingi hawapo na wazazi bali wapo na walimu ambao wamekatishwa tamaa na jamii

Shule za private sasa wameanza kubadili mfumo, sasa shule zimeanza kuajiri hadi watu wakufanya usafi shuleni,,, tunatengeneza kizazi cha broilers cha hapo mbeleni,,,

WALIMU WANALIPWA MSHAHARA LAKI 3 HADI 5 ,,, hii ndo hali ya walimu nchi hii.

Wanaweza wakakosea kwa msongo wa mawazo ila ndo wanaolea watoto wenu, warekebishwe na sio kupost mitandaoni, mnaharibu taswira ya ualimu,shule na kuwapa Vichwa wanafunzi,
Sawa jiandae ukawe mtetezi wake court huyo mwalimu muuaji
 
Umepotoka mkuu,Yuko shule Gani huyo mtoto wako,yaani mtoto katukana au kachelewa nikutafute wewe mzazi,umeniweka vocha!? Ni mboko tu ila sio za huyu mwalimu aliwajeruhi watoto.
We piga mboko zako ila nikimkuta mtoto na dosari isiyoelezeka jua kesi itahama kutoka kwa mwanafunzi na kuelekea kituo chochote cha polisi mhanga ukiwa wewe mwalimu maana lazma nikuharibu vibaya mno. Yani lazma nikuvunje vunje ili kichaa chako kikae vizuri
 
Mwalimu Kisogi wa shule ya Sekondari Mwilibona awapiga wanafunzi wake 2 na kuvimba mikono na damu kumwagika kisa wamechelewa kufika shule.

Wanafunzi wao wamesema walikuwa wanakwenda kusaini ofisini kwake kwa sababu walikuwa wanakosa shule. Kwahiyo walitakiwa kila siku wasaini saa moja na nusu sasa leo wakiwa wamechelewa baada ya hapo mwalimu huyo akawashushia kipigo kizito wanafunzi hao.

Soma Pia: Mwalimu adaiwa kumpiga ngumi mwanafunzi na kumng'oa jino, eti Kisha kapata alama 29 za Hisabati
Aione LIKUD mzee wa Kayumba..
Anyways, tukio la lini hili!?
 
Kuna haja gani kumpiga mtoto wa mtu kwakuwa tu amechelewa kufika shule au jana yake hakuja shule? Wewe mwalimu kazi yako ni kufundisha tu hayo mambo mengine hayakuhusu sanasana unaweza kumuita mzazi wake na kumueleza tatizo la mwanawe ili kama kumpiga ampige yeye mwenyewe.
Ningekuwa mwalimu haya matatizo ya kujitakia ningeyaepuka kabisa ningeacha kujitia kiherehere kwa kujifanya nampenda sana mwanafunzi wakati yeye mwenyewe hana mpango na elimu.
Madeni mkuu...😂😂
 
Kwani mwalimu ukifundisha na kuachana na kuadhibu watoto mshahara unapungua ama ni vipi?

Kuna mwalimu ni mshikaji wangu tangu aajiriwe hajui kumuadhibu mwanafunzi yeye anajali job descriptions yake na ni rafiki wa wanafunzi wengi anawazoa kwenye tuition haina kifani.

Siku zote ukiona mwalimu anapenda kutoa adhabu ujie kichwani ni empty hivyo anajificha kwenye ukali aogopwe ili kuficha ukilaz,a wake.
Mkoa gani huko ambao wanafunzi bado wanaenda tuition miaka hii!??
 
We piga mboko zako ila nikimkuta mtoto na dosari isiyoelezeka jua kesi itahama kutoka kwa mwanafunzi na kuelekea kituo chochote cha polisi mhanga ukiwa wewe mwalimu maana lazma nikuharibu vibaya mno. Yani lazma nikuvunje vunje ili kichaa chako kikae vizuri
Nipe location ya shule mwanao alipo,atakusimulia,hutaki mboko mpeleke feza,walimu wa hizi shule za kata tunatabu sana
 
Back
Top Bottom