Mwalimu wa Kanisa ahukumiwa miaka 30 kwa kosa la kulawiti

... kwani kuna aliyekuzuia kutiririka? Tiririka umwage "sumu" iliyokujaa kifuani

Itakuwa wamewaachia na nyie mtiririke kama wao wanavyotiririka kwa ustaadh mkuu

Huyo mwl kafanya upumbavu na imempasa hiyo adhabu
lakini dini yake haiusishwi kwenye komenti lakini ingekuwa muislam ndio kafanya hivyo zingeaNZA KASHFA KWA UISLAM
 
Dah habari kama hizi sio za kutangaza.

Serikali ipige marufuku kutangaza mambo ya kikatili kama haya lakini hukumu ziendelee.

Kuyapaza sauti haya mambo inakera,omba yasimkute ndugu yako haya mambo utaona inavyouma kutangaza.

Nimesema kutangaza sio kuhukumu,hukumu ziendelee ila isiwe matangazo.

Kutangaza pía kunasaidia kuwaonesha Jamii namna adhabu ilivyo kali, hvyo hata kama kuna wengne wenye nia ya kutenda huo uovu basi wataacha mara moja kwa kuhofia kupotelea jela kwa miaka 30
 
Utamfanyiaje mtoto hivyo
Huyo lazima kichwani ana
Fuse imekatika

Ova
 
Hii dunia sasa tukimbilie wapi na watoto wetu, tunawapeleka kanisani tukihisi ni sehemu salama kiasi na kuna hofu ya Mungu, kumbe siyo kweli mtoto wa miaka 4 jamani😒
Usipeleke mtoto tu bils kujua utaratibu wa kufundisha watoto, na tabia za waalim. Hakikisha unampeleka mwenyewe na ibada ikiisha kamchukue.

Mungu atakudai pale mtoto atakapoumizwa kwa uzembe wako. Mungu atusaidie na tusiache kuwaombea wanetu!
 
Kutangaza pía kunasaidia kuwaonesha Jamii namna adhabu ilivyo kali, hvyo hata kama kuna wengne wenye nia ya kutenda huo uovu basi wataacha mara moja kwa kuhofia kupotelea jela kwa miaka 30
Inassidiaje wakati matendo bado yanaendelea ?

Huyu aliyefsnys hivi unadhani hakujua hukumu ya alitendalo na adhsbu yake ilivyo kali ?
 
Usipeleke mtoto tu bils kujua utaratibu wa kufundisha watoto, na tabia za waalim. Hakikisha unampeleka mwenyewe na ibada ikiisha kamchukue.

Mungu atakudai pale mtoto atakapoumizwa kwa uzembe wako. Mungu atusaidie na tusiache kuwaombea wanetu!
Aisee haya ila ni Kuwaombea tu, utawachunga mara ngapi mkuu huko shule pia nk.
 
Dunia hii inazidi kuoza. Sio shule tu, hata TV zinabaka, kulawiti na kuharibu akili za watoto. Ni vyema mzazi kufanya sehemu yako kwa uaminifu. Mengine ni Mungu ndiye atafanya. Waombee lakini pia pambana kuwalinda kadri utakavyoweza.

Ushauri wa bure kwa wale wanaopenda kupeleka watoto shule kwa kuangalia ufaulu. Kabla hujampeleka shule mtoto, hakikisha shule inasimamia maadili mazuri na usalama wa watoto kwa maana ya mazingira na walezi wako vizuri ndio uangalie issue ya ufaulu.

Pili fundisha mwanao mbinu za kujilinda. Mfano mwambie maeneo ambayo mtu yeyote awe mwalimu, mwanafunzi et al akimshika awe mkali, apige kelele au kuripoti. Hii itamsaidia kwa kumtia hofu mtu aliyepanga uovu. Angalau inaongeza line of defense.

Bwana aturehemu!
 
Mahakama ya Mkoa wa Kinondoni imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Elisha Mushi, mkazi wa Ubungo Kibangu baada ya kuthibitika kumlawiti mtoto wa miaka minne kanisani.

Mushi, ambaye alikuwa akifanya kazi ya kufundisha watoto kanisani anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 19, mwaka huu katika Kanisa la Embassy Kingdom.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Ester Mwakalinga baada ya kuwasikiliza mashahidi saba wa upande wa mashitaka, akiwamo mtoto mwenyewe, mama mzazi pamoja na mchungaji wa Kanisa la Embassy Kingdom aliyekiri kumfahamu mama mzazi wa mtoto aliyetendwa.

Mashahidi wengine ni daktari wa Hospitali ya Sinza Palestina aliyempima mtoto huyo pamoja na askari wa Kituo cha Polisi Osterbay. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Ester alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa, mahakama imejiridhisha pasipo shaka yoyote kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa analotuhumiwa nalo.

“Kutokana na vielelezo vilivyowasilishwa, ikiwemo ripoti ya daktari (PF3) na ushahidi wa mama na mtoto mwenyewe, mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo, hivyo inakutia hatiani kwa kosa la kulawiti,” alisoma Hakimu Ester.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Hilda Kato aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia ya kufanya vitendo vya udhalilishaji na kikatili kama hivyo katika jamii.

Source: Gazeti la Mwananchi

Kumbe hata huko yapo[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Unaona Eeeee pangekua hapatoshi ukumbin

Wangesema ndio michezo yao wanafundishana huko mara kwanini mnawaacha watoto wenu na mwalimu qa madrasa mara ungesikia ndio dini yao ilivyo
 
Mshitakiwa hakujitete,kweli hiki kizazi cha laana nakumbuka mwanzirishi wa hii tabia jamaa mmoja akiitwa Maumba sijui yuko wapi
Tabia hii ilikuwepo hata kabla ya Maumba kuzaliwa. Vile tu yeye alikuwa wa kwanza kutangazwa hadharani
 
Mahakama ya Mkoa wa Kinondoni imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Elisha Mushi, mkazi wa Ubungo Kibangu baada ya kuthibitika kumlawiti mtoto wa miaka minne kanisani.

Mushi, ambaye alikuwa akifanya kazi ya kufundisha watoto kanisani anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 19, mwaka huu katika Kanisa la Embassy Kingdom.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Ester Mwakalinga baada ya kuwasikiliza mashahidi saba wa upande wa mashitaka, akiwamo mtoto mwenyewe, mama mzazi pamoja na mchungaji wa Kanisa la Embassy Kingdom aliyekiri kumfahamu mama mzazi wa mtoto aliyetendwa.

Mashahidi wengine ni daktari wa Hospitali ya Sinza Palestina aliyempima mtoto huyo pamoja na askari wa Kituo cha Polisi Osterbay. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Ester alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa, mahakama imejiridhisha pasipo shaka yoyote kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa analotuhumiwa nalo.

“Kutokana na vielelezo vilivyowasilishwa, ikiwemo ripoti ya daktari (PF3) na ushahidi wa mama na mtoto mwenyewe, mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo, hivyo inakutia hatiani kwa kosa la kulawiti,” alisoma Hakimu Ester.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Hilda Kato aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia ya kufanya vitendo vya udhalilishaji na kikatili kama hivyo katika jamii.

Source: Gazeti la Mwananchi
Hakuna kitu kinachoitwa mwalimu wa kanisa, nadhani mwandishi amejaribu kubalance na walimu wa madrasa. Lakini pia kanisa linaitwa Embassy Kindom, hili kanisa au kijiwe cha wahuni wanaotumia mwamvuli wa uhuru wa kuabudu
 
Madangulo kibao unapata mbunye za buku 2000 yanini kubaka acha akome
 
Inassidiaje wakati matendo bado yanaendelea ?

Huyu aliyefsnys hivi unadhani hakujua hukumu ya alitendalo na adhsbu yake ilivyo kali ?
Wanajua adhabu ilivyo, lakini kitendo cha kutangaza hadharani namna hukumu ilivyo inasaidia kupunguza japo itachukua miaka kadhaa vitendo hivi kuja kukoma kabisa
 
Elezea inapunguza vipi wakati hawa wanaofanya weshasikia yaliyowakuta wenzao

Usiseme yanapunguza tu,sema yanapunguza kivipi ?
 
Mama mwema na mpole, Samia Suluhu Hassan, ampe msamaha kama alivyofanya kwa wengine siku za kwanza za Urais wake.
 
Back
Top Bottom