SueIsmael
JF-Expert Member
- Dec 11, 2013
- 932
- 1,282
Kuna namna ya kuwasilisha ujumbe kistaarabu hasa unapokuwa kiongozi; tena kiongozi msomi. Ukiwa kiongozi unawajibu wa kuwa na ustaarabu na umakini kutoleta/kuchochea mkanganyiko na uhasama. Kama ni vigumu kutofautisha uwasilishaji kama "John Magufuli" na "Rais John Magufuli" ni vyema akitayarishiwa kwa maandishi ujumbe wake. Akumbuke kila anachokisema na kukifanya kinaingia kwenye kumbukumbu, tena kama akisi ya Tanzania na Afrika kwa miaka ijayo.Alichokisema rais ni msimamo wa serikali. Chanjo hizo hazieleweki, wanaotuletea hizo chanjo kwa siku wana 4000, kwanini hawakufanya kwao kwanza wapone? Na kingine na sio nchi moja inatengeneza chanjo pia. Tusipokua makini tutalishwa sumu.
Ila mnaotamani kutafuta chanjo mkachanjwe at your own risk
Ni muhimu kuwa makini na maswala ya kiafya - hasa janga hili ambalo ni geni kwa ulimwengu mzima - na kwa hilo nitamshukuru. Ila ninamlaumu kwa namna anavyowasilisha ujumbe wake, na mkanganyiko anaozidi kuleta.