Mwambieni Rais Magufuli apunguze sauti. Nchi hii bila wazungu ni tajiri kwa kipi?

Kuna namna ya kuwasilisha ujumbe kistaarabu hasa unapokuwa kiongozi; tena kiongozi msomi. Ukiwa kiongozi unawajibu wa kuwa na ustaarabu na umakini kutoleta/kuchochea mkanganyiko na uhasama. Kama ni vigumu kutofautisha uwasilishaji kama "John Magufuli" na "Rais John Magufuli" ni vyema akitayarishiwa kwa maandishi ujumbe wake. Akumbuke kila anachokisema na kukifanya kinaingia kwenye kumbukumbu, tena kama akisi ya Tanzania na Afrika kwa miaka ijayo.

Ni muhimu kuwa makini na maswala ya kiafya - hasa janga hili ambalo ni geni kwa ulimwengu mzima - na kwa hilo nitamshukuru. Ila ninamlaumu kwa namna anavyowasilisha ujumbe wake, na mkanganyiko anaozidi kuleta.
 
Umeongea ukweli mkuu,Rais ni nembo ya nchi hizi kauli zake zinaifanya nchi yetu ionekane ni ya vichekesho,Covid 19 ni pandemic ya dunia na sisi sio kisiwa katika glope hii.
Umeandika upumbavu wa kiwango cha hali ya juu kabisa.
 
Kila mtu ana style na tabia yake kwenye kushughulikia mambo ndio maana hata wanasaikolojia waligawa makundi ya watu kadri ya tabia zao. Rais Magufuli yuko hivyo hana konakona kama unavyotaka wewe ila ana ustaarabu na imani kwenye kile anachokijua

Sijui Yule aliyetuita SHITHOLE countries yuko kundi gani😥😥😥
 
Sitaki kumfananisha Trump na Magufuli hata siku moja! Ningependa kumfananisha Rais wetu na viongozi wa maana zaidi.

Ni kweli kila mtu ana hulka yake. Ila yeye mpaka mwaka 2025 siyo kila mtu, na anapozungumza hadharani hazungumzi kama mtu yoyote. Yeye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni Amiri Jeshi Mkuu ni taswira ya nchi yetu. Neno lake lina nguvu ambayo siyo kila mtu anayo. Hivi vyeo vinampa jukumu la kuzungumza na hadhara kwa kuzingatia weledi.
 
Neno lake lina nguvu ndio maana jana amekataa chanjo zisizoeleweka
 

Wenzako wako maabara wanatafuta mbadala wa cobalt km ilivyokuwa magari ya mafuta now ni magari ya umeme
 
Watu wenye akili Kama zako wanatakiwa kupigwa Vita kwa nguvu zote. Haki za watu weusi Marekani zingepatikanaje Kama kusingekuwa na watu jasiri Kama Marthin Luther waliokuwa tayari kufa kwa ajili ya kupigania haki za watu weusi dhidi ya wazungu?

Tunahitaji viongozi wengi wenye ujasiri Kama Magufuli, wanaoweza kusimamia masilahi ya nchi zao dhidi ya mabeberu bila uwoga wowote. Wanaoweza kujisimamia katika maamuzi yao bila kuingiliwa na mabeberu.
Kwa dunia ya sasa ushirikiano hauepukiki lakini uwe ni ushirikiano wenye manufaa pande zote mbili, siyo ushirikiano wa kinyonyaji.

Ni dhambi kubwa kutambua kuwa unaonewa na wewe ukakubali kuendelea kuonewa kwa sababu tu anayekuonea ni mkubwa. Mungu ametupa uwezo wa kutambua zuri na baya, haki na uonevu.
 
Haki za watu weusi Marekani zingepatikanaje
Ktk zama hizi, haki za binadamu na watu siyo ishu tena. Kwani wazungu wanakandamiza haki za binadamu?


Tunahitaji viongozi wengi wenye ujasiri Kama Magufuli,
Tunataka watu jasiri lkn wenye akili na maarifa, wanaojua wanasema nn, wanataka nn na wanapinga nn. Siyo wakurupukaji kamq huyu Magufuli.

Anazodoa wazungu kuhusu chanjo wakati nchi yake haina ubavu hata wa kutengeneza Panadol. Huu siyo ujasiri ni ujinga.

Ktk nchi hii kuna chanjo nyingi sana zinatolewa kwa mama na mtoto. Mama akiwa mjamzito anapewa chanjo. Mtoto akizaliwa anapewa chanjo kama zote. Mbona hajawahi kuhoji usalama wa hizi chanjo? Zinatengenezwa Chato hizi?

Kama wazungu wangekuwa na nia mbaya na sisi wangeshindwa kufanya yao kupitia chanjo hizi?
 
Zama hizi haki za binadamu siyo ishu? Umesahau US wanaziandama nchi za Afrika wakizituhumu kukiuka haki za binadamu wakati wao ndo wanaongoza kwa ukiukwaji wa haki za binadamu katika majeshi yao huko Syria, Libya. Unakumbuka gereza la Quantanamo namna lilivyokuwa likitesa wafungwa? Vipi mauaji ya wamarekani weusi yalivyozua maandamo nchi nzima?
 
NANI WA KUMWAMBIA SASA??
 
Kwani haya ndiyo anayoyapigania Magufuli?

Yeye anasema wazungu wana nia mbaya na waafrika, wanaleta chanjo zenye madhara. Ndiyo maana tunahoji ana ubavu wa kujitegemea ktk hili??
 
Hii nchi inaongozwa na extremists. Nyerere alikuwa extremist akabana kila kitu eti Ujamaa. Akaja Mwinyi akafungua kila kitu eti utandawazi. Akaja Mkapa akanafsisha kila kilichotaifishwa kwa kuamini hiyo ndiyo dawa! Akaja Kikwete akawa Mzungu boy! Wazungu wakaja wakaogelea wakacheza, wakachukua...
Na sasa tunaanza upya kwa mara ya pili.
Nchi hii haijapata kiongozi alie balanced hata kidogo. Wote vichwa maji!
Ah, tungepata viongozi kama wa Botswana!
 
Mropokaji mkuu wa taifa. Hajui chochote kuhusu globalization yule alisoma wapi mbona mbumbumbu vile???
 
Ujasiri wa kijinga
 

Sidhani kama unaelewa maana halisi ya kutegemeana hata wazungu wanaendelea kiteknolojia kwa malighafi zinazotoka Tanzania pia so wasiponunua na wao maendeleo yao..... Jaza mwenyewe!
 
Wewe hujawahi kusoma sifa za wasukuma "hata akielemewa na mzigo atasema twente tu" sishangai mimi
 
Hata nguo na viatu anavyo vaa havitengenezwi Tanzania
Umeongea ukweli mkuu,Rais ni nembo ya nchi hizi kauli zake zinaifanya nchi yetu ionekane ni ya vichekesho,Covid 19 ni pandemic ya dunia na sisi sio kisiwa katika glope hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…