Mwami Theresa Ntare VI wa Heru - Chifu wa kwanza mwanamke

Chachu,
Hayo makala sikuandika mimi mwandishi hataki jina lake litokee lakini siku hiyo ya mazungumzo tulikuwa pamoja ilikuwa tarehe 6 November 1992.
Kwanini hataki kufahamika kwa mchango wake?
 
Umenena haswaa?
 
Ulakoze cyane. Je, Kuna sehemu naweza kupata kitabu chake kinachoelezea zaidi?
 
Safi sana mkuu.

Siyo kama siku hizi tuchifu uchwara mbuzi twiiingiii kila jimbo halafu tunakuwa bought like sweets or candy.
 
Hivi inakuaje wadau wanacopy li story loote li refu halafu anajibu ka neno ka moja tu " shukran"???? Very annoying.
F £€#@*** off.
 

I have the same sentiments here. If I am not mistaken, Nyerere returned back from his studies in 1952 and he was just 30 years old. If you accept the current narrative, then you would have to agree that we as a country didn't have any appetite for our own independent until the arrival of 30 or 32 years old politician.
 
 
Hivi inakuaje wadau wanacopy li story loote li refu halafu anajibu ka neno ka moja tu " shukran"???? Very annoying.
F £€#@*** off.
Thamani ya hako kaneno kamoja unaielewa??
Mtu kashasema kwa kina.
Ulitaka ajibiweje?
 
Mzuvendi,
Nakuwekea hapo chini post ambayo niliiweka hapa siku ziizopita.
Nadhani kuna ndani yake kitu cha kujifunza:

Umuhimu wa Abdul Sykes ulianza Burma akiwa katika 6th Battalion ya KAR
wakati wa Vita Kuu ya Pili (1938 - 1945).

Hapo ndipo alipowaeleza askari wenzake umuhimu wa kuunda chama cha siasa
kuwaondoa Waingereza Tanganyika.

Wakati huo Abdul alikuwa na umri wa kiasi cha miaka 23 hivi.
Angalia hiyo picha yake hapo chini akiwa Burma:



Ukipitia Tanganyika Intelligence Gazette kuanzia 1950 hizi ni taarifa
za kikachero za Waingereza zikiandikwa na Special Branch utaona
habari za Abdul akiwa Dar es Salaam na mikoani alikokuwa akipita
kuongea na viongozi wa TAA kuhusu hali ya baadae ya Tanganyika.

Moja ya taarifa hizi ambazo mimi ninayo ni ni safari ya Abdul Sykes
ya Kanda ya Ziwa aliyofanya mwaka wa 1952 akiwa Katibu na Kaimu

Rais wa TAA kukutana na Paul Bomani na kisha kuelekea Uganda.
Lakini kabla ya hapa mwaka wa 1950 Abdul Sykes alifanya mkutano
na Jomo Kenyatta na kundi lake la kina Paul Ngei, Kungu Karumba,
Bildad Kaggia
na wengine Nairobi agenda kuu ikiwa kuunganisha nguvu
za Waafrika wa Tanganyika na Kenya kupambana na Waingereza.

Huu ulikuwa wakati wa Mau Mau.
Nimeeleza habari hizi kwa kirefu kwenye kitabu chake.

Mimi sikulaumu kuwa wewe hujui historia hii.

Utaijuaje ikiwa haikupatapo kuandikwa hadi nilipoiandika na kitabu kuchapwa
Uingereza mwaka wa 1998?

Tatizo lako ndugu yangu Nguruvi3 ni kuwa unataka kuleta ubishi katika jambo
ambalo wewe huna ujuzi nalo.

Katiba iliyoandikwa na wazee wangu mwaka wa 1950 ipo.

Abdul Sykes
kaieleza katika taarifa yake kwa wanachama wa TAA (Angalia:
Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January,
1951 Sykes' Papers).

Cranford Pratt katika kitabu chake ''Critical Phase in Tanzania,'' kaieleza na
kaisifia (Angalia: Cranford Pratt, The Critical Phase in Tanzania 1945-1968,
Cambridge University Press, London, 1976, uk. 29-31.)

''Document'' hii hutoweza kuiona popote pale kwa sababu hata Tanzania National
Archives (TNA) imenyofolewa jalada liko tupu.

Hata kwenye maktaba yake ya ''microfilm,'' pia imeondoshwa.
Halikadhalika katika Maktaba ya CCM Dodoma jalada pia liko tupu.

Nimepata kuandika kuhusu, ''Lost Documents,'' naitafuta hii paper nikiipata nitaileta
barzani In Shaa Allah.

Leo sishangai kwako wewe kunitaka mimi nikupe ushahidi wa katiba iliyoandikwa
na wazee wangu mwaka wa 1950.

Wakati tunahariri mswada wa kitabu kulikuwa na ubishani mkubwa kati yangu na
wachapaji kwa kuwa neno nililoandika ni kuwa nyaraka hii ya katiba ''imeibiwa.''

Mhariri hakupenda neno hili na akasema niseme, ''imepotea,'' au ''haionekani.''
Isiwe ''imeibiwa.''

Nguruvi3,
Nimekupa ushahidi wa katiba iliyoandikwa na wazee wangu waliokuwa katika
TAA Political Subcommittee.

Document hii ilijadiliwa katika mkutano mkuu wa TAA 1954 mkutano uliounda
TANU na mwaka wa 1955 Nyerere alisoma yaliyokuwa katika ''document,'' hii
UNO mbele ya Kamati ya Udhamini.

Ikiwa hujaridhika na haya niliyokueleza mimi nipo hapa In Shaa Allah nasubiri.
Bahati mbaya unachoshwa na kusoma vitabu.
 

WanaMajlis:
Hiyo hapo chini ni Tanganyika Political Intelligence Summary March 1952:

Mohamed Said: TANGANYIKA POLITICAL INTELLIGENCE SUMMARY, MARCH 1952
"Tanganyika Political Intelligence
Summary, March 1952":

"...it is reported that the Secretary of the Association, Abdul Wahid Sykes has
dispatched letters to all branches asking members for suggestions under
the following heads for a memorandum to be prepared for the Royal
Commission..."

“...Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association who, as
reported in last month's summary (paragraph 20) was going on safari up
country, visited Mwanza, where he met Paul Bomani, President of the
Bukoba African Association, and accompanied him to Bukoba. Sykes then
visited Kampala alone.....on 8th March, a secret meeting was held, attended

by leading members of the Mwanza Branch...”

(Hizi ni taarifa kutoka Rhodes House Library, Oxford kutoka majalada ya
kikachero ya Waingereza baada ya miaka 50 yanawekwa wazi kwa mtafiti
yeyote kuyasoma na kufanya nakala akipenda.)
 
We had alot of appetite the reason why parties were formed.
Nyerere was already groomed by the system thus he was all over the independence tire.
 
We had alot of appetite the reason why parties were formed.
Nyerere was already groomed by the system thus he was all over the independence tire.
Fofofoo,
Bora uandike Kiswahili ili wengi waweze kuchangia.

Kama Nyerere alikuwa katayarishwa na hicho unachokiita ''system,''
mbona hakuna ushahidi ila maneno tu kama haya yako?

Mimi nimekuwekea ushahidi kuwa wazee wangu waliamua kupambana
na ukoloni toka miaka ya 1920 na kuna ushahidi wa kutosha katika hili.

Mbona hakuna ushahidi wa hiyo, ''system,'' kuja na chama cha siasa
kwa ajili ya Nyerere, kinyume chake kuna ushahidi wa kuonyesha kuwa
mwelekeo ulikuwa kupiga vita juhudi za Waafrika kuwa na chama cha siasa?

Lakini kubwa kwa Nyerere kukubalika katika siasa alipofika Dar es Salaam
kulitegemea sana kuungwa mkono na viongozi ambao tayari walikuwa na
sauti ndani ya TAA.

Sijui kama unajua kuwa Nyerere aliingizwa ndani ya ''inner circle,'' ya TAA
na Hamza Mwapachu na Abdul Sykes na uamuzi ulifanyika 1952 nyumbani
kwa Mwapachu Nansio, Ukerewe.
 
Rekebisha hapo sio Said Sykes uliomsoma ni Ally Sykes hata mimi niliwasoma pia na akina Dossa Aziz na John Rupia. Tupo pamoja.
Ahsante mkuu. Lakini nadhani (kama kumbukumbu yangu ipo sahihi) palikuwa na Sykes wawili na wote walihusika katika harakati hii. Sijui kama walikuwa ndugu. Naweza kuwa wrong, lakini pia nimeona kuna mdau anasema palikuwa na mtu anaitwa Abdul Sykes. I blame mfumo wa elimu yetu.
 

Jamani hakuna haja ya Malumbano au kuonyeshana umwamba wa nani anajua historia ya nchi yetu. Tukubaliane kwamba palikuwa na watu waliomtangulia Nyerere katika harakati za kudai uhuru. Ni jambo lisilopingika. Hata ukikumbuka enzi Mkoloni wa kijerumani na hata kabla ya kipindi cha Sultani mababu zetu walionyesha nia yao ya kuwa huru, kuendeleza himaya zao bila kuingiliwa na wageni, hivyo wakaanza kupigana na hawa wavamizi wa himaya yao. Na hawa kina Mkwawa, Milambo,kina Mangi, Kinjekitile na nisiokumbuka wanahitaji kutajwa kama waanzilishi wa harakati hizi hata kama walikuwa hawajui kusoma wala kuandika kama kina Nyerere, Mwami Theresa Ntare ambao walitumia Elimu ya Mkoloni dhidi ya Mkoloni. Nadhani sote tunakumbuka kusoma historia ya vita ya Maji Maji ambayo ilitokea miaka michache kabla ya vita ya kwanza ya Dunia na miaka mingi kabla ya kuzaliwa kina Nyerere, Mwami Theresa Ntare nk. Hawa mababu zetu nadhani wangepewa sifa Fulani pia. Kitu ambacho nacholaumu ni mfumo wa elimu yetu ya kumpa all credits Nyerere na kusahau kwamba palikuwa na mamia na maelfu ya wengine walioshiriki. Inaweza kuwa sio kosa la Nyerere personally nadhani alitumia charismatic, convincing, negotiation personality yake kuwa kama kiongozi wa harakati. Nadhani ni sawa na yaliyotokea kwa Mandela, Martin Luther King nk. Sio kwamba wao harakati za kudai haki, uhuru zilianzishwa na wao bali walikuja kuwa Leading Figures katika harakati hizo. Tofauti wenzetu (South Africa, USA) wanawapa credits wote walioshiriki bega kwa bega na hawa leaders, sisi ni Nyerere, Nyerere, Nyerere tu. Sijui kama hao waliotajwa Sykes, Mwapachu,Rupia, Bomani wana hata uchochoro ulipewa majina yao, Majengo yenye majina yao? Yaani ni kama hawakuwahi kulitumikia hili Taifa letu kubwa. Inasikitisha..
 
Zito Kabwe siyo Mwami wa Heru kwani kwao Mwandiga hapastahili kuwa na Mwami? Tafadhali sana, usiwatukane Wanyaheru(Buha) kwa kuwavika sifa bandia wanasiasa. Wanyaheru ndiyo Waha halisi na HERU JUU ndiyo BUHA, wengine wote ni RUNDI
Duh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…