Mwamnyeto kuzikosa mechi muhimu sana za Al-Merreikh ni fundisho kwake na wazawa

Mwamnyeto kuzikosa mechi muhimu sana za Al-Merreikh ni fundisho kwake na wazawa

kuna kazi halaf kuna life binafsi ya mtu hivi vitu usivichanganye yule anafanya kazi kwa mkataba elewa hilo
 
Kwamba kutomuacha kwako ndio mzee wako atapata nafuu au?

Binafsi ningekuwa mzazi wake mwamnyeto ningempa go ahead aende akapambanie kibarua chake kwanza maana kibarua chake ndio kinacholipia bill hospitalini

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Angekuwa Nkane nisingejali sana, lakini kwa nahodha wa timu haijakaa vizuri. Mfano, kama clatous Chama asingesafiri na timu kwenda Zambia kwenye mechi dhidi ya power Dynamos Simba isingeingia makundi.
 
Swali la masingi

Mwamnyeto ni doctor?

Kwamba kubaki kwake nchini ndio mzee wake ndio akapata nafuu au?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile ap
Huduma zetu za afya si rafiki kama unavyodhani, mimi mdogo wangu alilazwa hosipitali ya Mwananyamala asubuhi apelekewe chai na kumuogesha, mchana apelekewe chakula na kwenda madukani kununua dawa zilizoandikwa na dakitari! Jioni apelekewe chakula. Tanzania hosipitali za serikali hazihudumii lolote zaidi ya dakitari kukuandikia dawa na nesi kumpa dawa kama utakuwa umeinunua na kama umekwenda kucheza mpira watakusubiri urudi ili wampe dawa kama atakuwa bado yuko hai.
Ukiwa hauna ndugu yote haya niliyoyaandika utaona ni porojo na hautajua kuwa kuna watu wanakufa kwa kukosa mtu wa kuwanunulia dawa, nenda hosipitali ukaone jinsi wagonjwa wanavyosaidiwa dawa na chakula na manesi au watu wanaokwenda kuwaona wagonjwa wao.
 
kuna kazi halaf kuna life binafsi ya mtu hivi vitu usivichanganye yule anafanya kazi kwa mkataba elewa hilo
Ndio uswahili wenyewe huo, kama mzee Mwamnyeto amefikia umri alionao lakini hana mtoto mwingine, shemeji, ndugu, jirani wala waumini wenzake wanaoweza kumsaidia siku mbili tatu wakati akimsubiri Bakari arejee kutoka Rwanda basi ndio uswahili kedekede. Na kama mchezaji hana ndugu, rafiki, jirani wala muumini mwenzake anaeweza kumuomba amhudumie baba yake wake yeye anatekeleza kazi ya kuipeleka timu yake makundi japo kwenye first leg basi kijana is immature kuweza kumudu kazi ya unahodha wa timu kubwa yenye malengo kama Yanga. Mzee kama anakufa atakufa na kama anapona anapona hata bila ya Bakari, maadam mzee anapatiwa matibabu sahihi. Bakari anaweza kuamuru mzazi apelekwe kwenye hospitali ya private hata bila yeye kuwepo Tanga. Anyway labda kuna sababu nyingine kubwa zaidi ya ugonjwa wa baba ya kuikosa mechi ila uongozi unatuficha. Wakati mwingine uongozi unaweza kutoa sababu ya uongo ili kuficha kosa lao kwa mchezaji au kosa la mchezaji ili kuimarisha umoja ndani ya timu
 
Huduma zetu za afya si rafiki kama unavyodhani, mimi mdogo wangu alilazwa hosipitali ya Mwananyamala asubuhi apelekewe chai na kumuogesha, mchana apelekewe chakula na kwenda madukani kununua dawa zilizoandikwa na dakitari! Jioni apelekewe chakula. Tanzania hosipitali za serikali hazihudumii lolote zaidi ya dakitari kukuandikia dawa na nesi kumpa dawa kama utakuwa umeinunua na kama umekwenda kucheza mpira watakusubiri urudi ili wampe dawa kama atakuwa bado yuko hai.
Ukiwa hauna ndugu yote haya niliyoyaandika utaona ni porojo na hautajua kuwa kuna watu wanakufa kwa kukosa mtu wa kuwanunulia dawa, nenda hosipitali ukaone jinsi wagonjwa wanavyosaidiwa dawa na chakula na manesi au watu wanaokwenda kuwaona wagonjwa wao.
So ina maana mwamnyeto hana kaka dada mjomba shangazi wa kusimamia hayo masuala mpaka yeye mwenyewe aende akasimamie?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Huo ndio uswahili wenyewe kwa wachezaji wazawa. Baba akiwa mgonjwa sehemu yake sahihi ni hospitali na wajibu wa mchezaji kama Mwamnyeto ni kumkatia bima ya matibabu wazazi wake. Kwahiyo yeye alikwenda kufanya nini kwa baba yake? Je, kama mwamnyeto angekuwa anacheza mpira timu za Ulaya angerudi Tanga kumjulia hali baba yake mgonjwa kama alivyofanya? Akumbuke kuwa kocha wa Yanga sio Charles Mkwasa ambae anazifahamu mila na desturi zetu.
Yaani wewe unapaswa kuitwa mwehu, mjinga, mpumbavu na mshenzi.
 
Yaani wewe unapaswa kuitwa mwehu, mjinga, mpumbavu na mshenzi.
Matusi ndio dalili kuu ya mtu wa chini kabisa kwenye jamii, anatumia matusi kama silaha yake muhimu ya kuzuia kushindwa au mbadala wa kushindwa (low profile people). Jenga hoja kutetea uswahili tukuone. Timu kubwa yenye mashabiki wengi na uwekezaji mkubwa sana ishindwe kutimiza malengo yake eti kwasababu baba yako mgonjwa tu. Yaani Chama asicheze mechi ya kufuzu makundi kwasababu ameenda kupanga foleni ya baba yake hospitali.
 
Swali la masingi

Mwamnyeto ni doctor?

Kwamba kubaki kwake nchini ndio mzee wake ndio akapata nafuu au?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app

Mifano ya hivyo ni mingi sana. Objective aliyopewa kocha Gamondi na benchi lake la ufundi ni kuipeleka Yanga makundi la sivyo kibarua chake hakitaeleweka. Mchezaji muhimu sana (Kapteni) siku ya mwisho ya maandalizi ya mechi mchezaji anamwambia kocha wake kuwa hatakwenda kucheza kwakuwa baba yake hajisikii vizuri, habari kama hiyo LAZIMA itamchanganganya kila mdau lakini sanasana kocha ambae anajua umuhimu wa Bakari kundini. Amerudi na kufikia kwenye mbao ndefu ya kocha hadi aseme.
Mkeo anapojifungua wengi wetu huwa hatuendi hosipitali bali tunaenda muda wa kawaida wa kuona wagonjwa.
So ina maana mwamnyeto hana kaka dada mjomba shangazi wa kusimamia hayo masuala mpaka yeye mwenyewe aende akasimamie?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Usimpangie familia yake, hata wewe hautafurahi mtubaki akikupangia chakufanya kwenye familia yako, unaweza ukawa nao na wakawa na kasoro za kibinaadamu kama teja, udokozi na kutokupenda kushirikiana na ndugu, kumbuka kilichotokea Morogoro miezi mitatu iliyopita ambapo binti alimkana baba yake mzazi kiasi yule baba akawa anasaidiwa na majirani, alipofariki watu wakamtilia ngumu binti, pia huenda hsta humu JF kuna watu ambao hawaja watembelea wazazi wao kwa zaidi ya miaka ishirini(20)! Na hawategemei, hawa ni wale wanaowakataa watoto wao halali!
 
Aboubacar Titi Camara, mwamba mmoja wa Guinea akikipiga pale Liverpool enzi hizo, alikubali kucheza mechi licha ya kujulishwa kuwa baba yake mzazi amefariki. Alifunga goli na kwenda kwenye kona kuangua kilio

1696328459116.png
 
Mkeo anapojifungua wengi wetu huwa hatuendi hosipitali bali tunaenda muda wa kawaida wa kuona wagonjwa.

Usimpangie familia yake, hata wewe hautafurahi mtubaki akikupangia chakufanya kwenye familia yako, unaweza ukawa nao na wakawa na kasoro za kibinaadamu kama teja, udokozi na kutokupenda kushirikiana na ndugu, kumbuka kilichotokea Morogoro miezi mitatu iliyopita ambapo binti alimkana baba yake mzazi kiasi yule baba akawa anasaidiwa na majirani, alipofariki watu wakamtilia ngumu binti, pia huenda hsta humu JF kuna watu ambao hawaja watembelea wazazi wao kwa zaidi ya miaka ishirini(20)! Na hawategemei, hawa ni wale wanaowakataa watoto wao halali!
"Usimpangie familia yake" msemo huu ni dalili kuu ya uswahili uliokithiri. Una hiyari ya kuajiliwa au la, lakini ukishaajiliwa huna hiyari ya kufanya kazi. Hata huko serikalini hakuna likizo ya kwenda kuuguza mzazi wako. Wawekezaji wengi wanakataa kuwapa waswahili ajira kwasababu ya uswahili kama huu.
 
kuna kazi halaf kuna life binafsi ya mtu hivi vitu usivichanganye yule anafanya kazi kwa mkataba elewa hilo
Kuna sifa na tabia za wachezaji wakubwa. Mtu mzima aliyetimia hawezi kusahau/kuacha majukumu ya msingi kwasababu yoyote Ile bila kuyatafutia utaratibu
 
yeye ni daktari? alisaidia nini baba yake kupona? Kocha ni mzungu, na ana mipango yake. Klabu haiwezi kukosa kwenda makundi baada ya miaka 25 ya kusubiri kwasababu eti wewe baba yako ni mgonjwa tu hajafa.

UKo kwenye mipango ya kocha na first 11 ya kocha kwenye mechi ambayo inashikilia hatima ya kocha kubaki kwenye timu na hatima ya timu kutinga makundi baada ya miaka 25 halafu mchezaji muhimu (kapteni) anasema hawezi kwenda kucheza kwakuwa baba yake hana mtu wa kumkalia foleni ya kwenda kumuona dk wake wa tezi dume. Atakuchukia milele.

Mkuu umeeleweka vizuri, achana na hawa wanaoendekeza uswahili. Labda jamaa alienda kuwa karibu ili apokee mikoba ya mzee.
 
Mchezaji wa mpira siyo mashine kama roboti au trekta au tinganga.
Ana hisia, anachoka, anaumwa, ana sumbuliwa na sababu za kijamii n.k.

Kama hauna taarifa sahihi nini kimemsibu bora kukaa kimya. Msiwe mabingwa wa kulaumu.
Hoja yako ni nzuri kabisa.
Anaweza kuwa mzima kiafya, kifamilia lakini asiwe vizuri kisaikolojia.
Yapo mengi.
Ni ngumu kuwa vizuri kwa yote mwaka mzima.
 
Hoja yako ni nzuri kabisa.
Anaweza kuwa mzima kiafya, kifamilia lakini asiwe vizuri kisaikolojia.
Yapo mengi.
Ni ngumu kuwa vizuri kwa yote mwaka mzima.
Hakuna timu na kocha makini anaweza kupokea uswahili kama huo. Kocha na timu maombi yao ni kuona mchezaji analipwa vizuri, anakula vizuri, anapewa mafunzo na matibabu mazuri muda wote kwa wakati ili awe fiti 100% wakati wote kuitumikia club na sio kwenda kumuuguza mzazi. Matukio pekee yanayokubalika tena kwa huzuni kubwa ni mchezaji kuwa nje ya uwanja kwasababu za ugonjwa na kuumia. Mchezaji mwenye historia ya kukosa mechi kwasababu yoyote ile ya ugonjwa, majeraha, nidhamu ndani na nje ya uwanja na sababu za kifamilia za mara kwa mara huwa hapewi nafasi kusajiliwa na timu kubwa makini au kupewa malipo makubwa ambayo hutayatumikia ipasavyo. Mchezaji mkubwa anatakuwa awe na roho na akili yake kubwa pia.
 
Back
Top Bottom