Mwamposa ajitetea kuwakamua waumini 'sadaka ya kujimaliza', atoa ufafanuzi mujarabu

Mwamposa ajitetea kuwakamua waumini 'sadaka ya kujimaliza', atoa ufafanuzi mujarabu

Sadaka ya kujimaliza ni wizi sawa na wizi mwingine TU hakuna fundisho kama Hilo.
Sadaka zitolewaje utaratibu maandiko yameweka wazi.
 
Anachosema Mwamposa ni kua sio tu anahitaji chote ulichoenda nacho kanisani, bali na hata kile ulichokiacha benki na nyumbani pia anakihitaji.
Huu ni wizi kabisa.
Mungu sio wa kutoa toa hela Kila wakati.
 
Mashuhuda wengi makanisani huwa ni feki wamepangwa au huwa sio watu halisi.
Ukitaka kujua hili wafatilie hao watoa ushuhuda baada ibada ujue wakaapo ni lazima wakupotee kwenye kona akikata TU kona upotea ujui uelekeo.
Hawa magician Wana michezo mingi sana
 
Kumbe wale wanaotembe huku wanaimba
NATEMBEA NA YESU, NATEMBEA NA YESU ndio wametoka huko Kwa Mwamaposa
 
Yule wa Uganda aliitwa nani vile...Kinwetere sijui?

Ipo siku nia na hila za Mwamposa zitakuwa wazi
Joseph Kibweteere!

Mungu aepushe mabaya yasije tokea kama Yale! Na hv vitu mda mwingine ni ngumu sana kumshauri mtu akakuelewa
 
Kila kitu kitapimwa kwa maandiko, ni wapi pameandikwa aina hiyo ya sadaka? Kama hakuna itabaki kuwa utundu tu wa kinabii.
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Mtume Boneface Mwamposa (Bulldozer) amefafanua kwa ufasaha maana ya "sadaka ya kujimaliza" inayotolewa na waumini wa kanisa lake baada ya kupokea shutuma mbalimbali kutoka kwa wananchi kwamba amekuwa akiwakamua waumini hela zote hadi wanakosa nauli ya kurudia majumbani kwao.

Ufafanuzi uliotoka ni kwamba kutoa sadaka ya kujimaliza sio kutoa fedha zote ambazo mtu amekwenda nazo kanisani. La hasha! Maana ya sadaka ya kujimaliza ni kutoa fedha zako zote ulizonazo benki na kuziwasilisha kwa mtume kama sadaka. Kwa mfano, kama una akaunti 5 kwenye benki tofauti, komba pesa zote zilizomo kwenye akaunti hizo umtolee Mungu wako. Hii ndio maana halisi ya sadaka ya kujimaliza. Yaani unajimaliza kabisa na kuanza upya!

Mtume amesema hayo zikiwa zimesalia siku chache kabla ya mkesha wa mwaka mpya unaoenda kwa kaulimbiu ya "vuka na chako" utakaofanyika kanisani kwake katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.

MAONI YANGU
Binafsi nimewahi kusimuliwa na muumini mmoja aliyetoa sadaka fedha zote alizokuwa nazo hadi nauli lakini wakati anaondoka kwa miguu kuelekea kwake Gongolamboto akitokea Kawe, mtume akamfanyia muujiza akaokota noti ya Tsh 5000 akaitumia kama nauli, yeye na wanawe wawili aliokuwa ameandamana nao.

Afadhali sasa ufafanuzi umewekwa wazi kwani waumini na wananchi walikuwa hasa hawafahamu maana ya sadaka ya kujimaliza. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mungu wa Mwamposa hajawahi kushindwa.

Nawasilisha.

Pia soma >
Sadaka ya kujimaliza ya kwa Mwamposa inatia watu umasikini
Watu tu wanamsingizia


Kama umewahi kusali Kawe, sadaka ya kujimaliza ni ile pesa yenye thamani kubwa kuliko zote.
Mfano kwenye wallet una note ya elfu 5,2,,, 10
Hapo yenye thamani kubwa ni 10k
 
Watu tu wanamsingizia


Kama umewahi kusali Kawe, sadaka ya kujimaliza ni ile pesa yenye thamani kubwa kuliko zote.
Mfano kwenye wallet una note ya elfu 5,2,,, 10
Hapo yenye thamani kubwa ni 10k
Tulia. Hujawahi kumsikia akitoa ufafanuzi. Ina maana huu ufafanuzi aliotoa amejichanganya mwenyewe? Wewe ni nani hadi uupinge ufafanuzi wa Mwamposa? Acha ujuaji uchwara mkuu.
 
Tulia. Hujawahi kumsikia akitoa ufafanuzi. Ina maana huu ufafanuzi aliotoa amejichanganya mwenyewe? Wewe ni nani hadi uupinge ufafanuzi wa Mwamposa? Acha ujuaji uchwara mkuu.
Kama hujawahi kwenda kusali Kawe Kwa Mwamposa na kutoa hiyo sadaka ya kujimaliza basi wewe ndio utulie na uache ujuaji uchwara, na uache kupotosha umma.
 
Back
Top Bottom