Kweli ni wafuasii ni wapumbavu na askofu wao ni mshirikinaKwani uongo? Wafuasi wa Mwamposa ni misukule! Ni kama vichwa vyao vimekatwa! Hawafikirii/hawana akili kabisa!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli ni wafuasii ni wapumbavu na askofu wao ni mshirikinaKwani uongo? Wafuasi wa Mwamposa ni misukule! Ni kama vichwa vyao vimekatwa! Hawafikirii/hawana akili kabisa!
Ni kwa vile anajua ni tapelinsurvival yake ni kuwaunga mkono wahuni wenzie ccmKashasoma mchezo lazima ale nao ili aendelee kula.
ni mnyaki sio mzamiba. ila hatuongelei kabila kwasababu hata wanyakyusa wenzake wanamkataa.Zambia 1 sio nyakyusa hio hata kiboko ni Mkongo huyo ni Mzambia akifanya fyoloko anarudishwa mpakani pale aende kwao
Mkuu unashangaa hilo? Ukishaona mtu anaamini mahubiri ya aina ya watu wa Mwamposa, ujue hata uelewa wake ni duni. Kibwetere yeye aliwachoma kabisa waumini wa aina hiyo.Nimemshangaa sana huyu jamaa jinsi anavyowashikia akili waumini wake na kumhusisha Mungu na mambo ya kishetani (CCM). Huu uthubutu kaupata wapi? Analindwa na nani hadi awapotoshe watu hadharani kiasi hiki?
Kichaka cha wapigajiMtanzania yeyote mwenye pesa ukimuona yuko CCM jua kuwa huyo pesa zake ni za haramu.
CCM ndio njia nzuri ya kuzilinda pesa zako za haramu katika nchi hii
Kada maarufu wa CCM na Askofu wa kanisa la Arise and Shine, Dr Boniface Mwamposa (Buldozer) leo amewahimiza waumini wake waende wakajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura na kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Nabii huyo amesema hayo leo jioni wakati akiwahubiria mamia ya waumini wake waliofurika kwenye kiwanja alipokuwa akihubiri na kutoa mafundisho ya Yesu. "Hata Yesu alihesabiwa, hivyo nawasihi watu wangu wote mwende mjiandikishe na kuwapigia kura wagombea wa CCM". Amesema.
Askofu Mwamposa alitumia takribani saa nzima kabla ya kuanza mahubiri kuwahimiza, kuwasihi na kuwashawishi wafuasi wake wafanye kama alivyowaagiza na Mungu atawabariki.
MAONI YANGU
Huyu askofu sasa naona mahubiri yanakaribia kumshinda. Hakuwa na haja ya kuwahimiza wafuasi wake kuwapigia kura CCM kwa sababu waumini wake wote sio wanaCCM. Asitake kutumia fimbo ya upako na miujiza kulazimisha mambo kwa matakwa yake binafsi. Angeishia tu kuwahimiza wakajiandikishe kuliko kwenda mbali zaidi kuwaelekeza aina ya wagombea watakaowapigia kura. Hii ni sawa na kuwageuza binadamu wenzake kuwa misukule yake.Haifai, haipendezi na Mungu hapendi.
Kukubali kutapeliwa kupitia manabii tapeli, lazima uwe huna akili, uwe umekosa maarifa. Mwenye akiki timamu hawezi kutumia jasho lake kutafuta hela halafu akaitumia hela hiyo kwenda kununua udongo (siyo ardhi)!! Lazima ukose maarifa kabisa.Kwani uongo? Wafuasi wa Mwamposa ni misukule! Ni kama vichwa vyao vimekatwa! Hawafikirii/hawana akili kabisa!
Walimuonea bure kiboko ya wachawi ilhali matapeli wamejaa kila kona. Inauma sana.Nchi imejaa manabii fake. Wanalikufuru jina la Bwana kwa kulitumia jina lake kuwatapeli wajinga waliokosa maarifa.
Huu ni utimilifu wa lile neno lisemalo, "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa."
Mtu anauziwa mchanga, anauziwa maji, na bado anaamini anayemuuzia ni mtumishi wa Bwana!!
Niambieni ni wapi imeandikwa, Kristo aliwaponya wagonjwa, aliwaponya vilema na kuwafufua wafu kwa malipo ya fedha.
Kuwa mkristo ni kukubali kufuata yale aliyoyatenda Kristo. Kristo alijifanya mtu, akaubeba mwili wa kibinadamu ili atuoneshe namna mwanadamu astahilivyo kutenda.
Tapeli Mwamposa anatumwa na dolaMkuu umemaliza kila kitu. Huyu jamaa amelewa hela za bwerere, hasa baada ya kujenga hoteli ya nyota 5 inayomuingizia mamilioni ya pesa kila siku. Heri kuvimbiwa chakula kuliko kuvimbiwa fedha. Tangu Mwamposa alipovimbiwa pesa, anajiona yeye ndiye kila kitu hapa nchini. Mungu amsamehe bure.