LGE2024 Mwamposa: Watu wangu nenda mjiandikishe mkapigie kura CCM

LGE2024 Mwamposa: Watu wangu nenda mjiandikishe mkapigie kura CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kada maarufu wa CCM na Askofu wa kanisa la Arise and Shine, Dr Boniface Mwamposa (Buldozer) leo amewahimiza waumini wake waende wakajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura na kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nabii huyo amesema hayo leo jioni wakati akiwahubiria mamia ya waumini wake waliofurika kwenye kiwanja alipokuwa akihubiri na kutoa mafundisho ya Yesu. "Hata Yesu alihesabiwa, hivyo nawasihi watu wangu wote mwende mjiandikishe na kuwapigia kura wagombea wa CCM". Amesema.

Askofu Mwamposa alitumia takribani saa nzima kabla ya kuanza mahubiri kuwahimiza, kuwasihi na kuwashawishi wafuasi wake wafanye kama alivyowaagiza na Mungu atawabariki.

MAONI YANGU
Huyu askofu sasa naona mahubiri yanakaribia kumshinda. Hakuwa na haja ya kuwahimiza wafuasi wake kuwapigia kura CCM kwa sababu waumini wake wote sio wanaCCM.

Asitake kutumia fimbo ya upako na miujiza kulazimisha mambo kwa matakwa yake binafsi. Angeishia tu kuwahimiza wakajiandikishe kuliko kwenda mbali zaidi kuwaelekeza aina ya wagombea watakaowapigia kura.

Hii ni sawa na kuwageuza binadamu wenzake kuwa misukule yake. Haifai, haipendezi na Mungu hapendi
Hapa huwezi sikia ccm wakisema Dini isichanganywe na siasa. Lakini wakikemewa kupitia waraka Sasa ndio shughuli yake unaiona.
 
Nchi imejaa manabii fake. Wanalikufuru jina la Bwana kwa kulitumia jina lake kuwatapeli wajinga waliokosa maarifa.

Huu ni utimilifu wa lile neno lisemalo, "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa."

Mtu anauziwa mchanga, anauziwa maji, na bado anaamini anayemuuzia ni mtumishi wa Bwana!!

Niambieni ni wapi imeandikwa, Kristo aliwaponya wagonjwa, aliwaponya vilema na kuwafufua wafu kwa malipo ya fedha.

Kuwa mkristo ni kukubali kufuata yale aliyoyatenda Kristo. Kristo alijifanya mtu, akaubeba mwili wa kibinadamu ili atuoneshe namna mwanadamu astahilivyo kutenda.

Ushindi wa CCM sio kushindwa kwa Chadema wala ACT bali ni kumkataa Mungu katika Taifa hili na adhabu yake itawaumiza sana watu kama inavyokuwa kule Israel walipoanza kujisahau na kuona kuwa ushoga ni haki yao na kujitangaza hadharani huku wakiwakejeli wale wanaoupinga . Matokeo yake Mungu amekaa mbali na sasa Magaidi wanaingiwa na roho ya vita na mauaji na kuanza kazi ya kumfurahisha shetani kuliangamiza lile taifa teule. Waisrael wangemsikiliza Yesu na kuzitii amri za Mungu leo wanaishi kwa amani sana na Ndugu zao Waarabu maana waarabu sio adui yao. Adui zao walishaamalizwa siku nyingi sana na Daudi na Suleimani. Wengine waliopou adui unaotengenezwa kutokana na kumkataa Masihi wa Mungu awatawale kiMungu.

CCM nayo ilishasema haimtegemei Mungu kutawala apende asipende watawala na kubaki madarakani.

Sasa Mwamposa kutumia mgongo wa kanisa kuomba kura kwa CCM ni unafiki na uchawa wa kiLucufer kwa sababu CCM walishasema hawahitaji kura kushinda . Sasa huyo waakala wa shetani na CCM anapata wapi mamlaka ya kuomba kura wakati wenye chama walishasema hawahitaji kura za wananchi wala Mapenzi ya Mungu kushinda bali kwao ushindi ni lazima.

Waumini wote halasishaneni maana ushindi wa CCM ni wazi sasa kuwa utakua ni kufuru kubwa sana kwa Mungu aliyetuumba na kutuweka hapa Tanzania na rasilimali zote alizoumba yeye na sio CCM bali ni mapenzi yake Kutuumbia hii nchi.
CCM ikishinda Mungu atadharauliwa sana hapa Tanzania . Hili wakristo na waislam tusikubali kamwe. Tuna vyama viwili vilivyoonyesha angalau kulinda heshima na utu na angalau kutetea Haki na kupinga dhulma ,ambavyo ni CHADEMA na ACT . Tujipange tu wachague kuanzia serikali mitaa ,udiwani ,ubunge na urais ili CCM wakae pembeni watubu na kumheshimu Mungu kuliko mwenyekiti wao na wajue kuwa mwenyekiti wao na serikali yake wanaweza kutoa uhai wa mtu lakini hawawezi kuweka pumzi ya mtu wala kuleta mvua juu ya ardhi. Ndio maana hata wao watakufa kama wengine na watarejea kwenye asili ya viumbe vyote kama wengine hivyo kuwategemea CCM na kukufuru Mungu ni laana tosha kwa Taifa hili.

Kataa CCM, kataa Wahuni ,kataa wauaji na watakaji ,kataa tozo kubwa ,kataa , mfumuko wa bei,kataa matumizi makubwa ya serikali , kataa ufisadi , kataa kuuzwa kwa ardhi yetu ,kataa kumkufuru Mungu na kutukuza CCM ,kataa machawa .

Pigeni Kura nyingi kwa ACT na Chadema kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa . Hivi ni vyama vyenye kumjua Mungu wa Haki.
 
Huyo jamaa Kiboko ya wachawi ukimtaja hua naona sura yake alivyokua anawakejeli watanzania kule Kongo. Kwa kweli CCM imetuweza.
Nabaki kucheka tu jinsi wanavyotuona Nyani.
Tanzania ni nchi ambayo mtu unaweza kuja mikono mitupu ukaondoka na mamilioni ya hela. Haiingii akilini kuona yule tapeli amewaibia pesa wananchi kwa miaka chungu nzima wakati serikali inayopaswa kuwalinda dhidi ya matapeli ipo kimya. Inauma sana.
 
Sio Mazembe huyo ni Mzambia alielowea Mbeya akauzauza mafuta sheli kidogo pale mpakani
Basi kumbe hana tofauti na kiboko ya wachawi aliyefurushwa nchini. Ni kwanini yeye bado anaruhusiwa kuendelea kuwatapeli wananchi? Hii jeuri anaipata kutoka kwenye mamlaka ya nchi au anaipata wapi?
 
Kada maarufu wa CCM na Askofu wa kanisa la Arise and Shine, Dr Boniface Mwamposa (Buldozer) leo amewahimiza waumini wake waende wakajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura na kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nabii huyo amesema hayo leo jioni wakati akiwahubiria mamia ya waumini wake waliofurika kwenye kiwanja alipokuwa akihubiri na kutoa mafundisho ya Yesu. "Hata Yesu alihesabiwa, hivyo nawasihi watu wangu wote mwende mjiandikishe na kuwapigia kura wagombea wa CCM". Amesema.

Askofu Mwamposa alitumia takribani saa nzima kabla ya kuanza mahubiri kuwahimiza, kuwasihi na kuwashawishi wafuasi wake wafanye kama alivyowaagiza na Mungu atawabariki.

MAONI YANGU
Huyu askofu sasa naona mahubiri yanakaribia kumshinda. Hakuwa na haja ya kuwahimiza wafuasi wake kuwapigia kura CCM kwa sababu waumini wake wote sio wanaCCM.

Asitake kutumia fimbo ya upako na miujiza kulazimisha mambo kwa matakwa yake binafsi. Angeishia tu kuwahimiza wakajiandikishe kuliko kwenda mbali zaidi kuwaelekeza aina ya wagombea watakaowapigia kura.

Hii ni sawa na kuwageuza binadamu wenzake kuwa misukule yake. Haifai, haipendezi na Mungu hapendi.
Fungua na wewe kanisa lako utakuwa na waumini kisha wahimize wakahaiikishe wanaipigia chadema ,hakuna haja ya kuona wivu kwa mwamposa
 
Na akina mama huku mtaani huwaambia kitu kuhusu Mwamposa mpaka wapigwe na kitu kizito ndio wanashtuka
Akina mama, hasa wenye uwezo mdogo wa kufikiri, ni wafuasi wakubwa wa tapeli Mwamposa. Juzi mama mmoja kachukua Tsh 200,000 aliyopewa na mumewe kama pesa ya matumizi kaipeleka yote kwa Mwamposa kutoa sadaka ya kujimaliza.

Mume aliporudi akakuta pesa yote aliyoipata kwa jasho imeenda kwa Mwamposa, alikasirika sana akaanzisha timbwili la kufa mtu. Mpaka muda huu ninapotoa taarifa hii, wanandoa hao tayari wameishagawana mbao.
 
Back
Top Bottom