LGE2024 Mwamposa: Watu wangu nenda mjiandikishe mkapigie kura CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kada maarufu wa CCM na Askofu wa kanisa la Arise and Shine, Dr Boniface Mwamposa (Buldozer) leo amewahimiza waumini wake waende wakajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura na kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nabii huyo amesema hayo leo jioni wakati akiwahubiria mamia ya waumini wake waliofurika kwenye kiwanja alipokuwa akihubiri na kutoa mafundisho ya Yesu. "Hata Yesu alihesabiwa, hivyo nawasihi watu wangu wote mwende mjiandikishe na kuwapigia kura wagombea wa CCM". Amesema.

Askofu Mwamposa alitumia takribani saa nzima kabla ya kuanza mahubiri kuwahimiza, kuwasihi na kuwashawishi wafuasi wake wafanye kama alivyowaagiza na Mungu atawabariki.

MAONI YANGU
Huyu askofu sasa naona mahubiri yanakaribia kumshinda. Hakuwa na haja ya kuwahimiza wafuasi wake kuwapigia kura CCM kwa sababu waumini wake wote sio wanaCCM.

Asitake kutumia fimbo ya upako na miujiza kulazimisha mambo kwa matakwa yake binafsi. Angeishia tu kuwahimiza wakajiandikishe kuliko kwenda mbali zaidi kuwaelekeza aina ya wagombea watakaowapigia kura.

Hii ni sawa na kuwageuza binadamu wenzake kuwa misukule yake. Haifai, haipendezi na Mungu hapendi.

Hosea 4:6​

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
 
Kada maarufu wa CCM na Askofu wa kanisa la Arise and Shine, Dr Boniface Mwamposa (Buldozer) leo amewahimiza waumini wake waende wakajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura na kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nabii huyo amesema hayo leo jioni wakati akiwahubiria mamia ya waumini wake waliofurika kwenye kiwanja alipokuwa akihubiri na kutoa mafundisho ya Yesu. "Hata Yesu alihesabiwa, hivyo nawasihi watu wangu wote mwende mjiandikishe na kuwapigia kura wagombea wa CCM". Amesema.

Askofu Mwamposa alitumia takribani saa nzima kabla ya kuanza mahubiri kuwahimiza, kuwasihi na kuwashawishi wafuasi wake wafanye kama alivyowaagiza na Mungu atawabariki.

MAONI YANGU
Huyu askofu sasa naona mahubiri yanakaribia kumshinda. Hakuwa na haja ya kuwahimiza wafuasi wake kuwapigia kura CCM kwa sababu waumini wake wote sio wanaCCM.

Asitake kutumia fimbo ya upako na miujiza kulazimisha mambo kwa matakwa yake binafsi. Angeishia tu kuwahimiza wakajiandikishe kuliko kwenda mbali zaidi kuwaelekeza aina ya wagombea watakaowapigia kura.

Hii ni sawa na kuwageuza binadamu wenzake kuwa misukule yake. Haifai, haipendezi na Mungu hapendi.
Mimi toka miaka ile mtu akinambia anasali au anamfatilia mwamposa namuona kaishiwa kabisa na ni mfu anayetembea 😄😄
 
Kafanya kosa kubwa sana huyu Nabii, kura ni siri ya mtu na wala sio agizo kutoka kwa mtu mwingine.... Askofu ameharibu kila kitu, asipoangalia ataligawa hata kanisa lake.
Mwamposa anajua anachokifanya.

Hakuna kanisa litakalogawanyika, ataendelea kupiga hela na kuwa bilionea hadi hapo serikali itakapoona sasa inatosha.

Hana njia njia nyingine zaidi ya kuwapigia magoti CCM ili wamfumbie macho aendelee kupiga hela.
 
Nchi huru hii acha Mwamposa afanye jambo jema kwake na kwa utajiri wake
Hakuna mtu anayezuia utajiri wake mkuu. Lakini kamwe asitumie migongo ya maskini kujitajirisha kwa manufaa yake binafsi kwa misingi ya kishetani.
 
Huyu amekuwa raifiki yake mkubwa sana wa Paul makonda, sijui wanna ajenda gani ya siri ?
Inawezekana wanashirikiana katika utekaji na kuwapoteza watu. Hawa watu ni majitu ya ajabu sana. Ukiona askofu yeyote anashirikiana na CCM ujue wote ni wafuasi wa shetani.
 
Hakuna mtu anayezuia utajiri wake mkuu. Lakini kamwe asitumie migongo ya maskini kujitajirisha kwa manufaa yake binafsi kwa misingi ya kishetani.
Bila masikini hakuna tajiri, wacha atumie fursa kwasababu hakuna alie mshikia bunduki kuja hapo
 
Kwa hiyo wewe unaona ni sawa tu atumie ulaghai kwa masikini ili kujitajirisha mkuu?
 
Mwamposa anajua anachokifanya.

Hakuna kanisa litakalogawanyika, ataendelea kupiga hela na kuwa bilionea hadi hapo serikali itakapoona sasa inatosha.

Hana njia njia nyingine zaidi ya kuwapigia magoti CCM ili wamfumbie macho aendelee kupiga hela.
Na atazipiga sana. Huku wanapigwa na Mwamposa na kule wanapigwa na mafisadi wa CCM. Masikini wa nchi hii hawana pa kupumulia. Tuombe Yesu arudi haraka kuja kuwakomboa.
 
Kwa hiyo wewe unaona ni sawa tu atumie ulaghai kwa masikini ili kujitajirisha mkuu?
Naam hakuna tatizo kutumia masikini kutajirika, hili neno ulaghai silikubali , kwasababu wangekuwa hawapati msaada wasinge kwenda kwa Mwamposa kila siku wakati hawalazimishwi
 
Msaada gani wanapata mkuu? Kuwashirikisha watu kwenye maigizo ya shujuda feki ndiyo mafanikio unayoyaona? Ama kweli usilolijua litakusumbua sana.
 
sasa kama hawapati msaada wanafata nini ikiwa hakuna anaelazimishwa kwenda kwa Mwamposa? hapa ndio pa kutafakari badala ya kusema kuna ulaghai , mimi nina amini bila shaka wanapata wanachokitaka ndio maana kila siku wanakwenda
 
Kada maarufu wa CCM na Askofu wa kanisa la Arise and Shine, Dr Boniface Mwamposa (Buldozer) leo amewahimiza waumini wake waende wakajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura na kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nabii huyo amesema hayo leo jioni wakati akiwahubiria mamia ya waumini wake waliofurika kwenye kiwanja alipokuwa akihubiri na kutoa mafundisho ya Yesu. "Hata Yesu alihesabiwa, hivyo nawasihi watu wangu wote mwende mjiandikishe na kuwapigia kura wagombea wa CCM". Amesema.

Askofu Mwamposa alitumia takribani saa nzima kabla ya kuanza mahubiri kuwahimiza, kuwasihi na kuwashawishi wafuasi wake wafanye kama alivyowaagiza na Mungu atawabariki.

MAONI YANGU
Huyu askofu sasa naona mahubiri yanakaribia kumshinda. Hakuwa na haja ya kuwahimiza wafuasi wake kuwapigia kura CCM kwa sababu waumini wake wote sio wanaCCM.

Asitake kutumia fimbo ya upako na miujiza kulazimisha mambo kwa matakwa yake binafsi. Angeishia tu kuwahimiza wakajiandikishe kuliko kwenda mbali zaidi kuwaelekeza aina ya wagombea watakaowapigia kura.

Hii ni sawa na kuwageuza binadamu wenzake kuwa misukule yake. Haifai, haipendezi na Mungu hapendi.
Weka ushahidi.
 
Akina mama, hasa wenye uwezo mdogo wa kufikiri, ni wafuasi wakubwa wa tapeli Mwamposa. Juzi mama mmoja kachukua Tsh 200,000 aliyopewa na mumewe kama pesa ya matumizi kaipeleka yote kwa Mwamposa kutoa sadaka ya kujimaliza.

Mume aliporudi akakuta pesa yote aliyoipata kwa jasho imeenda kwa Mwamposa, alikasirika sana akaanzisha timbwili la kufa mtu. Mpaka muda huu ninapotoa taarifa hii, wanandoa hao tayari wameishagawana mbao.
Mwanamke si amejimaliza
 
Back
Top Bottom