LGE2024 Mwamposa: Watu wangu nenda mjiandikishe mkapigie kura CCM

LGE2024 Mwamposa: Watu wangu nenda mjiandikishe mkapigie kura CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kada maarufu wa CCM na Askofu wa kanisa la Arise and Shine, Dr Boniface Mwamposa (Buldozer) leo amewahimiza waumini wake waende wakajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura na kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nabii huyo amesema hayo leo jioni wakati akiwahubiria mamia ya waumini wake waliofurika kwenye kiwanja alipokuwa akihubiri na kutoa mafundisho ya Yesu. "Hata Yesu alihesabiwa, hivyo nawasihi watu wangu wote mwende mjiandikishe na kuwapigia kura wagombea wa CCM". Amesema.

Askofu Mwamposa alitumia takribani saa nzima kabla ya kuanza mahubiri kuwahimiza, kuwasihi na kuwashawishi wafuasi wake wafanye kama alivyowaagiza na Mungu atawabariki.

MAONI YANGU
Huyu askofu sasa naona mahubiri yanakaribia kumshinda. Hakuwa na haja ya kuwahimiza wafuasi wake kuwapigia kura CCM kwa sababu waumini wake wote sio wanaCCM.

Asitake kutumia fimbo ya upako na miujiza kulazimisha mambo kwa matakwa yake binafsi. Angeishia tu kuwahimiza wakajiandikishe kuliko kwenda mbali zaidi kuwaelekeza aina ya wagombea watakaowapigia kura.

Hii ni sawa na kuwageuza binadamu wenzake kuwa misukule yake. Haifai, haipendezi na Mungu hapendi.

hilo tapeli achaneni nalo. his days are numbered!

JESUS is Lord &Savior
 
Noma sana!
hatari iliyopo, kama leo anaweza kuwaelekeza anaowaita "watu wangu" kupigia ccm, kesho anaweza kuwaelekeza kupigia mtu wake toka kwenye dini yake, na siku ingine toka kwenye kabila lake. ameongea ujinga mkubwa sana.
sa
 
Viongozi wengi wakubwa wa Dini kubwa Chadema hawataki hata kuisikia

Chadema mtu anayeshimu Viongozi wakubwa kidini ila kibinafsi sio kichama ni Mbowe tu ana adabu kwa maaskofu wa dini yake KKKT nao ni wawili tu anaowaheshimu sana Askofu Shoo na Bagonza tu pamoja na kuwa KKKT ina maaskofu kibao

Askofu mkuu wa KKkT Malasusa Mbowe na Chadema hawana mpango kumheshimu japo ndie askofu wake mkuu KKKT .Magufuli CCM mkatotoliki alipooombwa na CCM kugombea uraisi alikimbia mbio kwenda kwenda kwa Mufti, kardinali na Askofu mkuu wa KKKT Malasusa nk kuomba ushauri na maombi

Lisu na Mnyika Katoliki lakini hawana adabu kwa maaskofu wao

CCM ina adabu kwa Viongozi wote wa Dini kubwwa wa juuu awe mufti wa Bakwata au Kardinali yeyote wa katoliki au askofu mkuu ,mtume au nabii mwenyewe umati wa watu wafuasi wake nchi nzima awe Mwamposya, Askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God, nk CCM ina waheshimu mno

Ndio maana hata kukiwa na issue serious hutaka kuonana nao na kuwa na mazungumzo na kupokea ushauri kwao

Sababu hao serikali huwaheshimu wagumu kutoa tamko la hovyo hadi wajiridhishe wanachotamka kimeenea kwa vigezo vyote vya hadhi zao za vyeo vyao vya kidini ? Tofauti na hao wengineo ambao huropoka tu kama vile wana tumbo la kuharisha wanaharisha chochote kupitia mdomoni

Viongozi wakuu wa dini kubwa wenye watu wengi nchi nzima ndio wenye watu ukiwadhalilisha unategemea nini? Ushinde uchaguzi sio rahisi
 
Back
Top Bottom