LGE2024 Mwamposa: Watu wangu nenda mjiandikishe mkapigie kura CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Huyu ni mchonganishi sana. soon atatokea shehe naye ataelekeza watu wapigie cuf. atakuja mchungaji ambaye hamkubali mwamposa atataka aongee kumkosoa na kuelekeza watu wampigie fulani, analeta fujo tu, shida ni shule na exposure. ukipata pesa za kitapeli wakati hukutarajia unajiona kama mkuuubwa. yaani yeye ndiye wa kuamulia watanzania hatima zao? hadi wasomi kabisa wanapokea maelekezo toka kwa huyu mnyakyusa tapeli wa dini?

wapentekoste najua wote wanapinga mafundisho ya mwamposa, wakatoliki wanapinga mafundisho yake, walutheran kadhalika. vipi hao nao wakijiunga wakatoa misimamo na maelekezo? yaani yeye kukusanya vile watu anaamini amekusanya watanzania wote? na vipi dini ya kiislam nao wakianza hivyo kuelekeza watu wapigie kuwa yule wanayemtaka? huyu anawaharibia though yeye anafikiri anawasaidia ccm.

Huyu jamaa kalewa. Ni ulevi wa umashuhuri. Anavyokusanya watu vile anahisi yeye yuko juu ya kitu chochote Tanzania 🇹🇿.
 
Kada maarufu wa CCM na Askofu wa kanisa la Arise and Shine, Dr Boniface Mwamposa (Buldozer) leo amewahimiza waumini wake waende wakajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura na kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nabii huyo amesema hayo leo jioni wakati akiwahubiria mamia ya waumini wake waliofurika kwenye kiwanja alipokuwa akihubiri na kutoa mafundisho ya Yesu. "Hata Yesu alihesabiwa, hivyo nawasihi watu wangu wote mwende mjiandikishe na kuwapigia kura wagombea wa CCM". Amesema.

Askofu Mwamposa alitumia takribani saa nzima kabla ya kuanza mahubiri kuwahimiza, kuwasihi na kuwashawishi wafuasi wake wafanye kama alivyowaagiza na Mungu atawabariki.

MAONI YANGU
Huyu askofu sasa naona mahubiri yanakaribia kumshinda. Hakuwa na haja ya kuwahimiza wafuasi wake kuwapigia kura CCM kwa sababu waumini wake wote sio wanaCCM.

Asitake kutumia fimbo ya upako na miujiza kulazimisha mambo kwa matakwa yake binafsi. Angeishia tu kuwahimiza wakajiandikishe kuliko kwenda mbali zaidi kuwaelekeza aina ya wagombea watakaowapigia kura.

Hii ni sawa na kuwageuza binadamu wenzake kuwa misukule yake. Haifai, haipendezi na Mungu hapendi.
Kavideo tuone alivyokuwa akiongea
 
Huyo ni KIBWETERE wa kizazi kipya. Onyo kwa wafuasi wake, yatawakuta ya Kibwetere siku sio nyingi maana hata maandiko yametahadharisha kuwa SIO KILA ATAJAYE JINA LANGU NI WANGU.
Shauri yenu

Yawakute mara ya pili bro!!?
Yalishawakuta kule Moshi.
 
Kada maarufu wa CCM na Askofu wa kanisa la Arise and Shine, Dr Boniface Mwamposa (Buldozer) leo amewahimiza waumini wake waende wakajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura na kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nabii huyo amesema hayo leo jioni wakati akiwahubiria mamia ya waumini wake waliofurika kwenye kiwanja alipokuwa akihubiri na kutoa mafundisho ya Yesu. "Hata Yesu alihesabiwa, hivyo nawasihi watu wangu wote mwende mjiandikishe na kuwapigia kura wagombea wa CCM". Amesema.

Askofu Mwamposa alitumia takribani saa nzima kabla ya kuanza mahubiri kuwahimiza, kuwasihi na kuwashawishi wafuasi wake wafanye kama alivyowaagiza na Mungu atawabariki.

MAONI YANGU
Huyu askofu sasa naona mahubiri yanakaribia kumshinda. Hakuwa na haja ya kuwahimiza wafuasi wake kuwapigia kura CCM kwa sababu waumini wake wote sio wanaCCM.

Asitake kutumia fimbo ya upako na miujiza kulazimisha mambo kwa matakwa yake binafsi. Angeishia tu kuwahimiza wakajiandikishe kuliko kwenda mbali zaidi kuwaelekeza aina ya wagombea watakaowapigia kura.

Hii ni sawa na kuwageuza binadamu wenzake kuwa misukule yake. Haifai, haipendezi na Mungu hapendi.

Hapo ile misukule ya kwetu utaiambia nini?
 
Tanzania ni nchi ambayo mtu unaweza kuja mikono mitupu ukaondoka na mamilioni ya hela. Haiingii akilini kuona yule tapeli amewaibia pesa wananchi kwa miaka chungu nzima wakati serikali inayopaswa kuwalinda dhidi ya matapeli ipo kimya. Inauma sana.

Hivi kweli kanisa kama la Mwamposa linalouza maelfu ya katoni za maji kwa bei kubwa linasamehewa Kodi lakini mtu anayeuza maji katoni moja mkononi anadaiwa ushuru.??
Hapa ni kweli kabisa CCM wanatuona nyani kabisa .
CCM wanafikiri wale watu elfu tano au sita pale Kawe wanaweza kuipigia kura ikashinda mamilioni ya waumini wasiokubaliana na dhulma na mauaji !!
 
Hivi embu tauambie ile michango cdm ilikuwa inakusanya kwenye mikutano imetumikaje ?

Mimi nazungumzia huyo Nabii wenu. Hayo ya michango au Chadema waulize wenyewe. Nabii wenu ni muhuni, Mwizi na tapeli. Period.
 
hatari iliyopo, kama leo anaweza kuwaelekeza anaowaita "watu wangu" kupigia ccm, kesho anaweza kuwaelekeza kupigia mtu wake toka kwenye dini yake, na siku ingine toka kwenye kabila lake. ameongea ujinga mkubwa sana.
Shida yetu ni kuamini kuwa baadhi ya watu wako smart kihivyo...
 
sasa kama hawapati msaada wanafata nini ikiwa hakuna anaelazimishwa kwenda kwa Mwamposa? hapa ndio pa kutafakari badala ya kusema kuna ulaghai , mimi nina amini bila shaka wanapata wanachokitaka ndio maana kila siku wanakwenda
Mkuu kwanini unapenda kushabikia uovu?
 
Kada maarufu wa CCM na Askofu wa kanisa la Arise and Shine, Dr Boniface Mwamposa (Buldozer) leo amewahimiza waumini wake waende wakajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura na kuwapigia kura wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nabii huyo amesema hayo leo jioni wakati akiwahubiria mamia ya waumini wake waliofurika kwenye kiwanja alipokuwa akihubiri na kutoa mafundisho ya Yesu. "Hata Yesu alihesabiwa, hivyo nawasihi watu wangu wote mwende mjiandikishe na kuwapigia kura wagombea wa CCM". Amesema.

Askofu Mwamposa alitumia takribani saa nzima kabla ya kuanza mahubiri kuwahimiza, kuwasihi na kuwashawishi wafuasi wake wafanye kama alivyowaagiza na Mungu atawabariki.

MAONI YANGU
Huyu askofu sasa naona mahubiri yanakaribia kumshinda. Hakuwa na haja ya kuwahimiza wafuasi wake kuwapigia kura CCM kwa sababu waumini wake wote sio wanaCCM.

Asitake kutumia fimbo ya upako na miujiza kulazimisha mambo kwa matakwa yake binafsi. Angeishia tu kuwahimiza wakajiandikishe kuliko kwenda mbali zaidi kuwaelekeza aina ya wagombea watakaowapigia kura.

Hii ni sawa na kuwageuza binadamu wenzake kuwa misukule yake. Haifai, haipendezi na Mungu hapendi.
Zawadi Ngoda na hapa unasemaje ?
 
Zawadi Ngoda na hapa unasemaje ?
Hii mimi naikubali sana. Nitafungua UZI maalum kuhusu Dini na Siasa. Hii itakuwa topic nyingine.

Ni hivi, ninachowataka CHADEMA wasibague wapiga kura. Wanyooshe mikono yao miwili kwa taasisi zote, wasiegemee taasisi moja tu. Kwa sababu hata wakichaguliwa kama wabunge, madiwani, viongozi wa serikali za mitaa au Urais bado watakutana na wananchi katika taasisi zote hizo. Sasa watawahudumiaje? Hii ndio nia yangu ya kufungua UZI huu.
 
Mkuu Mwamposa kuwahimiza watu wake wawapigie kura CCM ina uhusiano gani na CHADEMA?
 
MWAMPOSA ANAWAKOSESHA USINGIZ, ANAWANYIMA RAHA, ANAWAKERA WAPUMBAV NDIO MAANA KILASIKU MNAMJADILI MWANAUME KIDUME WENU...
 
Waumini Wana akili timamu, Si vyema kuwapangia chama Gani wakipigie kura.

Ilitosha kuwahamasisha kushiriki ktk zoezi la uchaguzi.

Kwako Askofu Mwanamapingduzi!!
 
Back
Top Bottom