eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Huyu ni mchonganishi sana. soon atatokea shehe naye ataelekeza watu wapigie cuf. atakuja mchungaji ambaye hamkubali mwamposa atataka aongee kumkosoa na kuelekeza watu wampigie fulani, analeta fujo tu, shida ni shule na exposure. ukipata pesa za kitapeli wakati hukutarajia unajiona kama mkuuubwa. yaani yeye ndiye wa kuamulia watanzania hatima zao? hadi wasomi kabisa wanapokea maelekezo toka kwa huyu mnyakyusa tapeli wa dini?
wapentekoste najua wote wanapinga mafundisho ya mwamposa, wakatoliki wanapinga mafundisho yake, walutheran kadhalika. vipi hao nao wakijiunga wakatoa misimamo na maelekezo? yaani yeye kukusanya vile watu anaamini amekusanya watanzania wote? na vipi dini ya kiislam nao wakianza hivyo kuelekeza watu wapigie kuwa yule wanayemtaka? huyu anawaharibia though yeye anafikiri anawasaidia ccm.
Huyu jamaa kalewa. Ni ulevi wa umashuhuri. Anavyokusanya watu vile anahisi yeye yuko juu ya kitu chochote Tanzania 🇹🇿.