Mwana FA: Kuendesha timu Kabla ya kukamilisha taratibu za kisheria za uwekezaji chanzo cha Mgogoro Simba

OMOYOGWANE haya njoo hapa unakumbuka nilichokua nakuambia jana kwenye uzi wako?
 
So far yanga wapo katika njia sahihi.
 
Iyo haikua sharti la serikali bali ni taratibu za uwekezaji ndizo zinataka ivyo yaani hata ingekua yanga, azam, singada n.k nao pia wangetakiwa kufanya ivyo
 
Mo anataka kufanya uhuni.

Huyu mtu aliwahi kuwa Simba akatoka akaenda kuanzisha katimu kake ka African Lyon.

Akaachana nako.

Akarudi Simba kutufanyia utapeli wake.

Hata kama ana hela ila hiyo sio tiketi ya kufanya uhuni wake.
 
Mwana FA anamjua anayekwamisha huo mchakato kukamilika?

Kuna wale viumbe wanaitwa UCC kama sijakosea hao ndio chanzo cha yote, wamekuwa wakiweka vikwazo kila mara Mo anapotaka kukamilisha mchakato.

Kwa hili Mo asilaumiwe.
Hakuna kikwazo wanasimamia taratibu zifuatwe. Prospectus ya mabadiliko imeletwa badala ya kuipitia wakatoa mrejesho kwamba upande wa zile hisa 49% za mwekezaji wanatakiwa kuwa shareholders angalao watatu(kumbuka ilo sio sharti lao binafsi bali ni utaratibu ndio upo ivyo yaani hata ingekua azam, yanga, ihefu n.k walitakiwa kufanya ivyo) kutokea hapo simba hawakurudi tena kusubmit katiba ilifanyiwa marekebisho sehemu ambayo wameelekezwa sasa nani anaekwamisha mchakato hapo
 
Nafikiri mwana fa yupo sahihi. Serikali kupitia vyombo vyake tayari ishasema maeneo ambayo katiba ya mabadiliko inatakiwa kufanyiwa marekebisho sasa hapo ni jukumu la wanachama na mwekezaji kufanya marekebisho then waipeleke tena katiba ili isajiriwe. Unachotaka kusema wewe sasa serikali iingilie maamuzi ya taasisi.
 
Hilo la kuwepo shareholders watatu limeainishwa kwa sheria ipi?

Kwasababu nakumbuka hata lile la 49% ni kama serikali walilipachika ghafla ili kumuondolea Mo absolute power, jambo ambalo halikuwa baya wanachama wabaki na nguvu.

Kama sio sheria imeainisha hayo kufanyika basi ndio maana Mo amekuwa mzito kukubaliana na hilo jambo, kwasababu wanachofanya hao jamaa wa FCC ni kama wanamkomoa kwa kupachika vipengele visivyo na manufaa kwake.

Inakuwaje mtu awe tayari ameshawekeza sehemu ya pesa zake kwenye klabu halafu ghafla wamwambie wanatakiwa wawe watatu, hicho alichokwishatoa atarudishiwa na nani?!
 
Hapo ndio namshangaa Kadugida na wale wanaolaumu washabiki na kuwaita mbumbumbu, mashabiki zaidi ya kununua jezi na kuingia uwanjani Hana nguvu yoyote ya kisheria kuingilia mchakato.
Wanachama na viongozi wa Simba upande wa wanachama wanawajibika kwa hili.
Watu eanaoonekana wanampinga mo sio kwamba hawataki awekeze Bali ni taratibu zilizotumika kuingia mfumo wa uwekezaji.
Kama kungekuwa na wawekezaji wasiopungua watatu Leo hii hakuna mtu ambaye angemlaumu mo Bali Bodi ya Simba .
 
Hilo la kuwepo shareholders watatu limeainishwa kwa sheria ipi?
Kanuni zinataka ivyo mkuu
Kwasababu nakumbuka hata lile la 49% ni kama serikali walilipachika ghafla ili kumuondolea Mo absolute power, jambo ambalo halikuwa baya wanachama wabaki na nguvu.
Ni Mo mwenyewe ndie alikuja na ilo pendekezo la 51%/49%
Inakuwaje mtu awe tayari ameshawekeza sehemu ya pesa zake kwenye klabu halafu ghafla wamwambie wanatakiwa wawe watatu, hicho alichokwishatoa atarudishiwa na nani?!
Kigezo cha kuwepo shareholders watatu ni takwa la kisheria na Mo alitaarifa tangu mwanzo alivyo-submit katiba ya mabadiliko nakumbuka hata bakhresa alikua tayari kununua sehemu ya hisa kati izo 49%. Kama Mo alitoa pesa wakati mchakato wa mabadiliko haujakamilika hayo sasa ni makosa ya Mo mwenyewe, kwanini uwekeze pesa zako kwenye mali ambayo bado haujakamilisha taratibu za kuimiliki?
 
Hili limewekwa baada ya Simba kutaka mchakato wa uwekezaji, mwanzoni mo alitaka kununua asilimia 51 lakini baada ya malalamiko serikali wakati huo Mwakyembe akiwa waziri wa michezo ilitunga Sheria timu za wananchi Kama Simba na yanga ziuze hisa asilimia 49 na wawekezaji wasipungue 3
 
Ninavyowajua Simba itatafutwa mechi moja ya kirafiki na either Jamhuri ya Pemba au Manyema ya Congo DRC Simba watashinda migogoro yote itazimika au Azizi Ki anaweza akatumwa akamtembelee MO au Mangungu ofisini apige picha itumee mitandaoni, hapo kelele zote zitayeyuka.
Simba wala hawana makuu
 
Mo alitoa rushwa kwa kifupi aliuteka m hakato kwa kuanza kutoa pesa kabla hii ilinyima fursa wawekezaji wrngine
 
MO hawawezi akakubali kugawana share na mtu mwingine. Yeye anataka share zitakazomuwezeshavkusema “Simba ni club yangu, nimeinunua”
 
Mo alitoa rushwa kwa kifupi aliuteka m hakato kwa kuanza kutoa pesa kabla hii ilinyima fursa wawekezaji wrngine
Watu wengi hawana uelewa wa masuala ya finance katika hili sakata wanafikiri sheria na kanuni za uwekezaji zimepachikwa kumkomoa Mo kumbe izo ni kanuni ambazo zinatumika kwa kila mtu.
 
Niliwaambia hapa kuna mgogoro Simba wakaja wapumbavu kunitukana na kunidhihaki. Au ni mpaka hivi Naibu Waziri aseme mwenyewe ndio ionekane kweli?
MUBENDE
 
kwanini serikali walikuwepo wakati MO anatoa hundi ya 20B ikiwa mchakato ulikuwa bado?
 
Hata katika izo 49% akichukua 30% akawaachia wawekezaji wwngine wagawane izo 19% bado atakua main shareholder.
MO hata ku share hizo 49 na wengine, kwa kifupi anataka iwe upande mmoja wanachama, halafu upande mwingine ni yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…