Mwana FA: Kuendesha timu Kabla ya kukamilisha taratibu za kisheria za uwekezaji chanzo cha Mgogoro Simba

Serikali itoe tamko kwamba kinachoendelea kufanyika Simba siyo sahihi na iamuru utaratibu ufuatwe na ikiwezekana mchakato uanze upya chini ya katiba inayotambuliwa na serikali pamoja na TFF,haiwezekani serikali itoe maelekezo halafu muda unaenda bila maelekezo yake kufanyiwa kazi halafu yenyewe nayo iseme inasubiri tu! Hadi lini? Na tayari mvurugano ushaanza kutokea kwahiyo ni wakati sasa serikali ichukue jukumu lake kama baba mlezi wa kila kitu hapa nchini.
 
Kama kweli Sheria inataka hivi basi nimeshaelewa chanzo cha matatizo yote. Mo hataki kushirikiana na watu kuimiliki Simba kwa 49%. Tena alitamani hata aimiliki peke yake kwa 100% kama sheria ingekua inaruhusu. Kwakifupi Kanjibhai anapolalamika kua anakwamishwa basi itakua hao watu ambao wanakazia hiyo sheria ya wamiliki watatu na zaidi kwa hizo 49% na wala si vinginevyo. Just imagine kwa nature ya Mo tunavyomfahamu anapenda kuabudiwa unadhani wakiwa watatu au zaidi hiyo publicity ataipata wapi?! Lakini pia anaamini nguvu na sauti yake itapungua. Vipi kuhusu pesa zake ambazo tayari ameshatumia yeye anaona zitakua zimeenda tu bure. Sina uhakika kama hiyo sheria ya wamiliki watatu ama zaidi ipo kweli, lakini kama ni hivyo basi tusubiri kuna moto mkubwa zaidi ya huu unakuja
 
Hivi ndugu zangu nisaidieni hili...simba ni mbovu sana kama inavyoelezwa au ni sababu yanga na Azam wapo vizuri zaidi yao??....hii ishu ya uongozi kibongo bongo naona kama ipo common hivi ...nyuma kidogo Yanga ilivyokua vibaya pia kina mwakalebela walikua wanaonekana wabaya ...azam hivyo hivyo kina popat hawajawahi kuonekaana wema sanasana they are blamed to support simba and Yanga ...isije ikawa Tatzo ni sisi mashabiki wenyewe tunaopenda mafanikio ya haraka kila sekta pasipo kutaka kufanya kazi kwa bidii which hata ndo inayoiathiri taifa stars pia.
 
Ukiangalia pia kuna watu mpaka leo hawaoni impact ya karia kwenye soka letu ...which is hapo ndo napata shida kuamini hii sababu inayosababishwa na mashabiki, wanachama wa simba kwamba shida ni viongozi wajiuzulu, je wakijiuzulu au Mo akaondoka je wapya wataleta nini ikiwa kuna vitu vya msingi hatujafanya. Leo hii Yanga wanaperfom vizuri ila ni hawa hawa watu endapo Yanga ikaanza kuperform vibaya bas Hersi na Gsm watatakiwa waache timu.. Je tutafika kwa staili hii??
 
Serikali ni mambo mengi muhimu ya kufatilia. Wanachama na mmiliki wamalize tofauti zao warekebishe vipengere husika kwenye katiba ya mabadiliko then mchakato upitishwe na mamlaka husika
 
Ukiangalia hapa kwa undani sana kuna chembe chembe za usiasa zinaathiri hizi Tim pengine wawekezaji na viongozi nao ni waathirika wa hii siasa...na iam sure kinachoiharibu taifa stars ndo kinachoaaffect hizi simba na Yanga...this two teams are more than we think na ndio mana usishangae hata zinaingizwa kwenye vitu nyeti serikalini kama bajeti ...its like there are remoted kwamba aya sasa hiki kipind ni cha Tim flan then mda ukiisha itafta nyengine ...akili yangu fupi inaniambia hili ni tatzo na incase its stopped then probably hatutayaona haya.
 
Inashangaza kuona VAR Tanzania haijawa proposed kwenye bajeti ya wizara ya michezo ila bajeti kuu ndo imetoa official statement .
 
Serikali ni mambo mengi muhimu ya kufatilia. Wanachama na mmiliki wamalize tofauti zao warekebishe vipengere husika kwenye katiba ya mabadiliko then mchakato upitishwe na mamlaka husika
Ukizungumzia mmiliki pale wamiliki ni wanachama MO na wanahisa wenzake watatambulika kama wamiliki wenza pale mchakato utakapokamilika na wao kulipia hizo 49%.
Unajua MO anachukulia poa anafikiri tayari amaeshamaliza mchezo lakini hajui kama siku zote sheria ndiyo msema kweli ipo siku atajuta na kulia kilio cha mbwa kwa sababu naamini kuna watu ndani ya Simba wanamlia hela zake na kumdanganya mambo yote safi na wala asiwe na wasiwasi kumbe uongo tu.
 
Nashukuru.
 
Furaha Bila ukweli huwezi kuipata Manala hupenda kusema Simba wanapenda kuendesha mambo Kwa ,(chupri chupri),yaani kiujanja ujanja
Yaani tatizo lipo lakini wanajifanya hawalioni.
 
Soma vizuri uelewe. Kabla ya Mo hajaingia kuwekeza Simba hapakua na muongozo wowote kutoka FCC na BMT iliyotoa mwanga kuhusu mchakato huo. Mo na Simba wakawa wanaendelea na zoezi la kutaka kumpa Mo timu kama mwekezaji, ilifikia hatua hadi Mo alikuwa anataka hati ya jengo la Simba huku Kilomoni na wafuasi wake wakigomea, serikali ilikuwa hadi hatua hiyo inafikia, serikali ilikuwa kimya hadi inafikia hatua ya Mo anajithaminishia uwekezaji wake kwa Simba ataweka kiasi gani. Kuna hatua ikafikia kwa Mo na Simba ndipo serikali ikaamka kupitia FCC na BMT na kuweka muongozo kwa Simba kurekebisha mchakato wao
 
Sheria zinatungwa na kurekebishwa kila siku kulingana na mahitaji ya wakati husika. Iyo sheria hajatungiwa Mo ni sheria ambayo itakua applicable kwa yoyote. Mo afate utaratibu apewe timu
 
Sheria zinatungwa na kurekebishwa kila siku kulingana na mahitaji ya wakati husika. Iyo sheria hajatungiwa Mo ni sheria ambayo itakua applicable kwa yoyote. Mo afate utaratibu apewe timu
Kuna sehemu nimeandika kuwa katungiwa Mo? Kuna sehemu niliyohoji kuwa kwanini imetungwa? Kuna sehemu niliyosema kuwa isifuatwe? Point yangu ilikuwa kuonesha kuwa kipi kilianza kati ya mchakato wa Simba vs sheria za serikali jambo ambalo ulikuwa hulijui na ndio maana kwenye post yako namba 24 ukaihusisha hadi Azam kuwa inatakiwa nao wafuate hizo sheria.
 
Mwana FA anamjua anayekwamisha huo mchakato kukamilika?

Kuna wale viumbe wanaitwa UCC kama sijakosea hao ndio chanzo cha yote, wamekuwa wakiweka vikwazo kila mara Mo anapotaka kukamilisha mchakato.

Kwa hili Mo asilaumiwe.
Unaambiwa hivi huyo Mo wako hatakiwa kuwa peke yake kwenye 49%, na yeye ndio anadai katoa b20, sasa kwa hali hii kwanini tusihisi kwamba Mo nae ni tatizo ili aweze kuendelea kuwabebesha vindoo akina Saidoo??
 
Uko sahihi 💯
 
Unaambiwa hivi huyo Mo wako hatakiwa kuwa peke yake kwenye 49%, na yeye ndio anadai katoa b20, sasa kwa hali hii kwanini tusihisi kwamba Mo nae ni tatizo ili aweze kuendelea kuwabebesha vindoo akina Saidoo??
Nakubaliana na wewe Mo ni tatizo Ila watu wanaogopa kusema sababu ya kuhofia atasusa.
 
Sasa huyo mwana Fa km alijua yote hayo mbona hakusema hapo kabla, na kwann hakushauri kuwa mchakato ukamilike afu ndo mengine yaendelee?

Tukio la Yanga yeye anaisemea Simba, inahusuuu? Hata km aliongea akiwa Naibu waziri bado hakukua na haja. Aache unafiki huyu rafiki wa tajiri mtata.

Mxxxxiiiiiieeeew.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…