Mwana FA: Kuendesha timu Kabla ya kukamilisha taratibu za kisheria za uwekezaji chanzo cha Mgogoro Simba

Yeye ni Naibu Waziri kanena kama serikali. Na kasema Wazi wao kama serikali walinyamaza ili kupisha viongozi na wanachama kumaliza Mambo Yao wenyewe lakini si kama hawaoni. Akaongeza kama Hali itaendelea wataingilia Kati kama regulator. Unafiki wake uko wapi?
 
Namuunga mkono.
 
Hii serikali inachochea fujo tayari wanajua tatizo lipo wapi Ila wamekata kimya
 
Yanga walikuwa wawazi wawekezaji wanakuja hawatagusa Mali za yanga Ila mo hata hdjakamilisha uwekezaji alitaka hati ya jengo la Msimbazi,, uwanja wa Bunju anataka uitwe jina lake.
 
Em soma vizuri nilicho kiandika, kwakua wee ni uto huwezi elewa.
 
Watu wanazunguka Sana, tatizo la Simba ni mo, kabla ya kuja Simba mo alimiliki timu mbili na zote zikamshinda. African Lyon na mto Singida.
Mo alipotaka kuingia Simba alikuja na thamani yake apewe kwa bilioni 20, awe na hisa 51 lakini baada ya malumbano serikali. Ikaingilia Kati na kutunga kanuni kuwa vilabu vya wanachama Kama Simba na yanga vinatakiwa kuwa na wawekezaji wasiopungua watatu na wapewe hisa zisizozidi 49.
Mo bado alitumia ushawishi wake hizo hisa 49 awe mmiliki pekee na alianza kutoa pesa kabla mchakato haujaanza ili mradi yeye mwenyewe apitishwe. Lakini imebainika hata hizo bilioni 20 hajatoa badala yake anataka kugeuza misaada aliyotoa ndio iwe hisa zake.
Nia ya Simba kutafuta mwekezaji ilikuwa kufanya klabu ijitegemee na kuwa klabu kubwa zaidi Afrika . Swali la kujiuliza tangia mo ajishigulishe na Simba Nini kimeongezeka kwani rasilimali Kama jengo la msimbazi na uwanja wa Bunju alivikuta.

Alipinga mkataba wa Simba na Azam ambao wangeingia kwa miaka 10 na Simba kupata bilioni 40 kuwa hauendani na thamani ya Simba wakati yeye ametaka apewe asilimia 49 kwa pesa ambayo ni nusu ya thamani ya mkataba.
Amewazuia Simba kuingia mkataba na NIC ili atangaze kampuni zake ambazo zinatoa pesa kiduchu.
Simba wakubali walifanya makosa wake chini na kuanza upya.
 
Ikumbukwe kwa kanuni za FIFA serekali haipaswi kuingilia maswala ya ndani kuanzia TFF na Vilabu vyake, Serekali inasimamia sheria na kutoa ushauri tu.
 
Ikumbukwe kwa kanuni za FIFA serekali haipaswi kuingilia maswala ya ndani kuanzia TFF na Vilabu vyake, Serekali inasimamia sheria na kutoa ushauri tu.
Simba Sports Club ni zaidi ya mpira wa miguu ambao unasimamiwa na FIFA. Ni club ya michezo mingi. FIFA wanadeal na sehemu ya mpira wa miguu tu. Sasa serikali lazima ihakikishe hii club inayotaka kuwa kampuni kuwa inafuata taratibu.
 
Simba Sports Club ni zaidi ya mpira wa miguu ambao unasimamiwa na FIFA. Ni club ya michezo mingi. FIFA wanadeal na sehemu ya mpira wa miguu tu. Sasa serikali lazima ihakikishe hii club inayotaka kuwa kampuni kuwa inafuata taratibu.
Kuna Mambo serikali haiingilii Ila mengine wanaingilia ndio maana fbi waliweza kuingilia na kumtoa Blater.
Kama serikali ndio ilitunga kanuni kwanini ishindwe kusimamia.
 
Mtindo ni uleule ukikosa hoja unamwamishia Mtu upande wa pili. Ignored.
Nimekuambia soma vizuri andiko langu, sasa huo msuso unahusu nn hapa? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ikumbukwe kwa kanuni za FIFA serekali haipaswi kuingilia maswala ya ndani kuanzia TFF na Vilabu vyake, Serekali inasimamia sheria na kutoa ushauri tu.
Serikali hairuhusiwi kuingilia sheria na kanuni za uendeshaji soka lakini suala usajili na usimamizi wa vyama na vilabu na kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa ni jukumu la serikali, hakuna chama cha soka wala klabu isiyo sajiliwa na mamlaka ya nchi husika ikaruhusiwa kufanya kazi katika nchi hiyo.
 
Issue iliyobaki kwenye mchakoto wa simba inapaswa kumalizwa na wanasimba wenyewe ndani, kwa mujibu wa katiba yao.
 
Wewe na mjumbe wa Bodi wa Simba upande wa wanachama Tena ana cpa nani anajua zaidi
mbona mjumbe yuko wazi pesa ipo imewekwa equity na simba wanapata gawio lao la 200M kila mwezi, Haya ni maneno ya mwenyekiti wa Simba Mangungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…