Mwana FA: Waziri Pekee kwenye Baraza la mawaziri asiye na Degree

Kina pdf ama
 
Ulikuwa ukisoma advance diploma, unakwenda kufanya shahada ya pili moja kwa moja
Mpaka kesho advanced diploma ni equivalent ya bachelor degree na unaruhusiwa kufanya masters,ndiyo maana watu walipata mikopo ya 'elimu ya juu' pale CBE,ifm,tia, IAA nk
 
Ko ukiwa na advanced diplom ndo usome masters nyie acheni kutuchora sema ndoiv jamaa kajitahid kuunga mpk kafik ila iyo masters yake ndo inaleta utata maybe ipo ivo tusibishe sana
Advance diploma ni equivalent ya bachelor degree na unaruhusiwa kufanya masters ndiyo maana pale CBE ifm tia IAA nk watu walipata mikopo ya 'elimu ya juu',jifunzeni taratibu za elimu,tatizo lenu Hadi kuomba kusoma chuo mlisaidiwa pale machinga complex kwa ada ya 30k
 
Inawezekana kusoma Masters bila ya undergraduate degree kama umesoma na kufaulu Diploma. Wanaangalia education points kama halitosis basi unasoma Postgraduate Diploma kwa mwaka mmoja ukifaulu unaruhusiwa kusoma Masters degree nafikiri ndivyo alivyosoma, sio lazima kusoma Bachelor degree.
 
Nadhani wewe ndiye mwenye matatizo ya ulewa kwani inaelekea hujui hata maana ya digrii ni nini.
 
Mwana Fa na yeye, hataki kupata hata hizi degree za bwerere za kina msukuma wakau utudanganyie.
 
Ukitaka fupisha mlolongo wa kukaa darasani inakuwa hivi
Certificate ->Diploma ->Advance Diploma-> Masters Degree.
Kwake naona Advance Diploma ina miss ila inawezekana Mfumo unaruhusu kama vile kuwa na Associate Degree halafu kufanya mastres .
 
Sasa makasiriko ya ada ya machinga complex inahusian na nini ko wew unajiona una utajir kukashifu sis masikini sio wew elewesha mtu habar za hayo ya ada haihusiani hapa
 
wewe ndio unajua mkuu toa Elimu na ujibu je mwana FA Ana degree au hana?
Kwani masters siyo degree?


Tambua kuwa elimu ya chuo kikuu imegewanyika katika ngazi mbili (a) Undergraduate level, ambayo hutoa credentials kama Bachelors Degree, Advanced Diploma, Higher National Diploma, n.k., (b) Graduate (au Postgraduate) level, ambayo hutoa credentials kama Masters Degree, Professional Degree na Doctorate Degree)

Qualification za kujiunga na graduate level ni kumaliza undegrarduate level. Sasa iwapo mwana FA ana Advanced Diploma, hujui kuwa amemaliza undergraduate level ndipo akaanza postgraduate level ambyo ndiyo iliyomoatia Masters degree?.

Je unajua kuwa kuna vyuo ambavyo huungansiaha undergrdaute na Masters katika leve moja na kutoa digrii ya masters moja kwa moja? Huelewi pia kuwa Nyerere alikwenda Edindbuegh kupata masters akiwa na diploma ya ulaimu ?
 
kwa hiyo bachelor Degree MWANA FA anayo au hana?
 
kwa hiyo bachelor Degree MWANA FA anayo au hana?
Hana Bachelors degree, ila ana Masters degree; swali lililopo hapa ni hilo

"Mwana FA: Waziri Pekee kwenye Baraza la mawaziri asiye na Degree"​

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…