Nimepitia comments zote nikarudi hapa.
Kwanza pole sana.
Pili dogo anasema hajakutaja wewe kwenye utapeli. Ila tuachane nayo.
Unajua dear wewe ambacho pengine kinaweza kikawa ni adui yako na haujakigundua ni 'kuongea too much", na ku promise vitu public sana. Jitahidi kupunguza. Ongea kidogo tena sana wala hautaona haya maneno yanakufuata.
Unajua tatizo la mtu anayeongea au kama sio kuandika sana? Huwa hapati muda wa kutafakari anachotaka kuandika na kujua baadae kitakuwa na madhara gani kwa mtu. Unakumbuka ile issue ya yule dogo?, unamwona tena jf?. Ni matokeo yako ya kuandika sana ukiona unamsaidia mtu kumbe unamchafulia sifa yake. Tuachane nayo.
Yawezekana huyu dogo ulimpromise sana, ukampa matumaini ya juu. (Niliona ule uzi ulikuwa unapromise haswa na kusema umewasaidia wengi, hata kwenye huu Uzi nimeona unasema yaani unasaidiaga hadi hubby ako anakumind). Sasa kwa maneno kama yale pengine dogo aliweka matumaini makubwa kwako, na watu waliokuwa kwenye zile nyuzi wengi tuliamini hautamwacha dogo hivi hivi. Sasa kama alikuwa na matumaini yote hayo na mwisho wa siku hakuambulia hata 10,000 unafikiria nini? Lazima ajione unajimwambafy public tuu.
Kuepuka maneno, epuka kuandika sana bila kujua madhara ya unachokiandika baadae. Epuka pia kutoa promise hadharani kwamba utamsaidia mtu kabla haujamsaidia. Hauwezi kujua ni wangapi waliacha kusaidia wakijua "pedeshee" Manengelo atasaidia.
Huu ni ushauri wangu wala hauna chuki yoyote.
Sent using
Jamii Forums mobile app