Pre GE2025 Mwana JF, Be The First to Know CCM Ndie The Overall Winner wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 Kufuatia Ushindi Serikali za Mitaa。CCM Amekomba Almost Everything!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wana JF,

Maadam JF ni ukumbi wetu, na sisi humu JF, tuko members wengi, na tumefanya mengi, hivyo mimi member mwenzenu Pascal Mayalla, naomba niwe wa kwanza, kuwajulisha wana JF wenzangu, ili kuwapa ile JF advantage ya wewe kama Mwana JF, be the first to know kuwa CCM ndio mshindi wa jumla wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 kufuatia ushindi wa kishindo wa uchaguzi huu wa Serikali za mitaa kwa a landslide victory ya ushindi wa kishindo, kwa kwa kukomba almost everything,kila mtaa,kila kata,kila kitongoji na kila kijiji, hivyo mshindi wa serikali ya mtaa mwaka huu, ndie mshindi wa uchaguzi mkuu wa 2025!。

Ushindi huu ni kufuatia mimi mwana JF mwenzenu, Pasco Mayalla, nimesikia sauti ndani ya moyo wangu, yaani ile "voices from within", kuwa katika uchaguzi huu, wa serikali za mitaa, mshindi wa jumla ni CCM!, ndie anayekwenda kushinda uchaguzi wa 2025!。

Hii voices from within yangu is never wrong, maana ni sauti yake YEYE mwenyewe!,aliye ndani yangu!。

Lengo la uzi huu sio kutangaza ushindi wa CCM uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu 2024, bali kuutangaza kinachokwenda kutokea uchaguzi Mkuu wa 2025!, kwasababu kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa tulishauri Mnaonaje Uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu na Usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi? Samia Atabarikiwa Sana! haya sasa ni matokeo!

Kufuatia wengi hawana muda kusoma makitu marefu,wale wa short and clear mnaweza kuishia hapa na ku jump kwenye conclusion
Mjue Pasco
Mambo ambayo Pasco ni wa kwanza humu jf
leo ninapowaeleza humu mshindi wa jumla wa uchaguzi huu wa serikali za mitaa ni CCM,na mshindi wa uchaguzi Mkuu wa 2025 ni CCM, naombeni tuu mniamini, na kwa msio amini, endeleeni kusubiria matokeo rasmi ndipo mtaamini.

Hii predictability ya mshindi wa uchaguzi kabla hujafanyika,inamaana chaguzi zetu ni very predictable,uchaguzi haujafanyika,huku watu wanajua matokeo,hii inaweza kumaanisha sio kuwa tunafanya uchaguzi,bali ni tunafanya igizo tuu la uchaguzi!。
Maoni yangu Kuhusu uchaguzi huu wa serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa 2025
Conclusion
Tanzania sio nchi ya watu fulani tuu au chama fulani tuu, Tanzania ni nchi ya Watanzania wote, wa vyama vyote, dini zote, makabila yote, jamii zote, jinsia zote, rangi zote, hali zote za maisha, matajiri na masikini na Watanzania wa circumstances zote.

Nimesikia sauti, "voices from within" ikiniambia kuwa tukiendelea kufanya chaguzi zetu kwa Mutatis Mutandis, hizi, kuna jambo fulani litatokea tena kama lilivyotokea baada ya mutatis mutandis ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020.
Sijui ni wangapi humu wanaojua, kile kilichotokea ile 2021, kilichangiwa na matokeo ya uchaguzi wa 2019 na uchaguzi wa 2020, tusiporekebisha makosa, kinaweza kujirudia!.

Hivyo uchukulie uzi huu kama uzi wa an info pack ya mshindi wa uchaguzi mkuu wa 2025 ni CCM, Wapinzani labda 2030 Uchaguzi mkuu wa mwaka 2030, ndio mwanzo wa mwisho wa CCM! Wajinga karibu wote watakuwa wamemalizika!

Hongera sana CCM kwa ushindi wa kishindo baada ya Watanzania kutekeleza kwa vitendo wito huu Ukipokea Ujumbe Huu wa Rais Samia Kuhusu Kesho, Usikae Nao, Sambazia na Wengine!. Kesho Kazi ni Moja Tuu!, ni Unachukua...Unaweka...!.

Hata baada ya uchaguzi huu wa serikali za mitaa, fursa to make it right kwa uchaguzi wa 2025 bado ipo!.
Rais Samia ni fursa ya kutenda haki 2025, Ombi kwa Rais Samia: Japo wengi wape, wachache pia wasikilizwe, Hoja ya kufanya minimum reforms za Katiba ni hoja ya msingi sana kuliko hata Sheria! Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
 
Mtu utunge mtihani mwenyewe, usimamie mwenyewe, unyime wenzio peni za kufanyia mtihani, usahihishe mwenyewe halafu ukose kupass kwa alama zote basi utakuwa mjinga wa mwisho.

Hizo sio voices from within mzee, ni sad reality ya ubaradhuli wa CCM.
 
Kama umefanya mambo yote hayo je hawa akina salumu kikeke na Wengineo walikuacha wapi.

Kuna faida kubwa ya kuwa na weledi kuliko kusifu , kuabudu siasa ambazo hazina tija. Ile reputation Kama journalist haipo.

Japokuwa umebarikiwa uwezo mzuri wa kuchambua mambo Ila bado hauna legacy katika habari.

Ungetenganisha siasa na Kazi yako ungefika mbali japo hata ulipo sio padogo.
 
Ni mbumbumbu pekee ndiye atashangilia ushindi huo. Kabla hata ya uchaguzi kufanyika CCM ilikuwa imeshashinda 65% kwa figisu za waziwazi za wasimamizi wa uchaguzi.

Mchakato mzima ni doa kubwa kwa uhai wa demokrasia yetu.
Chaguzi kama hizi zina akisi namna sisi waafrica tusivyoweza kujisimamia wenyewe kwa mambo madodo madogo kama haya.
 
P this is extreme shame kuandika mada kama hii wakati unajua wazi huu haukuwa uchaguzi bali UCHAFUZI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…