Pre GE2025 Mwana JF, Be The First to Know CCM Ndie The Overall Winner wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 Kufuatia Ushindi Serikali za Mitaa。CCM Amekomba Almost Everything!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu, mbona kama unaaga kulikoni?
 
P this is extreme shame kuandika mada kama hii wakati unajua wazi huu haukuwa uchaguzi bali UCHAFUZI
Huyu amezeeka bila kuacha legacy

My Mama anagombea kupitia ccm ujumbe na amenambia kuwa tayari kuna kura fake yeye anaziita "Mazonge"

My mama , she has 56 yrs the samePascal Mayalla.
 
Ni taarifa au habari?Vyoyote vile ushindi umepatikana usiachekuleta taarifa ya kuwa ushindi huo ni wanamna ipi?
 
Binafsi nimekufahamu humu jf, huenda kazi zako huko mtaani sio popular kama unavyojisifu kua the first wa mambo mengi.
Au labda ulibase sana chamani??

Kazi yako ingekua na matokeo chanya huku nje si ajabu kawe ungelamba kura kadhaa.

Ccm ni lazima ashinde 2025 mkuu wala sio voice from within hilo liko wazi.
 
Journalist wa kijani hamnaga akili eeeh? Yaani uchafuzi wa kisiasa unaoendelea we huuoni unakuja kuandika liuzi la hovyo kuwahi tokea. Mkuu usitulazimishe tukuignore
 
USHINDI WA KISHINDO KWA FAIDA YA NANI??!!
 
Mligwa bayanda ....Mayala khunuyu 😂😂😂😂🙌🏾🙌🏾🙌🏾.......

Sina Shaka mara nyingi huwa upo mbele ya muda (taim traveliii nyingiiiii😂)..…..
 
Nimesoma mara ya pili nimegundua hili andiko ni very SATIRICAL and IONICAL!

" CCM wamekomba everything"
 
Tunapofunga vituo vya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Taifa limeendelea kushuhudia tena ubaradhuli wa wazi na wa aibu toka kwa mamlaka zote za Serikali kushirikiana kuipatia CCM na wagombea wake ushindi wa aibu hata kwa gharama za maisha ya Watanzania.

Tunalaani mauaji na kujeruhiwa kwa wagombea, viongozi na wanachama wetu mbalimbali wakiwemo:

1) Steven Chalamila wa Jimbo la Tunduma aliyevamiwa na kukatwakatwa mapanga kikatili hadi umauti kumkuta.
2) Modestus Timbisimilwa, Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Serikali ya Mtaa wa Ulongoni A, Kata ya Gongolamboto, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam aliyeuwawa na askari kwa kupigwa risasi wakati wa purukushani za kuzuia kura bandia na batili kuingizwa kituo cha kupiga kura.
3)George Juma Mohammed wa Kitongoji cha Stand Kata ya Mkwese Jimbo la Manyoni Mkoani Singida aliyevamiwa nyumbani kwake na watu waliofahamika kuwa askari na kumpiga risasi iliyomsababishia umauti.

Aidha, tuna taarifa kadhaa za kujeruhiwa na kukamatwa na Polisi viongozi, wagombea, wanachama na wapenzi wetu maeneo mbalimbali ya nchi walipokuwa wakijitahidi kukamata na kuzuia kuingizwa vituoni kura bandia na batili zilizopigwa tayari kuwabeba wagombea wa CCM.

Tunataka watu wetu hawa waachiwe haraka na bila masharti yeyote.

Tunaendelea kuwasiliana na Chama kitatoa tamko rasmi zoezi hili likikamilika.

Tunaamini kinachofanyika kina maagizo na baraka zote za @SuluhuSamia na Serikali yake na au nchi iko kwenye "autopilot" na yeyote katika eneo lake ana mamlaka ya kunajisi uchaguzi anavyotaka kwani tayari wamepewa kinga na Kanuni ya 49 ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa inayosema, nanukuu:

"Msimamizi wa Uchaguzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Msimamizi wa Kituo, Wajumbe wa Kamati ya Rufani au mtumishi yeyote wa Umma aliyehusika na usimamizi wa uchaguzi hatowajibika kwa Jinai au Madai au kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu au za kiutawala kwa jambo lolote alilolifanya au kuacha kulifanya kwa nia njema wakati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Kanuni hizi". Mwisho wa kunukuu.

Hakika Taifa lina Msiba mwingine!!
 
Hivi mna uhakika GENTAMYCINE hajadukua akaunti hii ya kada wa Sisiemu kweli? Mbona leo amekuja na kasi ya 6G+ yenye misifa kibao hivi?

Je, unaelekea kugombea uspika mwakani, baada ya kupewa ubunge? Tutonyane basi, komredi!
 
Huu ni uchaguzi au uchafuzi? God will keep taking them to Jehanam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…