Siyo kweli, kwanza familia yangi mimi wala hawajihusishi na Siasa, na majirani na marafiki wengi ni CUF na hawaipendi CCM kabisa, lkn sijawahi kusikia wakisema hawana haki hapa Tanzania, ...
Sasa hayo matatizo yako, kwanza CUF iliiisha kufa haipo, CUF kabaki Lipumba.
Nimekueleza mimi madhila niyapatayo na dola la ccm, na niyaonayo kwa macho.
Sio kweli nini tena, nikupe matatizo yangu ndio ujue ukweli?!
Mimi ni mtumishi wa umma muda mrefu nafasi tofauti, na ni mtaaluma pia, lakini siyo mwana ccm, na sitaki kulazimushwa hilo.
Nasitaki haki niipate kwa mgongo wa ccm au influences zao, nataka haki iwe haki kweli.
Ndugu yangu anashutumiwa wao wanadai kafanya kosa wakati ushahidi hawana, unauliza matokeo ya uchunguzi hayapo, na hawana ushahidi wowote, naye no mtumishi wa umma lakini wanataka wamuweke mahabusu, kwa kudhani atatoroka, na hiyo kesi ipo tangu 2016 na hajatoroka,leo ndio atoroke, au wanatafuta kumuumiza akae mahabusu tuwape hongo kumtoa?!
Kwamba yuko nje ya mahabusu hawafurahii kila siku anatokea nyumbani kwenda mahakamani, wanataja wambinye familia yake ipate taabu, na hawana ushahidi zaidi ya hear say, na kutafuta rushwa.
Tangu 2016 hawana hata ukurasa mmoja wa taarifa ya uchunguzi, wanadai uchunguzi unaendelea, ukikamilika kesi itasikilizwa, sasa kwanini wamuweke mahabusu kama hawana taarifa yoyote ya uchunguzi, naye hajawazuia kufanya uchunguzi.
Walimsimamisha kazi miezi 8 kupisha uchunguzi hawakuleta taarifa za uchunguzi kwa miezi yote hiyo, hakimu akasema, kama haingilii ucgunguzi basi arudishwe kazini. Akarudi kazini, wale mahasimu wanalazimisha awekwe mahabusu eti atatoroka.
Kupinga hilo la mahabusu, tunaambiwa tunaichafua mahakama, mara tunaisema vibaya mahakama, sisi sio wazalendo na manemo mengi ya kijinga, kwamba sisi ni wapinzani, kwanini tusikubali kisha tukate rufaa, mahabusu ukate rufaa?!.
Sasa kwanini niiendelee kuipenda serikali ya ccm, inayolazimisha kwa assumptions za kijinga.
Na hii ni single incident.
Achana na ccm, bora ni chague tumaini la HAKI, Lisu tu.