Mwanachama Bora Jamiiforums 2022

Mwanachama Bora Jamiiforums 2022

MWANACHAMA BORA JAMIIFORUMS STORIES OF CHANGE 2022

Picha zilizopo hapo chini zinajieleza zenyewe.
Nawashukuru sana JF kwa heshima hii waliyonipa.

Huu ni mwaka wa pili mfululizo napewa heshima hii.
Leo nimefika JF na nimekabidhiwa zawadi zangu.

Huo mfuko ndimo zilimo hizo zawadi zangu.
Zawadi nimepewa kwa faragha kwa hivyo basi sitosema nilichopewa.

Naamini haiba ya mfuko inaeleza nini kilikuwa ndani.
Furaha yangu haielezeki.

Ahsante sana JF.

338016085_885456025850971_7245240510941422239_n.jpg
337533860_144563275217510_1341642119159769444_n.jpg

Tabaraka Allah .
 
Hongera sana mzee wangu endelea kuwepo humu mjengoni ninafurahia sana thread zako za historia asante sana
 
Ukitoa udini mkali, labda ungekuwa mbali zaidi.
 
Ukitoa udini mkali, labda ungekuwa mbali zaidi.
Pay...
Ikiwa huwajui wenye udini soma kitabu cha Abdul Sykes Sehemu ya Tatu: "Njama Dhidi ya Uislam."

Hii ni sehemu inaeleza waliyofanyiwa Waislam wa Tanganyika waliopigania uhuru kwa hali na mali.

Unatumia kipimo gani kuniona siko mbali?
 
JF nao sasa wameanza kupwaya, sasa huyu mzee ndio apewe uana chama bora? Si bora wangempa haya mpwanyungu village,

Nb: JF mtupe nafasi sisi wanajf tupige kura ya kuchagua mwanachama bora.
 
Pay...
Ikiwa huwajui wenye udini soma kitabu cha Abdul Sykes Sehemu ya Tatu: "Njama Dhidi ya Uislam."

Hii ni sehemu inaeleza waliyofanyiwa Waislam wa Tanganyika waliopigania uhuru kwa hali na mali.

Unatumia kipimo gani kuniona siko mbali?
Nani alikwambia ni waislamu tu walipigania uhuru wa Tanganyika? Wachaga nao tunaowabagua tena waziwazi na wao waanze kuandika na kulialia? Mlitaka zawadi labda au mli overexpect sana, au mlijua nchi itakuwa ya kidini?
 
Back
Top Bottom