Mwanachama humu amenikumbusha nilivyomfanyia jamaa mmoja aliyekuwa anajiona kafika kazini

Mwanachama humu amenikumbusha nilivyomfanyia jamaa mmoja aliyekuwa anajiona kafika kazini

Kwa Imani ya dini yangu kabla ya kulala usiku huwa tunaomba kwa kumwambia Mungu
"Na unikinge na Shari ya hasidi anapo husudu"

Mahasidi wenyewe ndo watu kama wewe kweli dua ni muhimu sana
Sana..... Unaishi wapi nije kukutembelea
 
Sa ndo mkapata faida gan? Kumbe Bongo wachawi hivii?
 
Hapana. Hautakuwa umekosea hata kidogo. Unajua tushawahi kuitwa majina mabaya kuliko hilo lako.
unaoneaje wivu mwanaume mwenzako kisa anafanya kazi kwa bidii,badala mjifunze kwann yeye anafanya kazi kwa bidii nanyi muongeze bidii mnakalia kuwaalibia maisha wenzenu,pumbaf kabisa
 
Huyu jamaa alifika kazini akawa anajiona yeye ndo yeye. Kazi anaipenda sana kuliko sisi wengine. Basi ikawa kila mfano mzuri boss anamsema yeye. Kila jambo jema mfano yeye.

Jamaa akaanza kupewa pewa safaris nyingi sana. Akawa anapewa bonus kila mara, yaani kiufupi jamaa alianza kupendeza. Akawa anapiga tie, mara suits, anachomekea na siku hizi mnaita Unyakyusa mwingi sana. Nikaliona hili nalo likafikiriwe. Nikawaita wadau kamati ya roho mbaya.

Tukakaa wenyeji, tukajadiliana kuwa huyu dogo mbona kama sisi wenyeji anakosa heshima kwetu. Kaja tunamwona hivi hivi, jamaa mmoja akasema anabonga naye. Akaenda mshtua dogo akajibu yeye si mtu wa majungu kaja kufanya kazi.

Tukarudishiwa taarifa. Basi jamaa mmoja akasema tumpatie pesa fulani atashughulika naye. Akaenda Bagamoyo tu hapo. Wala si mbali.

Yule dogo akaanza kuwa kazini mara haji, akawa anagida sana pombe, anaweza akapotea siku mbili analewa analala bar. Akawa mkorofi kinyama kazini. Mpaka boss anamsemea mbovu. Anasema kwani hii nayo kazi? Basi tu ila yeye si wa kufanya kazi sehemu kama ile.

Tukamwekezea na majungu kinyama, akaharibu ile mbaya pale job. Wakamtimua. Aiseee tulifurahi sana. Tukampongeza fundi wetu kiungo mchezeshaji. Tukabaki wenyewe tu job kwa starehe zetu.

Hizi kazi umekuja umeikuta utaiacha. Usilete kujua saaaaana.watu tumekaa Zanzibar, tumekaa Tanga... tunajua kuishi na watu. Usitake jifanya wewe ndio unafaaanya sana kazi. Mwishowe kazi nayo itakufanya. Muwe mnaheshimu wakubwa. Tunaweza kukufanya kama tulivyomfanya Mashaka Gobwe. Huyu hawezi kutusahau milele... Ishini na watu vizuri.....shauri zenu.
Tangazo la mganga
 
Haya Mambo yalishanitokea .
Baba yangu aliniambia kuwa kazini ni sehemu ya kazi Tu usilete mazoea na kazi. Ila Fanya kazi yako inavyostahiki.
Nilitembea na maneno ya mzee kichwani kwangu , HOD wangu alinielewa Sana for sure nilitengeneza Sana hela by then.
Lakini nilikutana na watu dizaini ya huyu mleta Uzi sijui hata nini kilitokea mara Boss wangu akawa ananifokea Tu bila sababu za msingi. Hatuelewani sehemu ambayo mwanzo ananielekeza friendly akawa ananichapa email kama onyo na ana cc HR office.
End of the day nilikuwa terminated Kwa kazi Kwa kisingizio kuwa I was underperformance.
Nililipwa stahiki zangu ila nilichukia kuajiriwa Sana . Ukimpiga chura teke unamuongezea hatua.

Kwa mujungu Yao Leo nilipo sio pale nilipokuwa wakati ule. Na huenda yasingenikuta Yale ningekuwa pale naendelea Tu kupewa sifa na HOD na tuzo za ufanyakazi Bora.

Roho mbaya na majungu hufanywa na watu wasiotimiza majukumu Yao sehemu za kazi.
 
Tunaomba radhi kwa wale wote watakaokwazika mwandishi ni mmoja wa wagonjwa katika hospital yetu ya crazy for life.

Ndugu Chizi Maarifa ,alifanikiwa kutoroka jana na kuiba simu ya ofisi

Tunashukuru kwa ushirikiano wenu na tunaahidi tutalishughulikia swala hili hivyo mvumilieni

Naambatanisha ushahidi wa vyeti alivyovipata kutoka hospital

View attachment 2469207
Hahahaha nimecheka sana
 
Aiseeee..... Nina toto moja la kiume lilinishikia kisu nikalishikia shoka....moto uliwaka. Midada yake mitatu inazagaa zagaa tu na vitoto vyao....
Kwa Roho mbaya, unaongoza! Inakusaidia nini?
 
Back
Top Bottom