Kwa masikitiko makubwa ninapenda kuwapa taarifa ya mdau mwenzetu humu anayeitwa
warumi amefariki usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa anapambana kwa ugonjwa wa figo.
Warumi alikuwa kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 29.
Taarifa hii nimepewa na dada yake mda huu, msiba unaelekea kwao Tegeta .
UPDATE:
Msiba upo Tegeta Nyuki, ukifika Stand unachukua boda au bajaj unawaambia wakupeleke nyumbani kwa Kiboko, maana msiba upo opposite na utaona geti jeusi liko wazi - ingia.
Msiba utasafirishwa kwenda Mbeya, Nonde Mabatini.
UPDATE.
Misa ya kumuaga itafanyika kesgo tarehe 27 August saa 8 mchana Muhimbili.
Duh..., japo mimi sio mwanachama active wa celebrity forum, ila jamaa namkubali sana na nimeguswa.
Zamani JF ilikuwa tukipoteza mwanachama, if management ilikuwa inafanya some sort of organisation, nakumbuka msiba wa Regia if tulitengeneza hadi Tshirts na tuka jiorganize hadi kuhudhuria mazishi kule Ifakara, tena kuna member alijitolea gari yake!
Hebu tazameni hapa chini
Hawa walituwakilisha vyema:
|
|
| Vijana wa Mtandao wa Jamii Forum wakiwa wamevalia rasmi waliposhiriki kuuaga mwaili wa aliyekuwa mwanachama wa mtandao huo, marehemu, Regia Mtema. |
Naomba niishie hapa, nitaendelea kesho na tutakuwa Live kutoka Ifakara (pamoja na picha)
I don't know what happened now. Should we push for equal treatment during the demise of our members, tuweke system ya ndugu kuripoti kwa jf management kifo cha mwanachama wetu yoyote regardless umaarufu wake, kisha waweke number ya mchango, wana jf kuchangie, na siku ya kuaga jf management iwepo na kukabidhi mchango kwa wakiwa na mtu wa jf atoe neno.
Na kwenye mazishi ya wana jf wa eneo husika wahudhurie kutuwakilisha.
Kwenye mchango wa rambirambi hata tukiweka minimum TZS 1,000 tuu, kwa jinsi tulivyo wengi, hiyo fedha ina kuwa ina impact kubwa na ni faraja kwa familia kujua mpendwa wao alikuwa mwanachama wa mtandao wa jf na jf wanajali.
Na kwa vile wengi wa wana jf wanatumia pen names, ili kuheshimu the unanimity ya marehemu, humu jf tuu ndio atatajwa kwa jina lake la jf, mfano huyu
warumi , lakini
pale msibani no one will mention his name, hata kwenye Salaam za jf, hatamkwi popote kwa jina, bali "marehemu alikuwa mwanachama wetu, alijinga jf lini, amechangia mada mbalimbali etc just that, na if members watakao hudhuria msiba, kwa vile kule wataliona na kulijua jina halisi, kanuni yetu na "name calling" iwe strictly observed kumuheshimu marehemu kwa kutolitaja jina lake halisi, maadam humu kwetu alikuwa
warumi , then he/she will always be
warumi.
Mkuu
Maxence Melo , if there is anything jf can do kuhusu huyu fallen hero, let's do something kuonyesha solidarity yetu.
RIP
warumi !.
P