TANZIA Mwanachama wa JamiiForums - Jikeshupa amefariki dunia

TANZIA Mwanachama wa JamiiForums - Jikeshupa amefariki dunia

Apumzike Kwa Amani [emoji120][emoji120]
 
Yani mtaani hakuna mtu anayekujua kua we ni member wa jf kwa ID hii?

Hata mimi niko hivyo hivyo

Ila kwa wewe haitanipa sana shida kujua

Nikiona ukimya kwa muda mrefu kwenye jukwaa la michezo na katika kipindi ambacho simba kafanya vizuri ntaanza kuwa na mashaka
Ni kweli kabisa ndugu yangu hakuna mtu ninaye fahamiana naye nje ya hapa ambaye likitokea lolote anaweza kuleta taarifa humu.!!

Hilo ni kweli usipo niona hapo muda mrefu ujue Kuna shida sehemu mana siwezi acha chama langu Simba bila support ata siku Moja.

Binadamu maisha yetu ni kama umeme wa Tanesco tu muda wowote unaweza kukata.😭

Kikubwa kukumbuka Ibada, kuishi vizuri na watu, kutenda yaliyo mema Kwa kadri tuwezavyo, kupendana sisi Kwa sisi na kusameheana kwakuwa hatujakamilika hivyo ni muhimu kuchukuliana madhaifu yetu n.k.
Ili siku tukiondoka duniani tuwa na angalau chembe ndogo ya hadhina ya mema Kwa Mungu Muumba pamoja na Dua za wapendwa wetu tutao waacha basi tunaweza kuvuna rehema za mwenyezi Mungu mwenye haki ikiwa itampendeza Kwa mapenzi yake mwenyewe.

Duniani tunapita kaka mbele yako nyuma yangu, Mungu wa upendo atusaidie.

One love Brother!!
 
Miaka 17 ya kutumia dawa ndugu...

Kitambo huu ugonjwa ulikuwa na stigma sana familia zilikuwa zinaficha taarifa hata dawa wengine ilikuwa mbinde kuchukua... haiyumkini kwenye makuzi yake ya awali hata hakuwa akijua shida yake, hadi hapo baadae alipojielewa na kulichukua swala la kunywa dawa kama jambo lenye muendelezo (hapo ndio msingi wa hiyo miaka 17 ya kunywa dawa)
Waliposema tangu alipozaliwa anatumia ndipo waliponichanganya, kwamba kazaliwa miaka 17 iliyopita?
 
Pole kwa Familia yake

Mimi ninatoa zawadi kwa mtu atakeye nifahamu mimi ni Nani
 
Duh watu wanajuana kabisa, mimi nikifa mtasikia kwenye vyombo vya habari, na mtaona pilika za viongozi kadhaa. Maana sina hakika ila nina imani Rais atahudhuria au kutuma mwakilishi wake
 
Multiple organ failure itakuwa imemuondoa binti mbichi kabisa huyu, prolong use of ARV ziliathiri figo kwa kiasi kikubwa.

All in All nikikumbuka nilivyoponea kuambukizwa HIV na memba mmoja wapo humu ndani nikaponea chuchupu hadi sasa sitaki tena kuzamia PM za watu humu ndani (Hiki ni kisa nitakileta kwenu siku yoyote nikipata nafasi) mfahamu ni kwa jinsi gani baadhi ya watu hufanya makusudi kuambukiza watu wengine.

All in all Ukimwi upo na unaua chukua tahadhari.
Dah nimeogopa mkuu haya mambo ya kuzama bobo [emoji26]
 
Back
Top Bottom