TANZIA Mwanachama wa JamiiForums - Jikeshupa amefariki dunia

Apumzike Kwa Amani [emoji120][emoji120]
 
Ni kweli kabisa ndugu yangu hakuna mtu ninaye fahamiana naye nje ya hapa ambaye likitokea lolote anaweza kuleta taarifa humu.!!

Hilo ni kweli usipo niona hapo muda mrefu ujue Kuna shida sehemu mana siwezi acha chama langu Simba bila support ata siku Moja.

Binadamu maisha yetu ni kama umeme wa Tanesco tu muda wowote unaweza kukata.😭

Kikubwa kukumbuka Ibada, kuishi vizuri na watu, kutenda yaliyo mema Kwa kadri tuwezavyo, kupendana sisi Kwa sisi na kusameheana kwakuwa hatujakamilika hivyo ni muhimu kuchukuliana madhaifu yetu n.k.
Ili siku tukiondoka duniani tuwa na angalau chembe ndogo ya hadhina ya mema Kwa Mungu Muumba pamoja na Dua za wapendwa wetu tutao waacha basi tunaweza kuvuna rehema za mwenyezi Mungu mwenye haki ikiwa itampendeza Kwa mapenzi yake mwenyewe.

Duniani tunapita kaka mbele yako nyuma yangu, Mungu wa upendo atusaidie.

One love Brother!!
 
Waliposema tangu alipozaliwa anatumia ndipo waliponichanganya, kwamba kazaliwa miaka 17 iliyopita?
 
Pole kwa Familia yake

Mimi ninatoa zawadi kwa mtu atakeye nifahamu mimi ni Nani
 
Duh watu wanajuana kabisa, mimi nikifa mtasikia kwenye vyombo vya habari, na mtaona pilika za viongozi kadhaa. Maana sina hakika ila nina imani Rais atahudhuria au kutuma mwakilishi wake
 
Dah nimeogopa mkuu haya mambo ya kuzama bobo [emoji26]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…