Mwanadada anaefanya kazi melini anaeleza faida na changamoto anazopitia

Mwanadada anaefanya kazi melini anaeleza faida na changamoto anazopitia

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Nilisoma kutoka kwenye gazeti, dada mmoja anasimulia changamoto anazopitia katika ajira yake kama mhudumu wa meli. Alianza kazi akiwa na miaka 22 na amedumu katika ajira hii kwa miaka 10.

Kazi inakupatia malazi na chakula bure. Siku unazolipa kodi ya nyumba ni siku ukiwa likizo. Anasema ameishi kwa miaka 10 bila kulipa kodi ya nyumba wala kununua chakula. Akiwa likizo ni rahisi kwake kukaa hotelini kuliko kuanza kutafuta nyumba.

Changamoto ya kwanza huyu mwanamke alieleza ni kushindwa kudumu kwenye mahusiano kwa muda mrefu. Huyo boyfriend atakae kusubiri mwaka mzima mpaka uwe likizo na awe na mipango endelevu na wewe ni shida kumpata.

Changamoto ya pili ni abiria wa kiume kutongoza hasa wakati wa usiku wanapotafuta mtu wa kuua nae usiku. Tatizo wengi ni waume wa watu na wanakueleza kabisa taja bei yako lakini no strings attached. Ukizingatia mkiwa baharini hawawezi kupiga simu wampate mdangaji.

Kuna kusafisha sehemu ya engine na kutoa mafuta machafu. Anasema hii kazi ukiifanya ukiwa Caribbean au Bahamas ni raha tupu. Usiombe uifanye wakati wa Kipupwe na meli iko Norway.

Moja ya majukumu ni kufanya usafi katika meli. Anasema kuna wanaoacha kinyesi kwenye swimming pool. Kusafisha vyumba vya wapenzi wa jinsia moja hasa wanaume ni shughuli nzito, unaweza kukuta kinyesi kutoka chumbani mpaka chooni na shuka zimejaa kinyesi.

Ameeleza haya kwakua anaacha kazi sasa ili aanze maisha ya familia.
 
Natamani atokee muandishi wa kitabu au movie writer atengeneze kitabu au movie na main character awe mdada wa usafi wa meli aliyefanya kazi ya usafi kwa miaka 10.
😂😂😂😂 nilicho gundua ni uwezo wa wanawake kuelezea matukio. Wanaume wameifanya hii kazi kwa miaka mingi lakini hatukuwahi kuyajua yaliyomo.
 
Nilisoma kutoka kwenye gazeti, dada mmoja anasimulia changamoto anazopitia katika ajira yake kama mhudumu wa meli. Alianza kazi akiwa na miaka 22 na amedumu katika ajira hii kwa miaka 10...
Pengine pote nitafanya ila kusafisha vyumba vya wa penzi wa jinsia moja amepata laana ambayo haisameheki kwakuwa kitendo cha kusafisha kumbe anabaliki
 
Back
Top Bottom