MwanaFA azomewa na wananchi baada ya kuanza kusifia Awamu ya 6 kwenye Tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva

MwanaFA azomewa na wananchi baada ya kuanza kusifia Awamu ya 6 kwenye Tamasha la miaka 30 ya Bongo Fleva

Wananchi wakataa mapambio ya MwanaFa kwenye miaka 30 ya Bongo Fleva


Katika hali isiyo ya kawaida, Naibu waziri wa Michezo, Sanaa...., Mwinjuma Hamis maarufu kama mwanaFa amezomewa na kukataliwa na wananchi waliohudhuria tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva, pale alipotaka kuanza kusifia na kuipelemba serikali.

Nimecheka sana, kamaindi kishenzi akaishia kusema maneno ya mkosaji ''No problem, moja ya sababu zilizofanya sisi tukutane hapa, ni kwamba ninyi mmetuunga mkono, na mnavyotaka ndivyo tunavyotaka sisi''

Raia mtaani zimechoka, hazitaki ujinga
Tufanye hivi hivi kila wakati kwa wanaosifia ccm ukichanganya na maandamano ya kusafisha mitaa yote, nina imani tutafanikiwa sana!
 
Mpuuzeni tu Mwana F.A,kwake y Siasa ni -Zali La Mentali-kimaisha,hukuwahi kuwa na fikra wala msukumo binafsi wa kuwa Mwanasiasa.

Kati ya Wanasiasa wa Tanzania wanaotokea ghetto anayepwaya ni Mwana,F.A.

Ni zao la Siasa za kishamba za Marehemu Magufuli,kwamba CCM nayo uwe na Wabunge Wasanii eti waiongezee mvuto.
Ndiyo akapigiwa chapuo na Madam UMMY MWALIMU,aliyekuwa rafiki sana wa JPM.

Sugu,Baba Levo,Profesa J,Jokate..wao hata kazi zao za sanaa zilikuwa zina aksi utetezi wa haki na Siasa kwao bado inabaki kuwa ni moja ya platform ya kuendeleza harakati za kutetea wanajamii..na hata hawategemei msukumo wa Serikali pekee.

-Mifano michache:
1-Baba Levo anailalamikia Serikali juu ya Wanafunzi wa Elimu ya juu kukoswa Mikopo huku anaingia mfukoni mwake kuwapatia hela wakaendelee na Masomo kwa kadri uwezo wake unavyomuruhusu na si kuwakopesha.

2-Jokate-ametumia vilivyo exposure yake ya Usanii kwa kutafuta wafadhili wa nje wakajenga shule akiwa D.C.Kisarawe.
3-Sugu-akiwa mbunge aliwahi kusambaza tablets kwenye baadhi ya Shule akiwa Mbunge,kwa kuwatumia rafiki zake wa Marekani waliotokana na Usanii wake.

HAYA:-
Mwana,F.A:-

Amekuwa ni msambazaji wa pesa za Mama Samia kwenye Misiba ya Wasanii na kwa Wasanii wanao umwa!!

Na akifika utambulisho ni huu

-:..Mama amenituma pokea/anakupa pole...!!!

Hana Dira wala jipya,nje ya kusifu Serikali na Viongozi.
Sifa za kifala tu yule mwingine sijui jerry nashon naskia ni mkamataji sana tu wa vidumu vyetu hivi vya sh3.
 
Wewee, Dr Samia Suluhu Hassan, The Mother of Modern Tanzania, siyo mshamba wa kuumizwa na kajambo kadogo kama hako, yule ni mtoto wa mjini kitambo na anazijua siasa enyi nyumbu muelewe. Mipango yake inasonga kama kawa hivyo nyumbu jiandaeni tu kuwa killed softly.
Wewe unaweza kua Samia hii ID
 
Babu tale na madee machozi yamelenga
Naamini mwana Fa na Babu tale wakistaafu siasa hawatathubutu kuiongolea, pale angeoanda sugu na hata angesema wadau wamuimbee lisu atoke au hata Luhanga mpina angeshangiliwa.

Nashangaa watu kama Sugu lazima alikuwepo watu wa set-up wamelala
 
Wananchi wakataa mapambio ya MwanaFa kwenye miaka 30 ya Bongo Fleva


Katika hali isiyo ya kawaida, Naibu waziri wa Michezo, Sanaa...., Mwinjuma Hamis maarufu kama mwanaFa amezomewa na kukataliwa na wananchi waliohudhuria tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva, pale alipotaka kuanza kusifia na kuipelemba serikali.

Nimecheka sana, kamaindi kishenzi akaishia kusema maneno ya mkosaji ''No problem, moja ya sababu zilizofanya sisi tukutane hapa, ni kwamba ninyi mmetuunga mkono, na mnavyotaka ndivyo tunavyotaka sisi''

Raia mtaani zimechoka, hazitaki ujinga
Watazamaji hawakuingia na chupa za maji ?
Jamaa kajichekesha sana, sijui kama atasahau!
 
Waandaaji walibugi tu kidogo. FA angepiga simu kwa MAMA akaongea mwenyewe live sidhani kama kuna mtanganyika angezomea..
 
Falsafa imezomewa wazi wazi, Waja wameshachoka kuburuzwa na uongo wa mboga mboga.
 
Back
Top Bottom