Mwanafunzi aliyejiteka mwenyewe ili apate milioni 3.5 akutwa gest akiponda raha

Mwanafunzi aliyejiteka mwenyewe ili apate milioni 3.5 akutwa gest akiponda raha

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1683989276286.png


Mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi shirikishi ( CUHAS) cha Bugando mkoani Mwanza Kennedy Nyangige amekamatwa na Jeshi la Polisi wakati alipojaribu kuwalaghai wazazi wake kuwa ametekwa na watekaji wanahitaji fedha milioni 3.5 ili waweze kumuachia.

Kwa mjibu wa kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema, mwanafunzi huyo alijiteka na kukaa gesti moja iliyopo Igongo katika chumba namba 103 kwa lengo la kujipatia kipato.

"Huyu alikuwa amepumzika kitandani miguu juu maisha yanaendelea na yeye alikuwa anaendelea kunywa bia zake, Polisi baada ya kumkamata tulimhoji na alikiri kuwadanganya wazazi na viongozi wa chuo kwamba alikuwa ametekwa ili apewe fedha aendelee kula starehe," amesema kamanda Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa, akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza, amewahiza vijana kuacha janjajanja kwa kuwa wameaminiwa na familia zao kwa kuwalipia gharama kubwa katika vyuo kuvumilia na kusoma kwa bidii mpaka pale watakapo hitimu masomo, waende kutumia fedha zao wenyewe pindi watakapopata ajira.

Credit: Jambo TV
 
Jitu kama hilo mi silisomeshi tena! Jinga kabisa, wazee wa watu wangekufa kwa presha je?!
Tatizo la vijana wa siku hizi wao kila wanacho ona kwa tv basi lazima wageze! Hapo utakuta alisha angalia movie Kama hiyo na pesa ikatoka,basi na yeye anazani in real life itakua very simple Kama kwenye movie!!
 
Back
Top Bottom