Watanzania wabadilike katika kuchambua mambo na wasikurupuke. Ni wazi wachangiaji wengi katika thread hii ama ni marafiki wa mhanga au wana bifu na wana SAUT hasa akina dada. Wanafunzi wanapokuwa hostel au majumbani kwao kuna kanuni za kuwatembelea. SAUT mwisho wa mtu asiye mwanafunzi katika hostel ya chuo awe mwanaume au mwanamke ni saa 12 jioni. Wanafunzi wana uhuru wa kukaa hostel hadi saa 4 usiku. Kanuni hii si mpya katika vyuo Tanzania. Kijana mhanga ambaye ameuawa, kwanza si mwanafunzi wa SAUT na hajawahi kusoma SAUT. Aliyepost kwamba huyu ni mwanafunzi wa SAUT ana nia ya kudanganya jamii na kupaka matope chuo cha SAUT kwa maslahi yake au ya wahalifu wenzake. Wizi katika hostel za wanafunzi si jambo jipya na hivyo kutawala hasira za wanafunzi na wananzengo sio rahisi katika Tanzania ya leo. Juzi mtaa wa Nganza risasi zimepigwa na mtu amekufa, fedha zimekombwa na wengine kujeruhiwa. Je watanzania kweli wana sababu ya kutetea mtu anayekutwa maeneo ambayo hapaswi kuwepo? Kijana mhanga hakuwa na mpenzi SAUT. Na kama alikuwa anaye, basi ushahidi utolewa kwani hiyo picha inayozungushwa ni ya zamani na si ya jana wala leo. Mwizi ni mwizi hata avae suti. Mjaribu kuchunguza family history ya mwizi, na matukio yake ya awali kama wizi wa laptop hapo hapo SAUT, msikurupuke. Kupiga mayowe ili kujitetea ni natural reflex kwa mtu yeyote. Kukimbia na kushikwa na wanafunzi na wananzengo nje ya hostel ni dokezo wazi kwamba kijana alikuwa anajua ana hatia. Tangu lini mwanaume umkimbie mpenzi wako? Kama ilivyo elezwa na PR wa chuo, kijana alikutwa ndio anachomoka room na simu ya mtu. Mlitegemea dada wa SAUT afanye nini, usiku wa saa 3. Msiwalaumu mabinti bila kuchambua ukweli wa mambo. Za mwizi ni arobaini. Mnaotetea wizi na uhalifu katika mwamvuli wa mapenzi mtapata matatizo hayo hayo. Mabinti wawe na nidhamu wawapo chuoni, na akina kaka wawe na nidhamu pia. Wizi sio ajira nzuri. Msikurupuke katika thread hizi, kutukana wanafunzi nk, acheni vyombo husika vifanye uchunguzi.