Mwanafunzi wa UDSM akamatwa kwa kusambaza taarifa na Takwimu za uongo za Covid-19 WhatsApp

Mwanafunzi wa UDSM akamatwa kwa kusambaza taarifa na Takwimu za uongo za Covid-19 WhatsApp

Ndiyo; kwa mtazamo wangu. Kwa nini unadhania takwimu za mtu binafsi ndizo za kweli ambapo waziri anayepewa takwimu kutoka pembe zote za nchi takwimu zake ziwe si sahihi? Simple logic.
Hajalazimisha kwamba takwimu alozotoa kipindi anachati wasapu nduo za kweli.
Takwimu rasmi SI zinafahamika,,kwanini upoteze human resource kusneak kwenye magroup watu wanapiga soga kutafuta mtu wa kukamata?

bado upoteze resource kumsaka na kumkamata na bado resource za kumweka ndani na kumpeleka mahakamani kwa kupiga soga?
 
Wamsamehe tu,hii sheria huko mbeleni inabidi wake waifute,Uhuru wa kutoa maoni Hapa unakiukwa,kila mtu anajua takwimu rasmi Ni zipi na kila mtu anafuatilia taarifa rasmi kwa umakini Sana,
Uhuru wa kutoa maoni upo; lakini una mipaka yake. Siyo kwamba unaweza kusema cho chote tu hata kama kinaleta taharuki kwenye jamii. Ndiyo maana hata Marekani mnayoisifia kuwa na uhuru wa kusema, mpaka leo inamfuatilia mtu wa wikileaks;

na si kwa sababu alisema uongo, bali kwa sababu alitoa siri za serikali. Huo ni mfano mmoja tu wa kwamba uhuru una mipaka yake. Wapo wengi tu wanaoshikiliwa au kufuatiliwa na Marekani kutokana na walichokisema.
 
Ng'wanamalundi,
Ni kweli,,kwa hizo nchi lazima suala liwe critical na liwe na athari zinaonekana,lakini sio kea kufuatilia magroup ya watu wanapiga soga wasapu,ujue Kuna kupiga soga Ama kuchat na Kuna kutoa taarifa rasmi.

Mfano,online TV Kama kwanza ingetoa hizo takwimu Kama sehemu ya taarifa zake,amo blog tuseme ya Mr mchuzi ingeweka article za takwimu hizo,Hapo sawa.

Lakini watu wanachat,kuchat Ni sawa na mko kijiweni tu mnapiga story,hizo SI taarifa rasmi na hazina athari inayoweza ku influence situation
 
Maswali ya kitoto hayo. Taarifa sahihi ni zile zinazotolewa na waziri mhusika. Askari wamejua kuwa taarifa za mtuhumiwa sio sahihi kwa kuwa ni tofauti na taarifa ya waziri ambaye anaarifiwa kutoka pembe zote za nchi na baada ya kujumlisha takwimu hizo ndipo anatangaza. Huyu mtu binafsi amepata wapi takwimu zake? Swali la mwisho kwamba taarifa ya mtuhumiwa imeleta madhara gani ni la kipuuzi mno na halihitaji hata kujibiwa.
Jibu lako lipo sawa kabisa
Na kama hatoelewa hapa,Basi arudi darasani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom