MwanaHalisi ladai Ben Saanane huonekana kwa jamaa zake

MwanaHalisi ladai Ben Saanane huonekana kwa jamaa zake

Ninachokina ni kichokonoa habari tu ilikuvuta hisia za wengi na kutaka kufuatilia hii habari katika gazeti la mwanahalisi hivyo HATUWEZI kukomaa na hicho kichokonoa habari tena kinachoonyesha kimechukulia kutoka katika maoni ya mtu ambaye ni mjumbe wa kamati kuu CDM na kuifnaya sasa ndio habari kamili.Hapa naona kwangu ni mchezo tu wa kuvuta wasomaji na kuwajengea shauku ili wanunue gazeti na walisome kisha humo kwenye habari kamili ndio ilipaswa watu wajenge hoja siyo kwenye hiki kilicholetwa kama kichokonoa habari na ambacho hata hivyo kinaacha maswali mengi kuliko majibu na kimekaa kimtego zaidi
 
Hii ishu ya huyu kijana ni kuipotezea tu kama wafanyavyo serikali kwani hii ni Ze Comedy isiyokuwa na faida kwa taifa. Mtu kajificha mwenyewe kisha anataka atafutwe, kwa msingi upi?
huyu kijana jipya,na hii stori itamfanya asiaminike tena
 
Bado nina kumbukumbu ya Ben na mwanzilishi wa mtandao wa https://jamii.app/JFUserGuide wakati fulani; kisa eti "alishawishiwa" kutumia mtandao huo zaidi. https://jamii.app/JFUserGuide ilikuja kuwa mbadala wa JF kwa kupanua uhuru wa kutoa maoni. Sijajua kwa sheria ya mtandao ya sasa mtandao huo unatimizaje azma yake hiyo.
=======
Taarifa hii kama ina ukweli, basi nadhani ni dalili za mtu kuandaa utaratibu wa kubadili staili ya maisha yake.
 
Hata Sokoine yasemekana alikuwa akionekana ofisini kwake baada ya kifo chake miaka hiyo tuliadithiwa...

Pia tukaambiwa uzushi kuwa simu ya Kanumba huwa ukipiga inaita tu lakini haipokelewi tuliambiwa kwenye tigo pesa ukituma zinatolewa😀
 
Sioni sababu yoyote kwa Kubenea au gazeti lake la Mwanahalisi kuzusha habari hii. On top of that, ukweli kwamba Mbowe na viongozi wengine wa ngazi za juu Chadema wamepuuzia ishu ya "kupotea" kwa Ben, makes even more sense.

======


UTATA kuhusu kutoonekana kwa Bernard Saanane, msaidizi wa masuala ya siasa wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe sasa unazidi kuongezeka. Wanaandika Waandishi Wetu …. (endelea).

Taarifa zinasema Saanane ambaye haonekani nyumbani wala kazini, anaonekana kwa marafiki zake mitaani. Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema amesema, “Nina wasiwasi kama siyo mkakati binafsi wa kisiasa.

Kijana Saanane amekuwa akionesha kutaka kukwea madarakani haraka hata nje ya taratibu. Tafuteni tu mtaona.”

Rejea Mkenya aliyetengenezwa kwa issue ya Dr. Ulimboka
 
Hapa Public inaandaliwa na Tsunami aliyoandaa Ben dhidi ya Chadema ili asiaminike mapema (hii ilifanywa kwa Dr Slaa na kupumbaza wengi) ...hii itakuwa hivi mkiona mwelekeo wa habari kutoka Mwanahalisi ukiwa wa kumchafua Ben ....Nahisi serikali na CCM wameamua kukaa kimya ili liwalipukie wenyewe ....
Bado Upumbav u uleule wa kuhisi.eti nahisi.hii nchi ndiyo maana maskini
 
Fakenews ishakuwa tatizo la kidunia.
Juzi hapa wakaandika fakenews kuwa waziri wa ulinzi wa israel ameionya pakstan kutopeleka askari wake syria kwa kisingizio chochote kile na ikifanya hivyo israel itailipua syria kwa nyuklia,


habari ni fake,sijui pakstan hawakujua kuwa ni fake,waziri wa ulinzi wa pakstan akajibu,hata wao wana silaha hizo za nyuklia.

Fakenews zinaweza kuleta madhara makubwa yasiyotarajiwa.

this is fakenews


Una uthibitisho kwamba hii ni fake news Mkuu?
 
Bado nina kumbukumbu ya Ben na mwanzilishi wa mtandao wa ******************** wakati fulani; kisa eti "alishawishiwa" kutumia mtandao huo zaidi. ******************** ilikuja kuwa mbadala wa JF kwa kupanua uhuru wa kutoa maoni. Sijajua kwa sheria ya mtandao ya sasa mtandao huo unatimizaje azma yake hiyo.
=======
Taarifa hii kama ina ukweli, basi nadhani ni dalili za mtu kuandaa utaratibu wa kubadili staili ya maisha yake.
Mwanahalisi Forum
 
Uhuru wa kutoa habari mwandishi asihojiwe. Kwanini ahojiwe sasa mwandishi wa habari?

Labda wanaanza kuandaa watu kisakilojia kabla ya kutokea.
 
Back
Top Bottom