Laiti tungefanya mapinduzi katika nchi hii kuliko haya yanoendelea sasa,kwasababu mtanzania yeyote yupo subject kupatwa madhara na mauti,kwasababu tu ya kusimamia anachokiamini kwa vile tu hakiwapendezi viongozi.
Mambo mabaya na ya kutisha tunafanyiwa hakuna anayejali,tumefungwa kwenye gereza la njaa kutokana na wasimamiaji wetu wakuu wa uchumi wamegeuka kuwa vibaraka wa wageni.
Na mahali walipotuweka kiuchumi hawataki tutoke maana kama njaa itakuwa si tatizo tena kwetu basi tutahangaikia usalama wetu,ambao kimsingi wao(viongozi) ndo wenye dhamana kubwa kwenye hilo.
Kwa matukio yote haya ya kina Mwakyembe,Kubenea,Ndimara,Ulimboka,Mwangosi na kadhalika vidole vyote vinaelekezwa Ikulu halafu wabongo wametulia tuli,utasikia vijikelele vya hapa na pale baada ya muda kimya,na viongozi huko wanasema watz ni wasahaulifu yatapita tu.
Sasa sijui tunangoja adhurike nani au auwawe nani ndipo tuamke. Mpaka hapa tulipofikia hii serikali tuliyonayo imepoteza uhalali wakutuongza watanzania,MAPINDUZI nikitu cha lazima sana sasa, SAA ILIYOKUBALIKA NI SASA,WAKATI WA UKOMBOZI NI SASA.
Hawa jamaa tunatakiwa kuwaondoa kisha wanatiwa hatiani kwa yote yanayofanyika sasa hakuna cha The Hague wala nini tunawafanyia hapahapa,ili iwe mfano kwa wengine watakaokuja ili angalau tupumue,kwa kweli hali ilivyo sasa ni maisha ya mashaka,wasiwasi,haipaswi kuwa hivi kwenye taifa ambalo lipo huru.
Na ni wakati huo ukifika utaona na hapa jf patabadilika sana, kwasababu wengi tutaingia hapa kwa majina yetu halisi.