Nicas Mtei
JF-Expert Member
- Dec 21, 2010
- 11,556
- 7,097
Dah,
Na Chilisosi naye katoweka
Una akili za kitoto ee?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah,
Na Chilisosi naye katoweka
Mwanaharakati Marcosy Albanie ametoweka nyumbani kwake baada ya kufuatiliwa na watu wasio julikana kwa kipindi cha siku kadhaa.
Mtakumbuka mara ya mwisho Bwana huyu alionekana kwenye kipindi cha kipima joto kilicho rushwa kwenye runinga ya ITV kikimshirikisha yeye, mbunge wa Singida mashariki Mh Tundu Lissu pamoja na naibu spika Mh Job Ndugai.
Chanzo: Mabadiliko.
NB. Marcosy anajishughulisha na taasisi ya kiraia inayo fuatilia mwenendo wa shughuli za bunge pamoja na masuala mengine katika jamii.
UPDATE:
JamiiForums imewasiliana na Macossy yu mzima, hakuwa jijini Dar lakini yupo salama.
kitalolo
tanzania ya leo ni zaidi ya tunavyoifahamu
wanatulazimisha kurudi enzi za ujima
na ukijitokeza kusema kweli ni ole wako.
'..........Navumilia tu kwani haya yote yana mwisho..............'
duh!hii ni balaa,jf hivi imesajiliwa wap?nadhaan inawachefua zaidi ya kitu chochote wangeweza wangeshaifunga....Sasa kama Chadema wana uwezo mkubwa namna hiyo kuna hatari tukasikia Kikwete katekwa na Chadema
Mkuu. Naamini hawa manguli wanachukua hatua thabiti kuepusha macho na meno yao dhidi ya makoleo ya kina Joseph Mulundi.
Atakaye pona JF ni Invisible peke yake maana hawata muona au huenda wako naye lakini hawamuoni.
Mkuu wewe kweli ndo unaijua siasa!! Umeucheeeeki ule uzi wa Lwakatare, kila ukipiga mahesabu unakuta kukanusha haukanushiki, kuuunga mkono haiwezekaniki; badala yake ukaamua kuja kutudondoshea lijinyuzi lingine huku!
Kavaeni mikanda ya kujilipua mfe nayeYeye si ametaka afe, anakimbia nini tena. Aheshimu ujumbe wa bango lake. Shujaa hakimbii uwanja wa mapambano
Mkuu NasDaz
Umeniacha hoi; nimecheka sana; Mohamedi Mtoi anataka kutufanya sisi mapimbi kule kwa Lwakatare kwenye moto hatii mguu anatuletea uzushi ambao mods wamepangua; mkuu NasDaz hawa kina Mohamedi Mtoi wapo JF kwa viposho wanavyopewa pale mtaa wa Togo wapo wengi sana humu JF wanaganga njaa kwenye siasa; na wengine wanajipendekeza kwa viongozi ili wafikiriwe kupewa vijinafasi; sisi tupo JF tukiwa na uhuru wa mawazo hatupo hapa kumfurahisha mtu tunakupa kitu stereo kama kilivyo.
Chama
Gongo la mboto DSM
Mkuu chama.
Naona unazidi kujidhihirisha kuwa uwezo wako niwa chini sana! Hivi ulikuwa unataka nikaee kwenye uzi wa Rwekatale tu kutwa kucha kama unavyofikiria wewe?! Au mchango wangu hujauona?!
Na je, moderator amekanusha kuwa Marcossy hatafutwi au ali update kuwa ni mzima?! Au kwa akili yako kutafutwa na kuwa mzima ni jambo moja?! Hata ulimboka pia alikuwa mzima alipo tafutwa na Mulundi kufanya kazi yake nini kilijiri?! Je haiwezekani kwa Marcossy?!
Hata hivyo, wenye akili wanajua mchezo uliopo nyuma ya sakata la Rwekatare, siongozwi na ushabiki au kutetea kila kitu ila ukweli ukidhihirika kwa kuwa tuko hapa hapa tuta kumbushana.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Mkuu wewe kweli ndo unaijua siasa!! Umeucheeeeki ule uzi wa Lwakatare, kila ukipiga mahesabu unakuta kukanusha haukanushiki, kuuunga mkono haiwezekaniki; badala yake ukaamua kuja kutudondoshea lijinyuzi lingine huku!
Mkuu.
Usiwe na closed mind kama chama! Hivi kama tayari kuna uzi wa Rwekatare kwenye mjadala mimi kazi yangu ni kuja kukanusha ya Rwekatare hata kama sina uhakika na kinacho mhusu?! Mimi sio wa hovyo kiasi hicho mkuu!
Na kuanzisha uzi mwingine kuhusu jambo lingine ni haki yangu ya msingi kama jinsi aliye anzisha uzi wa Rwekatare alivyo tumia haki yake ya msingi. Swala la msingi ni kujiridhisha kama ni kweli au sio kweli.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Tuombe Mungu asije akawa amepelekwa Msitu wa Mabwepande.
Kwa ufupi leo nimepata mawasiliano na Marcossy na amesema hakika hajambo, japo hakutaka kuongea kwa urefu na kudai atulie kwanza akili ikae sawa ndipo ataongea.