Mwanajeshi kumshambulia dereva wa daladala ikiwa na abiria ni kuhatarisha maisha ya abiria pia

Hizi akili za kijeda hizi. Nani aliyekuambia kosa moja huondolewa kwa kufanya kosa lingine? Kwamba kwa sababu dereva wa daladala alikosea then inampa askari haki ya kufanya kosa la kushambulia na kudhuru mwili?
 
Madereva wa daladala acha wafundishwe adabu,hua wanakera na kujifanya wanajua uhuni wa mjini

Askari yupo sahihi kumpa kichapo,wengi wa hawa madereva hua ni wajeuri,hawana heshima wala ustaarabu

Safi sana Askari
 
Kweli madereva baadhi yao wa daladala wana lugha chafu na dharau , utasikia mara gari ya mkopo, mara ntakufanyia zengwe nkuchomkee ,mara gari si yako , mara huna la kunifanya

Lakini sio wote


Hapo nikuangalia tukuo zima lilivokuwa
 
Wanaume wa dar wanazingua sana,uwakute sasa na vibukta vyao asubuhi wanakimbia pembezoni mwa barabara,na vifua kama njiwa,utadhani wapo serious [emoji3][emoji3],gari zima wameshindwa kumkalisha huyo mpuuzi.
Halafu hawa ndio Mbowe kawaita wafanye maandamano kweli?? wanaume mjeshi mmoja wanamtizama tu. Ngoja tuone itakavyokua, ila kama wanaume wenyewe ndio hawa haahaaha, nchi ngumu sana hii.
 
Huu ni ushamba, sasa hapo Dereva akijihami kwa bisibisi akamuua mjeda utashangaa tena kesi inageuka kwa raia kwamba wameua askari. Watatuma platoon nzima kutandika madereva, makonda na wapiga debe wa daladala.

Haya majeshi ya watu weusi yamekalia nguvu kuliko akili ndio matokeo yake haya.
 
Watawatafuta na watakamatwa tu. Hawa ndiyo wale wasio raia wa Tanzania ( wakiwemo wakimbizi) tunaosema wamejipenyeza serikalini na kwenye taasisi nyingine za serikali na wengine kupewa uteuzi.
 
Ndio operations wanazoziweza ukiondoa kuvunja matofali kwa kichwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…