TANZIA MwanaJF Ndikwega afariki dunia katika ajali ya gari eneo la Igawa

Huwa mnamtambuaje mwanaJf akifariki? Wakati wengi wanatumia I’d fake
 
Pole ya wafiwa wote,
Najiwazia mimi nitakapokufa nani atajua humu? anyway mkiona kimya zaidi ya mwaka mjue nipo kwa baba namimi[emoji44]
Inabidi watu tufahamiane watu humu Kila siku majanga.
 
Hiv Eyce utapata vp taarifa uzilete hum siku nikuvuta???

Ila kama kweli vile kaka, ila hiyo simple ngoja nianze route za kuja huko familia inijue kwa ukaribu.. Ila mimi nitakusogezea account yangu ya facebook na linkedin maana huko nikivuta lazma utaziona R.I.P's za kutosha
 
Tuwe pole sote.
 
Sio wotr zimejaa tabu..wengine bata tu mpaka mauti yanawakuta wanakula bata..acha kukariri mistari vibaya
Siyo kwamba wewe ndiyo umekariri vibaya mkuu, kwenye kuitafsiri tabu maana kwenye akili yako umefikiria maisha ya shida lakini ukasahau hata kuipata hiyo hela ya kula bata ni tabu pia na ndiyo msingi wa aya
 
Poleni sana wanaJF kwa msiba huu mzito.
Igawa pale siyo pazuri kabisa, miaka mitatu nyuma almanusura na mimi nibaki historia kama siyo kuamua kulipeleka gari korongoni kwenye majabali ningekuwa maiti.

Kama unaingia Igawa kutokea Mbeya kilometa kama tatu nne hivi kuna kilima cha ajabu sana. Pale gari hasa mabasi ya abiria yanapaa eneo hilo, wanapiga ovateki za kifo na barabara imezingirwa na korongo lenye mawe mchongoko.

Loh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…