Kuna video inazunguka mtaani ikimuonyesha binti aliyebeba mtoto akihojiwa na mtu aliyefunika uso wake,
Nimefanya uchunguzi binafsi nakujiridhisha video hii niyakughushi kama vilivyo vyeti vya Daudi Bashite.
Bila kuangalia maudhui yaliyokwenye video, mimi naangalia uhalali wa video na Kadi iliyowekwa hadharani kwamba ni kadi ya kliniki ya mtoto aliyebebwa na mama huyu.
Kuna mambo makuu mawili ambayo kitaalamu kwamjibu wa Sheria ya uchunguzi hasa Forensic Psychology,
Jambo la kwanza ili ugundue kuwa mtu unayezunguma naye au mtu anayezungumza mbele yako ni muongo, utayaona macho yake,
Kuna uongo wakulishwa yani unasisitizwa useme hivi:, na uongo wakutengeza mwenyewe, yani kipaji cha uongo mtu anachozaliwa nacho, hapa kwenye macho hutoa majibu mawili.
Uongo wa kulishwa: Mtu wa aona hiyo utamtambua wakati akiongea mboni za macho yake zile nyeupe zitakuwa zikionekana zote kanakwamba anatumia nguvu hii husababishwa na misuri ya macho kuuvutika...
Uongo wa Kutengeneza mwenyewe: Mtu huyu macho yake huwa hayatazami mbele, huangalia pembeni, Hurusha mikono mara kwa mara aongeapo, hupenda sana kujiapiza.
Kwadhana hiyo sasa nawapeni tafakuri kwa video hiyo muamue huyo binti na kijana anayemhoji aliyeamua kujifunika uso.
Lakini kadi iliyowekwa mitandaoni ikiambatana na video hii kwa lugha rahisi imeivuruga video na kudhihirisha kuwa video hiyo ni feki.
Kuna mapungufu mengi ndani ya kadi hii yanayofuta uhalali wake. Hii kadi mmeshindwa hata kuijaza?
1. Jina la hospital aliyozaliwa,
2. Jina la daktari au mkunga aliyemzalisha.
3. Mhahali anapoishi.
4. Jina la mjumbe/mwenyekiti wa mtaa...
5. Hata muhuri wa kuchonga kariakoo tu au sahihi yakughushi imewashinda?
Mkitaka kuwa waongo msisahau vitu vidogovidogo hivi::::::::::::::::::