realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 3,925
- 8,853
Hususan Maeneo ya Vijijini na hata baadhi ya Familia Mjini Mwanamke akianza kutambua na kudai haki zake huonekana ana kiburi sana.
Halafu cha kushangaza sasa unakuta wanawake ndio wa kwanza kuanza kukandamiza haki ya Mwanamke mwenzao ili mradi tu na wao wasionekane wabaya.
Mwanamke huyu atakapoanza kudai haki yake basi Jamii itamtenga kwa kumuona hafai na anaikosea heshima familia yake.
Kuna tabia ambazo mwanaume anaweza kuwa nazo na ni zile zisizofaa ndani ya Jamii.
Tabia hizo ni kama kumpiga mkewe mara kwa mara, kulewa sana na kurudi nyumbani asubuhi au usiku wa manane, kufanyia watoto ukatili na tabia nyingine kama hizo.
Sasa Mwanamke atakapoinuka na kuanza kuzikemea na hata kuzifikisha kwenye mikono ya Sheria ili haki ipatikane basi Jamii huanza kumtenga.
Kumtenga kwenyewe ni kama kutokumsaidia kushinda kesi, kumlaumu na kumsema vibaya.
Ni muhimu Jamii ibadilike katika hili.