Mwanamke Akianza kudai haki zake, huonekana ana kiburi.

Mwanamke Akianza kudai haki zake, huonekana ana kiburi.

Haki anazidai kwa nani? Kwa nini adai haki kwa watu wengine? Ina maana mwanzo alikuwa nazo halafu akanyang'anywa? Mimi haki zangu hawezi mtu kuchukua mpaka eti nianze kumdai. Haki zangu ninazo, nimezihifadhi, na natamba nazo,ni zangu. Sina haja ya kudaiana na mtu.
😅😅
 
Ujuaji utawaponza sana na masingo mama wanazidi kutaradadi zaidi.

Mtu kulewa na kurudi usiku ni suala la kusema unaenda kudai haki mahakamani?

Mwanaume akiwa hana kipato na akawa na hayo mambo mnaondoka na kurudi makwenu kimya kimya.

Cha ajabu akiwa na uchumi mzuri ndio mnawahi mahakamani na kutafuta msaada eti wa kudai haki (tamaa za kutaka mali)

NINYI NI WEZI KAMA WEZI WENGINE.
Wanawake na waheshimiwe na watu wote
 
Hususan Maeneo ya Vijijini na hata baadhi ya Familia Mjini Mwanamke akianza kutambua na kudai haki zake huonekana ana kiburi sana.

Halafu cha kushangaza sasa unakuta wanawake ndio wa kwanza kuanza kukandamiza haki ya Mwanamke mwenzao ili mradi tu na wao wasionekane wabaya.

Mwanamke huyu atakapoanza kudai haki yake basi Jamii itamtenga kwa kumuona hafai na anaikosea heshima familia yake.

Kuna tabia ambazo mwanaume anaweza kuwa nazo na ni zile zisizofaa ndani ya Jamii.

Tabia hizo ni kama kumpiga mkewe mara kwa mara, kulewa sana na kurudi nyumbani asubuhi au usiku wa manane, kufanyia watoto ukatili na tabia nyingine kama hizo.

Sasa Mwanamke atakapoinuka na kuanza kuzikemea na hata kuzifikisha kwenye mikono ya Sheria ili haki ipatikane basi Jamii huanza kumtenga.

Kumtenga kwenyewe ni kama kutokumsaidia kushinda kesi, kumlaumu na kumsema vibaya.

Ni muhimu Jamii ibadilike katika hili.
Hapa ndipo matatizo ya wanawake yalipo,
Hapa ulicho andika ni HISA tu, hakuna logic/mantic.
Maisha ni Mantic na sio hisia, hisia ziko kwa mitume na manabii.

Ebi twende kwenye logic;
Mfano: Tabia hizo ni kama kumpiga mkewe mara kwa mara
Logic: kwa nini una pigwa mara kwa mara?
unafanya kosa gani mpaka upigwe?
na ukipigwa unachukua hatua gani?
je uliwahi fika kituo cha polisi/ dawati la jinsia?
Huyo mume Ulichaguliwa na watetezi wa haki za wanawake?
Je ulifungishwa ndoa kwa nguvu?
Je njia ya kurudi kwenu huijui?
je umefungwa pingu na minyororo?

KAMA WEWE HUWEZI KUJITETEA, NANI WA KUKUTETEA? JAMII?
 
Hususan Maeneo ya Vijijini na hata baadhi ya Familia Mjini Mwanamke akianza kutambua na kudai haki zake huonekana ana kiburi sana.

Halafu cha kushangaza sasa unakuta wanawake ndio wa kwanza kuanza kukandamiza haki ya Mwanamke mwenzao ili mradi tu na wao wasionekane wabaya.

Mwanamke huyu atakapoanza kudai haki yake basi Jamii itamtenga kwa kumuona hafai na anaikosea heshima familia yake.

Kuna tabia ambazo mwanaume anaweza kuwa nazo na ni zile zisizofaa ndani ya Jamii.

Tabia hizo ni kama kumpiga mkewe mara kwa mara, kulewa sana na kurudi nyumbani asubuhi au usiku wa manane, kufanyia watoto ukatili na tabia nyingine kama hizo.

Sasa Mwanamke atakapoinuka na kuanza kuzikemea na hata kuzifikisha kwenye mikono ya Sheria ili haki ipatikane basi Jamii huanza kumtenga.

Kumtenga kwenyewe ni kama kutokumsaidia kushinda kesi, kumlaumu na kumsema vibaya.

Ni muhimu Jamii ibadilike katika hili.
Sasa mbna mada na maelezo ni tofaut
Mwanaume kuacha pombe ni haki ya mwanamke?
 
Back
Top Bottom