3. Mwanamke mwenye marafiki wa Kiume wengi zaid ya wanawake
“Mimi sipendagi kampani ya wanawake maana hatupendani"
Hapa namba tatu(3) unafeli mjuba!!
Hao wanawake hawana yale mambo ya kugombana au kugombanisha watu, ni watu wanao kuwa huru sana hawafichi maovu yao kwa kujifanya wapo mbali na wanaume. Sio wanafiki.
I had one of them wakati huo nikiwa damu changa sana haitulii.
Sasa kaolewa ana familia yake, jamaa kapata mke kweli kweli.
Hawa wanajua wanaume tunavyo jisifu na kuwapondea wanawake wenzao wanaotoka na wanaume wengi ( hoochie ), kwa hivyo wao wanatoka na wachache wasidharauliwe na wajuba. Si wanasikia mastori wanapokaa na wanaume.
Wanaogopwa sana na wanaume wengi kutokana na kujiamini kwao.
Hawapendi maskendo ya kukusanya wenzie uliowatokea kuja kukuumbua au kukufanyia vurugu, unakuta huyu anakustua fulani nakuchana live umezingua unataka kutuchanganya kama watoto.
"Fulani alikuja tukapanga mmoja wetu akuite utukute wote tukushushue lakini mimi sipendelei makelele na kuaibishana kitaa hivyo ukiitwa na fulani mahali fulani usije. Nimekustua sababu nilikuelewa sana japo umezingua".
In short wanajiamini sana ndio maana umewaogopa na kuwapondea hao namba 3. Mwanaume hapendi mwanamke anaye jiamini sana, ndio sifa ya binadamu yeyote.
Bosi wako kazini akikuona unajiamini haumuogopi anakosa kuajiamini anaanza vita na wewe.
Angalizo: Hawa wanatakiwa wakiolewa waache kushinda na wanaume tofauti na ndugu au shemeji zake.