Watu Weusi bana, Wazungu walikuwa wakitamka hivi kuhusu weusi, hawana akili, dhaifu na hawatakiwi kupewa madaraka
Tukapinga kuwa haya Ni ubaguzi wa rangi, yakaondolewa, Sasa hayo hayo ambayo tukifanyiwa sisi tunalia, hayohayo ndio tunataka wafanyiwe wanawake
Hakuna anayemsema mwanamke awe juu ya mwanaume nyumbani, au popote, kinachosemwa Ni watu wote bila kujali jinsia yao wapewe fursa sawa za kiuchumi na kijamii, waweze kufanya biashara, kumiliki Mali, kusomeshwa, kugombea nafasi za uongozi n.k bila kubaguliwa wala bila kupendelewa.
haya yanaruhisiwa Tanzania kwa kiasi kikubwa Ila baadhi ya nchi na baadhi ya jamii hapa Tz yanakatazwa
Kusema watu wanatoka nje ya ndoa eti ndio iwe kisingizia Ni upumbavu, wanawake hawapo perfect Wala wanaume hawapo perfect, na kigezo Cha baadhi watu kufanya makosa sio kumhukumu jamii nzima