Mwanamke Akishaamua Kukuacha, Yamekwisha

Mwanamke Akishaamua Kukuacha, Yamekwisha

Wafanyavyo wazungu nikaonekana mpuzi mkuu
Dhahama mbele hadhara uzushi tu
Upendo wa dhati ilikuwa script ilikuwa ni uchi
‘Cause Vyote ilikuwa ni movie tu

Nikajajua wamebaki kwenye simulizi
Wale wakubaki njia kuu
Najua nilisema hivi nao wakanijia juu
Tofauti ya hayo maigizo na uhalisia huu
Kupendwa kwa hali na mali ni kwenye tamthilia tu

Tulioana na picha ikaenda slow slow
Aliniambia ananipenda kweli ndivyo
Alivyomwambia Fredy
Kisha akamwambia Francy
Nami nikamwambia Betty Fetty
Na Nancy tukaenda draw draw


Hakuna aliyejiforce alie
Kati yetu hakuna aliyemdosheaaw machozi mwenzie
Hakuwa yeye aliyeziwinda pochi za mashemu
Au mimi mwenye namba nyomi za mademu

Tukajua kuwa mahusiano sio kitu simple
Alliniumiza nikamuumiza tukaishi hivyo
Mwanzoni tulichorana mpaka matching tatoos
Leo wote ni washenzi nafuu hatukuitikia wito

Chorus
Nikikumbuka huwa nataka kulia
Watoto na wakubwa wanaaga dunia
Kwa sababu wanaumia mama wanaumia
Wanaumia mapenzi mabaya
Matajiri walisaza dunia
Hata masikini wanaotanga na njia
Wako ndani wanaumia mama wanaumia
Wanaumia mapenzi mabaya

Ukweli hakuwaa mbali kuujua
Kati yetu hakuna aliyekuwa tayari kukua
Niliokota vidonge vya kutoa mimba nikauchubua
Akakuta condom kwneye nguo zangu kila alipofua

Tukaacha kufanya kwa siri kufanya salama
Kila akitaka aishike hatamu
Alilala na rafiki yangu rashidi bosi wangu kazini
Nikalala na dada yeke wa damu

Mapenzi noma nakuhusia
Shangazi wajomba wanajutia niulize mimi
Mapenzi kidonda utaumia
Yalimtesa kocha wa dunia Mwijuma Muumini

Hii game ikikushinda buni yako
Wanandoa wanafunga ndoa
Hawafungi mlango
Wakimaanisha kuwa yeyote anaingia
Nakumbuka hata nikimshika
Nikimbusu kwa hisia hafumbi macho

Mapenzi karaha nyie msije hata kusikia
Nishaona wajanja wanaziacha Career
Ninapoona wanafunzi nao wanataka ‘dandia
Haki ya mama huwa nataka kulia
Huwa nataka kulia

Nishaona na mke wangu ana pete kidoleni
Akiwa na mshefa pembenj anasaini lodge anatimba ndani
Anaingia mi’ natoka mwili hoi nikiwa nimechoka
Pembeni nikiwa na mrembo ananiita honey

Akivua pete kwenye milango ya bar
Sikuchukia mi mwenyewe nina mipango kando kadhaa
Ngoja niwaambie wale wa true love msitaanie
Kumpenda binadamu ni ushujaa nyie


Kila alichofanya dhidi yangu
Nililipa twende sawa mchongo ndo huo
Alichukuwa mababa
Mpaka wenye umri wa dingi yangu kuniumiza
Nikachukua vitoto vya chuo

Aliingilia kushoto niliingilia kulia
Alipobuni uongo nami uongo niliujulia
Alirudi nyumbani na tai za wanaume tilatila
Nikarudi nikiwa na love bite bila bila

Na umalaya wangu na koti la mtumba
Bendi nikakodi na maua rozi ya size kubwa
Nikampeleka mke wa mtu lodge
Nikazuga ka’ sijaoa na mishumaa
Ilibaki kidogo nichome nyumba

Hizi romance ni filamu tu
Mara nikikuona nasinzia sijui napata homa ya dunia
Ni filamu tu
Kutembea slow motion hatuwezi
Ukimkiss kwenye mvua mvua hainyeshi ni filamu tu
Ni filamu tu
Kutembea slow motion bado hatuwezi
Ukimkiss kwenye mvua mvua hainyeshi ni filamu tu

Alishindwa kuuchukua moyo wangu auwekeze
Nilishindwa kumfanya awe wife anipendeze
Ujanja umeisha uhalisia umeturudisha ndani
Tumeathirika na hatujui ndani kauleta nani

Ushauri kwa kina dada mahusiano ni vita
Wanaume wasafi wapo kwenye vitabu vya kuandikwa
Ukiolewa na ndoa ikayumba jiongeze
Mwanaume ni mchafu ukitaka aliyetukuka mtengeneze

Kwa hisani ya dizasta vina..!
Noma sana!
 
Kuumizwa na mahusiano kupo.

Kwa mfano, mpenzi wangu akiiba ATM card kwenda benki kutoa pesa zangu, hapo nitaumia.

Au aniibie hati ya kiwanja akauze na kutokomea.

Yaani niumie kisa ameondoka tu?!

Siyo kweli. Eti mazoea!

Sikatai wapo wanaoumizwa, ila ni wanaume dhaifu sana na ni wapumbavu tu.

Mwanaume kuendekeza hisia ni ujinga wa kishamba.

Nasema hivi, huyo mwanamke hakuna alichonacho ambacho wengine hawana. Wapo wengi tu wanamzidi kwa kila sifa aliyonayo.

Lazima ujue, kwa asilimia zaidi ya 90, mwanamke ni liability kwa mwanaume, yaani nikae kulilia liability!, si watanicheka watu.
Noma sana!
 
Hakuna mwanamke aliteyeniacha ambaye hakunitafuta baadae kwa hiyo hii stori ni uongo tu
kwa namna nyingine inaweza ikawa kweli. Kuna wanawake huwa wanakua na sababu geniune kabisaa za kukuacha na hawa ni wale ambao walishafanya jitihada sana katika kupambania penzi likae sawa ila mwanaume akawa anazingua , hawa huwa hawarudi kwakua wamefanya maamuzi sio kwa kukurupuka na kutumia hisia zaid bali akili.

Ila wale wanaopata darasa la hovyo huko nje na wakakurupuka hawa ndio huwa wanarudi.
 
Wangu aliniacha kisa,

Alisema OOH akasema anataka kuconcetrate na masomo Tuliachana kipindi anaenda field
kwa namna nyingine inaweza ikawa kweli. Kuna wanawake huwa wanakua na sababu geniune kabisaa za kukuacha na hawa ni wale ambao walishafanya jitihada sana katika kupambania penzi likae sawa ila mwanaume akawa anazingua , hawa huwa hawarudi kwakua wamefanya maamuzi sio kwa kukurupuka na kutumia hisia zaid bali akili.

Ila wale wanaopata darasa la hovyo huko nje na wakakurupuka hawa ndio huwa wanarudi.
 
Wangu aliniacha kisa,

Alisema OOH akasema anataka kuconcetrate na masomo Tuliachana kipindi anaenda field
Ahahahahahahah..
Sasa field kweli, 😂 au kale ka boom ka field kalimchanganya!?
Dahh huyo alikupa sababu nyepes sana.
Angepata ajira je? Angekuambia "nataka ni concerntrate na ujenzi wa taifa" 🤣🤣🤣
 
Ahahahahahahah..
Sasa field kweli, 😂 au kale ka boom ka field kalimchanganya!?
Dahh huyo alikupa sababu nyepes sana.
Angepata ajira je? Angekuambia "nataka ni concerntrate na ujenzi wa taifa" 🤣🤣🤣
Dah mzee! Nikambembeleza kisenge wapi chief baadae akaniambia eti kumuoa mpaka nipate GPA ya 4 mzee
 
Na wenzio walisema hivyohivyo sasa hivi wapo humu kuandika nyuzi za kuomba ushaurii

Nasemaje kichaa anachekesha akiwa hatokei kwenu… omba lisikukute
Halafu ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu
Kama hujawai kuumizwa na mahusiano mpk ukatamani uingie chini ya ardhi trust me zamu yako itafika… na Kama ulishaumizwa basi hutoumizwa tena yakakuuma kama ya mwanzo
Biblia inasema “Upendo una nguvu kuliko mauti” usiwacheke wenzio ukawaona wapumbavu kulilia mahusiano

Watu wapo wengi ila hutompata kama huyo awe alikuwa mbaya ama mzurii
Ni udhaifu wa kiwango cha juu mno mwanaume kulialia kuhusu mahusiano.

Tangu niwe na akili zangu timamu nimepita na manzi kibao na hakuna aliyewahi kuniumiza hata baada ya kumwagana.

Haitatokea kwasababu huyo mwanamke sijazaliwa naye tumbo moja tumekutana tu ukubwani.

Hii principle huwa naishi nayo na ndiyo inanifanya mapenzi yasiniendeshe.

Yaani mnada wote wa wanawake ulivyojaa bado nihangaike na mwanamke mmoja? Haitatokea kamwe.
 
Kuumizwa na mahusiano kupo.

Kwa mfano, mpenzi wangu akiiba ATM card kwenda benki kutoa pesa zangu, hapo nitaumia.

Au aniibie hati ya kiwanja akauze na kutokomea.

Yaani niumie kisa ameondoka tu?!

Siyo kweli. Eti mazoea!

Sikatai wapo wanaoumizwa, ila ni wanaume dhaifu sana na ni wapumbavu tu.

Mwanaume kuendekeza hisia ni ujinga wa kishamba.

Nasema hivi, huyo mwanamke hakuna alichonacho ambacho wengine hawana. Wapo wengi tu wanamzidi kwa kila sifa aliyonayo.

Lazima ujue, kwa asilimia zaidi ya 90, mwanamke ni liability kwa mwanaume, yaani nikae kulilia liability!, si watanicheka watu.
Upo sahihi kabisa mkuu.

Mwanaume unaliliaje liability wakati ndiyo nafuu akiondoka?

Tatizo kuna baadhi ya wanaume wanatumia hisia kupenda wakati hilo ni jukumu la mwanamke.
 
...

Kaka yangu… acha kujidanganya. Acha kujipa matumaini yasiyokuwepo. Mwanamke akishaamua kukuacha, yamekwisha. Naomba nikueleze kitu—hawezi kurudi. Hawezi hata kusikiliza kilio chako.

Unajua ni kwanini?
Ni Kwa sababu hakukuacha leo. Hakukuacha jana. Alikuacha kitambo. Muda mrefu kabla hujagundua. Alianza kuondoka taratibu, polepole, hadi siku ile alipokusimamia kwa macho baridi macho makavu na kukuambia "hatuwezi kuendelea hivi." Lakini ukweli ni kwamba, siku hiyo ilikuwa mwisho kwa upande wako tu, kwa upande wake, ilikuwa ni hatua ya mwisho ya safari aliyokwishaianza mda sana .

Ulishawahi kuhisi yule mtu unayempenda anabadilika? Sauti yake ikawa baridi? Macho yake yakaacha kuwa na mwanga ule wa zamani? Mapenzi yake yakawa ni hisani badala ya hisia? Ndiyo, kaka yangu, haya yote yalikuwa ishara, lakini hukuwa tayari kuziona. Ukaziipuuza.

Nakuelewa kaka, inauma. Inauma kwa namna ambayo hutaweza kueleza kwa mtu yeyote. Ni kama kisu cha moto kinapita taratibu moyoni mwako, ukinyakua kila matumaini uliyokuwa nayo. Ni kama dunia imesimama, na wewe umetelekezwa ukiwa peke yako, ukiwauliza majirani na marafiki "Nilikosea wapi?" Lakini hakuna atakayekujibu.

Muda wa mwisho mlikuwa pamoja, uliona alivyokuwa tofauti. Hakukuchekea tena kwa furaha ile ya dhati ulioizoea. Alianza kukaa mbali. Alianza kukosa hamu ya kuwa na wewe. Kila ulipomgusa, aliinama pembeni. Kila ulipojaribu kumwambia "nakupenda," alijibu tu "Asante."

Na sasa amekwambia hadharani—yamekwisha. Mwisho.

Unataka umwambie nini ili abaki? Kwamba bado unampenda? Kwamba umebadilika? Kwamba utakuwa bora zaidi? Haijalishi, kaka. Haijalishi. Moyo wake umeshakufa ndani yako. Hisia zake zimezikwa. Huwezi kufufua mfu.

Labda amepata mwingine, mtu anayempa kile ulichoshindwa kumpa. Labda alishapata yote aliyohitaji kutoka kwako, na sasa huna maana tena. Au labda, amechoka tu, na hakuna unachoweza kufanya kumrudisha.

Inauma sana. Inavunja moyo. Inakufanya ujihisi mdogo, mnyonge, duni, asiye na thamani. Utabaki ukikumbuka sauti yake, harufu yake, mguso wake, kicheko chake
vyote vikitesa nafsi yako kwa kukukumbusha kuwa si vyako tena.

Lakini kaka… japo inauma, japo machozi yanakufunika macho, japo moyo unataka kupasuka, lazima ukubali. Huwezi kumbembeleza arudi. Huwezi kumlazimisha akupende tena. Mtu akikupoteza, usijipoteze na wewe pia.

Siku moja, utapona. Lakini kwa sasa, lia. Lia mpaka machozi yaishe. Umia mpaka uchoke. Lakini usirudi nyuma. Kwa sababu kilichokufa hakiwezi kufufuka.

Imekwisha. Mwisho. Piga moyo konde, maisha yanaendelea.

ibn kimweri.

Kwani ana thamani gani? That's the problem? Mnatafsiri upumbavu wa online kuwapa hawa watu mailage zisizo na maana, akienda naoungukiwa Nini????
 
Back
Top Bottom