Mwanamke aliniharibia kabisa maisha yangu, hawa viumbe hatari sana

Unakuta mwanamke anafanya kazi hachangii hata kumi nyumbani nampaka hela ya mafuta anaomba, huu ni ubinafsi wa hali ya juu. Mtu kama huyo ambaye hajazoea kuchangia majukumu ya familia siku mume akichacha lazima atamkimbia maana amezoea kuhudumiwa kwa kila kitu.

Mimi huo ukupe siutaki kabisa
Baba yangu alikuwa mwalimu, na mama alikuwa anafanya biashara ndogo ndogo, lakini tuliona mchango mkubwa sana wa mama. Yeye suala la mboga na mahitaji madogo madogo ilikuwa juu yake, baba yeye mausala ya ada na chakula kingine . Tumekuwa na hiyo dhana ya kujitegemea. Dada zangu wote walianza na waume wao wakiwa na hali ya chini kabisa , lakini walihakikisha wanachangia kwenye ustawi wa familia mpaka leo hii. Na wana maisha safi kabisa.

Mimi tu ndie nilipata bahati mbaya nikaangukia kwa gumegume.
 
Pole sana, nimeisoma huku maumivu yakiniingia kama mimi ndio wewe vile.

Mtu umemtoa shimoni then anakuacha ukijikwaa bila kukuinua.

Hongera sana kwa kupambana na kuinuka tena. Mungu akutangulie.
 
Sasa mwanamke asingesomba kila kiti ndani jamaa angepata pa kuanzia
 
Sijaona alichokufsnyia mwanamke hapo, kwanza, ulipoteza kazi, then ndio mwanamke akaanza vituko,akaondoka, sasa hapo bro! Chanzo sio mwanamke! Aliyoyafsnya ni matokeo ya wewe kupoteza kazi!
Angefanya vitu ambavyo vingeperekea wewe kuyumba hapo sawa, mfano, unamsomesha, anamaliza, anakimbia nyumba, anachukuliwa na njemba nyingine, na unagundua hata mtoto sio wako, unachanganyikiwa, ufanisi kazini unashuka! Then unapoteza kazi!
Lakini ulianza kupoteza kazi, mengine yakafata,sasa ulitegemea ni ni? Sio binadamu wote wanavumili shida, mi Bora Yule atakae nikimbia akaniachia watoto, kuliko abaki, aendelee kunisimanga, huku anapigwa pipe na wenye mishiko Yao kitaa,
 
Sijui hata nikuite jina gani baya
 
Dah gume gume sio mchezo mkuu, mwanamke lazma awe na mchango kiuchumi na kijamii katika kukuza na kuendeleza kizazi cha familia husika.

Kuendekeza ubinafsi ndio kunaua dhana nzima ya ndoa. Mtu kujifanya yeye ni malkia eti alishwe avishwe na kupewa hela by 100% bila yeye ku engage kwa namna yeyote ndio kunaleta matatizo endapo sponsor mrija wa hela ukikata.

Ukiwa na vyanzo na neema hela haisumbui utaona maisha marahisi sana na unaweza oa mke yeyote tu ambaye macho yako yanavutiwa naye ila ukiwaza deep juu ya maisha yajayo utakuwa very keen kuchagua mwanamke ambaye ni sahihi kwa shida na raha na malezi bora ya watoto wako. Kwa bahati mbaya wengi hili wanaligundua mambo yakishaharibika.
 
Huko mbele sitakuwa na muda mzuri kusoma michango yote.Ila kwanza nakupa pole na nakusifu kwa namna ulivyo na ufasaha wa kueleza kisa kirefu kwa njia nyepesi na kueleweka.
Kwa mtiririko uliokuja nao naamini mkasa wako kwa asilimia 95.Ama kuhusu wanawake ni kuwa kwa asilimia 90 huwa wanafanana katika kupenda mafanikio tu na kuwa ni wepesi wa kusahau inapokuja shida.Matusi na fedheha na vitisho ni kitu cha kawaida.
Jambo zuri kwako ni kuwa ulibaki na uhusiano mzuri na familia yako yaani wazazi wako na wao wakawa ni watu wa busara.Kama ingekuwa hukuwa na ukaribu na wazazi basi ungekuwa mwehu moja kwa moja,
Sasa nikuoneshe ulipokosea.Japo hukusema matatizo ya kazini kwako ni yepi lakini inaonekana huna uaminifu sana kazini kwako na ni mtu unayependa rushwa na huenda kwa mtindo wa rushwa uliwahi kudhulumu haki za wengine.Yale yaliyokupata ni matokeo ya masononeko ya uliowadhulumu.
Jengine ulianza mahusiano mabaya na huyo mke wako.Nimepata jibu la dini yako ni ipi.Ili upate baraka na utulivu kwenye ndoa basi usimguse mwenzako mpaka ndoa imeshafungwa.
Huko kazini uliko sasa jitahidi sana kuwa na uhusiano mzuri na wakubwa wako wa kazi.Na ukiona mwengine atakayekupendeza au atakayekufuata kijanja kwa kukupenda(hili la kufatwa na wanawake miaka hii ni maarufu sana) hata akiwa mzuri vipi fuata taratibu za kufunga naye ndoa kwanza.
Nakutakia maisha mema na mwisho mwema.
 
Hahahahahah mzee baba hio phrase ilikukong'oli kwelo kwelo kunako mtima 🤣
 
Ambaye hajawahi kuishi na mwanamke akiwa na dhiki hawezi elewa. Ile mikauli ya kejeli na dharau na kukuona kama ng'ombe tu hizo ni kwa uchache tu akichafukwa zaidi anaweza enda hata kutombesha mkoani huko kwa safari zisizo na kichwa wala miguu na hutakiwi kuuliza kitu 🤣🤣🤣
Hao wanao achana nao hawakupitia michakato?

Mwanamke ni kiumbe kingine likija suala la kuyumba kiuchumib
 
Hili sio geni na nikupongeze kwa kuwa mtu mwenye bahati sana sababu wanawake wameumbiwa uvumilivu ila kwa kizazi cha facebook hiki ni ngumu sana mwanamke kuvumilia shida.

Wanawake wako very exposed na utanadawazi na starehe kiasi kwamba sign yeyote inayoashiria starehe inaelekea tamati huwa inawavuruga kishenzi. Sign mojawapo ni kusikia sponsor kafukuzwa kazi yani, hapo maana yake hela hamna tena na bata zimekufa. 🤣
 
Haswaa. Kama mtu amepata mtu wa kula naye mkate na maji basi ashukuru
 
Naunga mkono hoja yako mkuu 100%
 
Pole sana chief na hongera kwa kusimama tena.

Ila huyo mwanao usimtelekeze ukamsahau kabisa kabisa, bado atahitaji msaada wa baba yake kipindi kijacho.
Kilichoharibu maisha yako ni kufukuzwa kazi. Hayo mengine ni matokeo tu
Word....
Kilicho kuharibua maisha siyo mwanamke ni kukosa kipato.
Word.....
 
Mkuu umeeleweka kabisa. Ila tu kuhusu kazini nilieleza kwenye comments, team members walitaka tupige deal. Sikutaka kuwa sehemu ya mpango huo, walio ya tu nisije kuwareport maana endapo ingejulikana basi moja kwa moja ningekuwa ni mimi nimevujisha kwakuwa sikuwa sehemu ya mpango wao.

Bahati mbaya kwenye tathmini ya ofisi ilikuja kuonekana loss ya kutosha na imetokea kwenye team yetu. Moja kwa moja maboss hawakutaka kuelewa utetezi wangu kama sijahusika. Hapo ndipo msala ulipoanzia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…