Mwanamke anaposema "Mwanaume wake haeleweki" anamaanisha moja kati ya haya

Ushauri wako xaxa tufanyeje manaa mim nimeacha mademu weng sababu ya kigeugeu

Tafuta wakumpenda na uishi naye kama Mwanaume.

Huwezi kubadili ugeugeu wao. Huo ndio uanamke wenyewe.

Hata mwanaume ukimuona ni Kigeugeu ujue anahulka ya kike.

Na Mwanamke ukiomuona anamsimamo ujue anahulka ya kiume
 
Wise man once said:

Kwa wanaume: Historia ya mwanamke wako kabla yako ni muhimu sana kujua wapi alipotokea.

Kwa wanawake: Future ya mwanamme wako ni muhimu sana kujua wapi anakoelekea.

Ncha Kali.
History ya wanawake wengine ni ngumu sana nyingine hazibebeki
 
Ijumaa Kareem!

Moja ya sababu zinazofanya mwanamke amuache mwanaume kimahusiano ni pamoja na "kutoeleweka Kwa Mwanaume". Bila Shaka ulishawahi kusikia Kauli Kama hizi Kwa wanawake, wakisema mwanaume Yule haeleweki, mume wake haeleweki, mchumba wake haeleweki.

Haya ni baadhi ya mambo yanayomaanishwa na wanawake wasemapo Kauli hiyo.

1. Umeshindwa kumfanya ajione yupo peke yake moyoni mwako. Yaani hana uhakika yeye ndio utamuoa.

2. Kipato chako anashindwa kukikadiria. Hajui unafanya shughuli gani hasa inayokuingizia kipato. Hivyo hana uhakika na huduma utakazompa pindi utakapomuoa.
Kumbuka Mwanamke anahitaji Security.
Security yake ya Kwanza ni Kupendwa yeye pekeake. Pili, kuhudumiwa na kutunzwa.

3. Kutoa ahadi lakini unashindwa kuzitimiza.
Wanawake hupenda kukujaribu kwenye ahadi. Huweza kukuuliza; Baby utaninunulia Mkoba Kama ule wa Doreen, ni elfu 60 tuu.
Utajibu, atakuuliza lini, utajibu. Basi atasubiri hiyo siku. Ukishindwa kutimiza ahadi za namna hiyo zaidi ya tatu nne atasema haueleweki.

Kumbuka wanawake huwaelewa wanaume wanaotimiza ahadi hasahasa ahadi ndogondogo kwani kupitia kutimiza ahadi kunamfanya akuamini na azidi kukupenda.

Kwa mwanamke ni Bora usimuahidi kuliko utoe ahadi usitimize kwake analichukulia Kama Deni.

4. Kupoteza kumbukumbu.
Mwanaume anayepoteza kumbukumbu Kwa mwanamke huwa hamuelewi. Wanawake hawawaelewi wanaume wanaopoteza kumbukumbu hasa zile za muhimu kama birthday zao, au Jambo Fulani mliopatana.
Mwanamke anaona mwanaume anayepoteza kumbukumbu Hajali na sio responsible Man.

5. Kutoa Kauli za kumtisha.
Kauli Kama, ondoka kwenu, nitakupa talaka, nitaongeza mke mwingine n.k.
Wanawake huamini maneno zaidi kuliko hata matendo.
Mwanamke hawawaelewi wanaume wanaowatisha kuwa wanasema kweli au wanatabia na kuwatisha tuu.
Kadiri unavyomtisha mwanamke unamtengezea mazingira ya kujihami na kujiandaa Kwa lolote. Tena hata usipomfukuza anaweza kujipanga kuondoka mwenyewe wakati unamhitaji.

Wanawake hawapendi kuishi na mtu wasiyemuelewa. Wanaona usalama wao ni mdogo.

Hata hivyo mwanamke hapendi kumuelewa mwanaume Kwa baadhi ya mambo. Hasa Ratiba zake, maamuzi yake endapo litatokea Jambo la hatari kwenye familia.

Taikon niishie hapa.
kuna mwanamke anasema nina fake promise wakati honestly not hua nasahau tu😀
 
Sasa hivi watu tuna mambo mengi bhana,tuwaze namna ya kupambana na Umasikini,kukabiliana na gharama za maisha zilizo panda,n.k.Tena uniongezee na kazi ya kukumbuka tarehe ya kuzaliwa kwa mtu mzima, wakati Mimi mwenyewe tarehe yangu ya kuzaliwa huwa ninaisahau.Bora aniite Mwanaume nisiyeeleweka lkn hiyo kazi siwezi kuifanya.
 
Na huwezi pambana na umasikini Kwa kuwa na Mwanamke Masikini
 
Back
Top Bottom